Sura ya 83 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Mutaffifin (Wapunjaji)

سُورَةُ المُطَفِّفِينَ
Aya 36

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَيْلٌۭ لِّلْمُطَفِّفِينَ
Ole wao hao wapunjao! [1]
Maelezo ya chini[1] Wataangamia wanao punja,
Kiungo 83:1
2
ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكْتَالُوا۟ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسْتَوْفُونَ
Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. [2]
Maelezo ya chini[2] Ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi,
Kiungo 83:2
3
وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ
Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. [3]
Maelezo ya chini[3] Na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!
Kiungo 83:3
4
أَلَا يَظُنُّ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ
Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa . [4]
Maelezo ya chini[4] Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa,
Kiungo 83:4
5
لِيَوْمٍ عَظِيمٍۢ
Katika Siku iliyo kuu! [5]
Maelezo ya chini[5] Katika siku ya vitisho vikuu?
Kiungo 83:5
6
يَوْمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? [6]
Maelezo ya chini[6] Siku watapo simama watu kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote na hukumu yake?
Kiungo 83:6
7
كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلْفُجَّارِ لَفِى سِجِّينٍۢ
Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. [7]
Maelezo ya chini[7] Wacheni kupunja, na kughafilika na kufufuliwa! Kwani hakika waliyo andikiwa wakosefu katika a'mali zao mbovu, bila ya shaka yamo katika Sijjin.
Kiungo 83:7
8
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا سِجِّينٌۭ
Unajua nini Sijjin? [8]
Maelezo ya chini[8] Na nini kitakujuvya nini hiyo Sijjin?
Kiungo 83:8
9
كِتَـٰبٌۭ مَّرْقُومٌۭ
Kitabu kilicho andikwa. [9]
Maelezo ya chini[9] Hicho ni Kitabu kilicho pigwa mistari baina ya maandishi yake.
Kiungo 83:9
10
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! [10]
Maelezo ya chini[10] Wataangamia wanao kadhibisha siku itapo kuwa kufufuliwa na kuhisabiwa.
Kiungo 83:10
11
ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ
Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. [11]
Maelezo ya chini[11] Ambao wanaikanusha Siku ya Malipo.
Kiungo 83:11
12
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ
Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. [12]
Maelezo ya chini[12] Na wala haikanushi Siku ya Malipo ila kila mwenye kupindukia mipaka mwingi wa madhambi.
Kiungo 83:12
13
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَـٰتُنَا قَالَ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! [13]
Maelezo ya chini[13] Na akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu zenye kutaja kuwepo malipo husema: Huo ni uwongo wa walio tangulia!
Kiungo 83:13
14
كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. [14]
Maelezo ya chini[14] Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.
Kiungo 83:14
15
كَلَّآ إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍۢ لَّمَحْجُوبُونَ
Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. [15]
Maelezo ya chini[15] Hakika ni kweli kuwa hao wanao kadhibisha watazuiliwa siku hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya maasi waliyo yachuma.
Kiungo 83:15
16
ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُوا۟ ٱلْجَحِيمِ
Kisha wataingia Motoni! [16]
Maelezo ya chini[16] Kisha hakika hao bila ya shaka wataingia Motoni.
Kiungo 83:16
17
ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. [17]
Maelezo ya chini[17] Kisha wataambiwa kwa kuwakebehi: Hii basi ndiyo adhabu inayo kuteremkieni ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani!
Kiungo 83:17
18
كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلْأَبْرَارِ لَفِى عِلِّيِّينَ
Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. [18]
Maelezo ya chini[18] Ni hakika kuwa vitendo vya watu wema bila ya shaka vimeandikwa katika I'liyyin.
Kiungo 83:18
19
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? [19]
Maelezo ya chini[19] Na nini cha kukujuvya nini I'liyyin?
Kiungo 83:19
20
كِتَـٰبٌۭ مَّرْقُومٌۭ
Kitabu kilicho andikwa. [20]
Maelezo ya chini[20] Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake,
Kiungo 83:20
21
يَشْهَدُهُ ٱلْمُقَرَّبُونَ
Wanakishuhudia walio karibishwa. [21]
Maelezo ya chini[21] Wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.
Kiungo 83:21
22
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍ
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. [22]
Maelezo ya chini[22] Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi,
Kiungo 83:22
23
عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. [23]
Maelezo ya chini[23] Juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.
Kiungo 83:23
24
تَعْرِفُ فِى وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ ٱلنَّعِيمِ
Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, [24]
Maelezo ya chini[24] Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.
Kiungo 83:24
25
يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍۢ مَّخْتُومٍ
Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, [25]
Maelezo ya chini[25] Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa;
Kiungo 83:25
26
خِتَـٰمُهُۥ مِسْكٌۭ ۚ وَفِى ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ ٱلْمُتَنَـٰفِسُونَ
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. [26]
Maelezo ya chini[26] Kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.
Kiungo 83:26
27
وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسْنِيمٍ
Na mchanganyiko wake ni Tasniim, [27]
Maelezo ya chini[27] Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi,
Kiungo 83:27
28
عَيْنًۭا يَشْرَبُ بِهَا ٱلْمُقَرَّبُونَ
Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. [28]
Maelezo ya chini[28] Nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.
Kiungo 83:28
29
إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ كَانُوا۟ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يَضْحَكُونَ
Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. [29]
Maelezo ya chini[29] Wale walio kuwa wakibeba madhambi kuipingia Dini walikuwa wakiwacheka kuwakejeli Waumini duniani.
Kiungo 83:29
30
وَإِذَا مَرُّوا۟ بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ
Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. [30]
Maelezo ya chini[30] Na wakipita Waumini mbele yao basi wao hukonyezana kwa kuwabeza.
Kiungo 83:30
31
وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمُ ٱنقَلَبُوا۟ فَكِهِينَ
Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. [31]
Maelezo ya chini[31] Na hao wakosefu wakirejea kwa ahali zao hurejea kwa furaha na kuona ladha kwa vile kuwakejeli Waumini.
Kiungo 83:31
32
وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوٓا۟ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. [32]
Maelezo ya chini[32] Na wakiwaona Waumini husema: Ama hakika hawa wamepotea kweli kwa kumuamini Muhammad.
Kiungo 83:32
33
وَمَآ أُرْسِلُوا۟ عَلَيْهِمْ حَـٰفِظِينَ
Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. [33]
Maelezo ya chini[33] Wala hao wakosefu hawakutumwa wawe wa kuwahukumu Waumini kwa kuwaongoza au kuwapoteza, wala kuwa ni walinzi wa vitendo vyao.
Kiungo 83:33
34
فَٱلْيَوْمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنَ ٱلْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ
Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, [34]
Maelezo ya chini[34] Basi Siku ya Malipo walio amini watakuwa ndio wa kuwacheka hao makafiri kwa kuwalipizia kile kicheko chao na kejeli yao ya duniani.
Kiungo 83:34
35
عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. [35]
Maelezo ya chini[35] Ilhali wako juu ya vitanda na matakia watakuwa Waumini wakiziangalia neema za Mwenyezi Mungu alizo wapa.
Kiungo 83:35
36
هَلْ ثُوِّبَ ٱلْكُفَّارُ مَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ
Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda? [36]
Maelezo ya chini[36] Je! Makafiri watalipwa huko Akhera kwa waliyo yatenda duniani?
Kiungo 83:36

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure