Sura ya 89 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Fajr (Alfajiri)

سُورَةُ الفَجۡرِ
Aya 30

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلْفَجْرِ
Naapa kwa alfajiri! [1]
Maelezo ya chini[1] Naapa kwa mwangaza wa asubuhi unapo ufukuza usiku.
Kiungo 89:1
2
وَلَيَالٍ عَشْرٍۢ
Na kwa masiku kumi! [2]
Maelezo ya chini[2] Na kwa masiku kumi yaliyo tukuzwa na Mwenyezi Mungu. (Na hayo ni masiku kumi ya mwanzo wa Mwezi wa Alhaj, Mfungo Tatu).
Kiungo 89:2
3
وَٱلشَّفْعِ وَٱلْوَتْرِ
Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja! [3]
Maelezo ya chini[3] Na shafi' yaani hisabu inayo gawika kwa mbili, kama 4, 6, 8 n.k. na witri, yaani isiyo gawika kwa mbili, kama 1, 3, 5 n.k. katika kila kitu.
Kiungo 89:3
4
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَسْرِ
Na kwa usiku unapo pita! [4]
Maelezo ya chini[4] Na kwa usiku unapo pita kwa kwenda ulimwengu kwa namna ya ajabu.
Kiungo 89:4
5
هَلْ فِى ذَٰلِكَ قَسَمٌۭ لِّذِى حِجْرٍ
Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? [5]
Maelezo ya chini[5] Je! Katika vitu vilivyo tajwa vinavyo onekana kwa akili hapana kiapo cha kukinaisha?
Kiungo 89:5
6
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di? [6]
Maelezo ya chini[6] Kwani hujui jinsi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake kaumu ya Hud, ?
Kiungo 89:6
7
إِرَمَ ذَاتِ ٱلْعِمَادِ
Wa Iram, wenye majumba marefu? [7]
Maelezo ya chini[7] Watu wa Iram wenye majengo marefu?
Kiungo 89:7
8
ٱلَّتِى لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِى ٱلْبِلَـٰدِ
Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? [8]
Maelezo ya chini[8] Ambayo haikupata kujengwa mfano wake kwa umadhubuti na ujenzi katika nchi.
Kiungo 89:8
9
وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُوا۟ ٱلصَّخْرَ بِٱلْوَادِ
Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni? [9]
Maelezo ya chini[9] Kwani hukujua jinsi Mola wako Mlezi alivyo teremsha adhabu yake kwa Thamudi, kaumu ya Saleh, walio chonga majabali kujengea nyumba zao huko bondeni?
Kiungo 89:9
10
وَفِرْعَوْنَ ذِى ٱلْأَوْتَادِ
Na Firauni mwenye vigingi? [10]
Maelezo ya chini[10] Au kwani hukujua vipi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake Firauni mwenye majeshi yaliyo upa nguvu ufalme wake kama vigingi vinavyo simamisha makhema?
Kiungo 89:10
11
ٱلَّذِينَ طَغَوْا۟ فِى ٱلْبِلَـٰدِ
Ambao walifanya jeuri katika nchi? [11]
Maelezo ya chini[11] Ambao walipita mipaka katika nchi?
Kiungo 89:11
12
فَأَكْثَرُوا۟ فِيهَا ٱلْفَسَادَ
Wakakithirisha humo ufisadi? [12]
Maelezo ya chini[12] Na wakazidisha kufanya uharibifu kwa ukafiri na udhalimu?
Kiungo 89:12
13
فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ
Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. [13]
Maelezo ya chini[13] Basi Mola wako Mlezi aliwateremshia adhabu kali ya kuwaunguza.
Kiungo 89:13
14
إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلْمِرْصَادِ
Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia. [14]
Maelezo ya chini[14] Hakika Mola wako Mlezi anaviangalia vitendo vya watu, na anawahisabia, na atakuja kuwalipa kwavyo.
Kiungo 89:14
15
فَأَمَّا ٱلْإِنسَـٰنُ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكْرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَكْرَمَنِ
Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! [15]
Maelezo ya chini[15] Ama mtu akijaribiwa na Mola wake Mlezi na akamkirimu, na akamneemesha kwa mali na cheo na nguvu, basi husema kwa kughurika na hayo: Mola wangu Mlezi amenitukuza kwa kuwa ninastahiki haya!
Kiungo 89:15
16
وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَهَـٰنَنِ
Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge! [16]
Maelezo ya chini[16] Na pindi Mola wake Mlezi akimjaribu mtu kwa kumdhikisha riziki, basi hughafilika na hikima ya hayo na husema: Mola wangu Mlezi kanidhalilisha!
Kiungo 89:16
17
كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ ٱلْيَتِيمَ
Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, [17]
Maelezo ya chini[17] Wacheni mtindo huo! Mambo siyo hayo kama msemavyo; bali nyinyi hamumkirimu yatima;
Kiungo 89:17
18
وَلَا تَحَـٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ
Wala hamhimizani kulisha masikini; [18]
Maelezo ya chini[18] Wala hamhimizani kuwalisha masikini;
Kiungo 89:18
19
وَتَأْكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكْلًۭا لَّمًّۭا
Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, [19]
Maelezo ya chini[19] Na mnakula mali ya urithi kwa pupa, hamchagui linalo faa na lisilo faa.
Kiungo 89:19
20
وَتُحِبُّونَ ٱلْمَالَ حُبًّۭا جَمًّۭا
Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. [20]
Maelezo ya chini[20] Na mnayapenda mali mno, yanayo kupelekeeni kupapatika katika kuyakusanya na ubakhili wa kuyatumia.
Kiungo 89:20
21
كَلَّآ إِذَا دُكَّتِ ٱلْأَرْضُ دَكًّۭا دَكًّۭا
Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, [21]
Maelezo ya chini[21] Wacheni vitendo hivyo! Kwani inakungojeeni siku itapo lazwa ardhi iwe sawa sawa,
Kiungo 89:21
22
وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلْمَلَكُ صَفًّۭا صَفًّۭا
Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, [22]
Maelezo ya chini[22] Na aje Mola wako Mlezi kama anavyo stahiki kuja kwake Subhanahu na Malaika waje kwa safu safu;
Kiungo 89:22
23
وَجِا۟ىٓءَ يَوْمَئِذٍۭ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍۢ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَـٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكْرَىٰ
Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? [23]
Maelezo ya chini[23] Na siku hiyo iletwe Jahannamu, nyumba ya adhabu, siku hiyo yatapo tokea hayo mwanaadamu atakumbuka aliyo yaharibu - lakini wapi! Kukumbuka huko kumfae nini, na wakati umekwisha pita?
Kiungo 89:23
24
يَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى قَدَّمْتُ لِحَيَاتِى
Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu! [24]
Maelezo ya chini[24] Atasema kwa majuto: Laiti ningeli jitangulizia katika dunia vitendo vyema vya kunifaa katika maisha ya Akhera!
Kiungo 89:24
25
فَيَوْمَئِذٍۢ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٌۭ
Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. [25]
Maelezo ya chini[25] Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
Kiungo 89:25
26
وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٌۭ
Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. [26]
Maelezo ya chini[26] Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
Kiungo 89:26
27
يَـٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفْسُ ٱلْمُطْمَئِنَّةُ
Ewe nafsi iliyo tua! [27]
Maelezo ya chini[27] Ewe nafsi uliye tulia juu ya Haki!
Kiungo 89:27
28
ٱرْجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةًۭ مَّرْضِيَّةًۭ
Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. [28]
Maelezo ya chini[28] Rejea kwenye radhi ya Mola wako Mlezi nawe uradhi kwa neema ulio pewa, nawe umemridhisha kwa a'mali uliyo ikadimisha.
Kiungo 89:28
29
فَٱدْخُلِى فِى عِبَـٰدِى
Basi ingia miongoni mwa waja wangu, [29]
Maelezo ya chini[29] Basi ingia katika kundi la waja wangu walio wema!
Kiungo 89:29
30
وَٱدْخُلِى جَنَّتِى
Na ingia katika Pepo yangu. [30]
Maelezo ya chini[30] Na ingia katika Pepo yangu, nyumba ya neema ya milele!
Kiungo 89:30

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure