Sura ya 82 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Infitar (Kupasuka)

سُورَةُ الانفِطَارِ
Aya 19

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتْ
Mbingu itapo chanika! [1]
Maelezo ya chini[1] Itakapo pasuka mbingu,
Kiungo 82:1
2
وَإِذَا ٱلْكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتْ
Na nyota zitapo tawanyika! [2]
Maelezo ya chini[2] Na nyota zitakapo pukutika na kutawanyika,
Kiungo 82:2
3
وَإِذَا ٱلْبِحَارُ فُجِّرَتْ
Na bahari zitakapo pasuliwa! [3]
Maelezo ya chini[3] Na bahari zikafurika na kuingiliana kwa kuondoka viziwizi baina yao,
Kiungo 82:3
4
وَإِذَا ٱلْقُبُورُ بُعْثِرَتْ
Na makaburi yatapo fukuliwa! [4]
Maelezo ya chini[4] Na makaburi yakafunuliwa na wakatoka maiti walio kuwamo,
Kiungo 82:4
5
عَلِمَتْ نَفْسٌۭ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. [5]
Maelezo ya chini[5] Hapo basi kila nafsi itajua nini kheri au shari iliyo tanguliza na iliyo chelewesha.
Kiungo 82:5
6
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَـٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلْكَرِيمِ
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? [6]
Maelezo ya chini[6] Ewe mwanaadamu! Kitu gani kilicho kukhadaa wewe na Mola wako Mlezi Mtukufu hata ukafanya jeuri ya kwenda kumuasi? (Ni dhaahiri kuwa Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir aliye tunga utenzi wa Kiswahili maarufu uitwao Al Inkishaf aliiwaza Aya hii alipo tunga ubeti huu: Moyo wangu nini huzundukani Likughurielo hela ni nni? Hunelezi nami kalibaini Liwapo na sura nisikataye )
Kiungo 82:6
7
ٱلَّذِى خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha! [7]
Maelezo ya chini[7] Mungu wako huyo ndiye aliye kuumba nawe hukuwa chochote, akakuumba na viungo vya kukuletea manufaa, akakufanya umenyooka kwa umbo sawa sawa.
Kiungo 82:7
8
فِىٓ أَىِّ صُورَةٍۢ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. [8]
Maelezo ya chini[8] Akakujenga na akakuleta katika sura yoyote aliyo itaka.
Kiungo 82:8
9
كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. [9]
Maelezo ya chini[9] Hamwachi? Bali nyinyi mnakadhibisha malipo ya Siku ya Kiyama!
Kiungo 82:9
10
وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَـٰفِظِينَ
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, [10]
Maelezo ya chini[10] Na hakika wapo juu yenu Malaika walinzi, ambao ni waheshimiwa kwetu,
Kiungo 82:10
11
كِرَامًۭا كَـٰتِبِينَ
Waandishi wenye hishima, [11]
Maelezo ya chini[11] Wanasajili vitendo vyenu vyote mvitendavyo, vya kheri na shari.
Kiungo 82:11
12
يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ
Wanayajua mnayo yatenda. [12]
Maelezo ya chini[12] Wanayajua mnayo yafanya ya kheri na ya shari
Kiungo 82:12
13
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍۢ
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, [13]
Maelezo ya chini[13] Hakika wale walio ni wa kweli katika Imani yao wapo katika neema kubwa.
Kiungo 82:13
14
وَإِنَّ ٱلْفُجَّارَ لَفِى جَحِيمٍۢ
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; [14]
Maelezo ya chini[14] Na hakika walio iacha amri ya Mwenyezi bila ya shaka watakuwa katika Moto unao unguza,
Kiungo 82:14
15
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ ٱلدِّينِ
Wataingia humo Siku ya Malipo. [15]
Maelezo ya chini[15] Wataingia humo Siku ya Malipo.
Kiungo 82:15
16
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَآئِبِينَ
Na hawatoacha kuwamo humo. [16]
Maelezo ya chini[16] Na wala hawatatoka katika Jahannamu!
Kiungo 82:16
17
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? [17]
Maelezo ya chini[17] Na nini kitakujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo, na mambo yake yamepindukia ujuzi wako na fikra zako?
Kiungo 82:17
18
ثُمَّ مَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? [18]
Maelezo ya chini[18] Tena ni nini kitacho kujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo kwa vitisho vyake na shida zake?
Kiungo 82:18
19
يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌۭ لِّنَفْسٍۢ شَيْـًۭٔا ۖ وَٱلْأَمْرُ يَوْمَئِذٍۢ لِّلَّهِ
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. [19]
Maelezo ya chini[19] Siku ambayo nafsi haitakuwa na mamlaka yoyote juu ya nafsi ya kuifaa au kuidhuru; na amri yote siku hiyo itakuwa ni ya Mwenyezi Mungu peke yake!
Kiungo 82:19

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure