Sura ya 80 kati ya 114 · Makkiya

Sura Abasa (Alikunja Uso)

سُورَةُ عَبَسَ
Aya 42

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ
Alikunja kipaji na akageuka! [1]
Maelezo ya chini[1] Uso wake ulitaghayari kwa kuchukia na akageuka,
Kiungo 80:1
2
أَن جَآءَهُ ٱلْأَعْمَىٰ
Kwa sababu alimjia kipofu! [2]
Maelezo ya chini[2] Kwa sababu kamjia kipofu anamuuliza khabari ya Dini yake.
Kiungo 80:2
3
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? [3]
Maelezo ya chini[3] Na wewe unajuaje, pengine huyo kipofu atatakasika kwa atayo yapata kwako,
Kiungo 80:3
4
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكْرَىٰٓ
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? [4]
Maelezo ya chini[4] Au atawaidhika na mawaidha yamfae.
Kiungo 80:4
5
أَمَّا مَنِ ٱسْتَغْنَىٰ
Ama ajionaye hana haja! [5]
Maelezo ya chini[5] Ama yule anaye jiona ametosheka kwa mali yake na nguvu zake,
Kiungo 80:5
6
فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ
Wewe ndio unamshughulikia? [6]
Maelezo ya chini[6] Wewe ndio unamkabili na unamshughulikia kumfikishia wito wako.
Kiungo 80:6
7
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ
Na si juu yako kama hakutakasika. [7]
Maelezo ya chini[7] Na wewe una lawama gani ikiwa yeye hakutakasika kwa Imani?
Kiungo 80:7
8
وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسْعَىٰ
Ama anaye kujia kwa juhudi . [8]
Maelezo ya chini[8] Ama anaye kukimbilia kutafuta ilimu na uwongofu,
Kiungo 80:8
9
وَهُوَ يَخْشَىٰ
Naye anaogopa! [9]
Maelezo ya chini[9] Naye anamkhofu Mwenyezi Mungu .
Kiungo 80:9
10
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ
Ndio wewe unampuuza? [10]
Maelezo ya chini[10] Wewe unampuuza.
Kiungo 80:10
11
كَلَّآ إِنَّهَا تَذْكِرَةٌۭ
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. [11]
Maelezo ya chini[11] Hakika Aya hizi ni mawaidha.
Kiungo 80:11
12
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Basi anaye penda akumbuke. [12]
Maelezo ya chini[12] Mwenye kutaka atawaidhika kwa Qur'ani.
Kiungo 80:12
13
فِى صُحُفٍۢ مُّكَرَّمَةٍۢ
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, [13]
Maelezo ya chini[13] Nayo Qur'ani imo katika kurasa zilizo tukuzwa kwa Mwenyezi Mungu,
Kiungo 80:13
14
مَّرْفُوعَةٍۢ مُّطَهَّرَةٍۭ
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. [14]
Maelezo ya chini[14] Zina cheo cha juu, na pahala palipo tukuka, zimetakasika na kila upungufu.
Kiungo 80:14
15
بِأَيْدِى سَفَرَةٍۢ
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, [15]
Maelezo ya chini[15] Katika mikono ya Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewafanya ndio mabalozi baina yake na Mitume wake;
Kiungo 80:15
16
كِرَامٍۭ بَرَرَةٍۢ
Watukufu, wema. [16]
Maelezo ya chini[16] Walio bora, wema.
Kiungo 80:16
17
قُتِلَ ٱلْإِنسَـٰنُ مَآ أَكْفَرَهُۥ
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? [17]
Maelezo ya chini[17] Ameangamia mwanaadamu! Nini kilicho mfanya akufuru na hali Mwenyezi Mungu amemfanyia hisani zote hizi?
Kiungo 80:17
18
مِنْ أَىِّ شَىْءٍ خَلَقَهُۥ
Kwa kitu gani amemuumba? [18]
Maelezo ya chini[18] Hakumbuki yeye kaumbwa kutokana na nini?
Kiungo 80:18
19
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. [19]
Maelezo ya chini[19] Kutokana na maji ya kudharauliwa Yeye Mwenyezi Mungu alimwanzisha kumuumba akamjaalia apitie daraja mbali mbali za kukua.
Kiungo 80:19
20
ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ
Kisha akamsahilishia njia. [20]
Maelezo ya chini[20] Kisha akamfanyia nyepesi njia ya kufikia Imani, na akamfunza njia hiyo.
Kiungo 80:20
21
ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقْبَرَهُۥ
Kisha akamfisha, akamtia kaburini. [21]
Maelezo ya chini[21] Kisha akamfisha na akamtukuza kwa kumtia kaburini.
Kiungo 80:21
22
ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ
Kisha apendapo atamfufua. [22]
Maelezo ya chini[22] Na tena akipenda atamhuisha baada ya kufa kwake.
Kiungo 80:22
23
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَآ أَمَرَهُۥ
La! Hajamaliza aliyo muamuru. [23]
Maelezo ya chini[23] Ni kweli mwanaadamu, juu ya kuwa umri wake mrefu duniani, hakutimiza aliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu katika mambo ya Imani na ut'iifu.
Kiungo 80:23
24
فَلْيَنظُرِ ٱلْإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ
Hebu mtu na atazame chakula chake. [24]
Maelezo ya chini[24] Hebu mtu na aangalie shani ya chakula chake - vipi tulivyo kipanga na kumsahilishia!
Kiungo 80:24
25
اَنَّا صَبَبْنَا ٱلْمَآءَ صَبًّۭا
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, [25]
Maelezo ya chini[25] Ni Sisi tumeiteremsha mvua kutoka mbinguni, ikateremka.
Kiungo 80:25
26
ثُمَّ شَقَقْنَا ٱلْأَرْضَ شَقًّۭا
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, [26]
Maelezo ya chini[26] Tena tukaipasua pasua ardhi kwa ajili ya mimea.
Kiungo 80:26
27
فَأَنۢبَتْنَا فِيهَا حَبًّۭا
Kisha tukaotesha humo nafaka, [27]
Maelezo ya chini[27] Tukaotesha humo nafaka ambazo watu huzila na huweka akiba.
Kiungo 80:27
28
وَعِنَبًۭا وَقَضْبًۭا
Na zabibu, na mimea ya majani, [28]
Maelezo ya chini[28] Na mizabibu na mimea ya majani inayo liwa mibichi.
Kiungo 80:28
29
وَزَيْتُونًۭا وَنَخْلًۭا
Na mizaituni, na mitende, [29]
Maelezo ya chini[29] Na mizaituni mizuri, na mitende yenye kuzaa,
Kiungo 80:29
30
وَحَدَآئِقَ غُلْبًۭا
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, [30]
Maelezo ya chini[30] Na mabustani yaliyo songamana matawi ya miti yake,
Kiungo 80:30
31
وَفَـٰكِهَةًۭ وَأَبًّۭا
Na matunda, na malisho ya wanyama; [31]
Maelezo ya chini[31] Na matunda ya kustaladhi nayo, na malisha ya kula nyama hoa (mifugo).
Kiungo 80:31
32
مَّتَـٰعًۭا لَّكُمْ وَلِأَنْعَـٰمِكُمْ
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. [32]
Maelezo ya chini[32] Tumeotesha yote hayo kwa ajili ya faida yenu na wanyama wenu wa kufuga.
Kiungo 80:32
33
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ
Basi utakapo kuja ukelele, [33]
Maelezo ya chini[33] Basi utakapo kuja ukelele wa Kiyama utakao tia uziwi masikio,
Kiungo 80:33
34
يَوْمَ يَفِرُّ ٱلْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, [34]
Maelezo ya chini[34] Siku mtu atakapo mkimbia ndugu yake,
Kiungo 80:34
35
وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ
Na mamaye na babaye, [35]
Maelezo ya chini[35] Na mama yake, na baba yake,
Kiungo 80:35
36
وَصَـٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ
Na mkewe na wanawe. [36]
Maelezo ya chini[36] Na mkewe, na wanawe!
Kiungo 80:36
37
لِكُلِّ ٱمْرِئٍۢ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍۢ شَأْنٌۭ يُغْنِيهِ
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha [37]
Maelezo ya chini[37] Kila mmojapo katika hawa atakuwa na jambo lake la kumshughulisha!
Kiungo 80:37
38
وُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍۢ مُّسْفِرَةٌۭ
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, [38]
Maelezo ya chini[38] Zipo nyuso siku hii zenye mwangaza,
Kiungo 80:38
39
ضَاحِكَةٌۭ مُّسْتَبْشِرَةٌۭ
Zitacheka, zitachangamka; [39]
Maelezo ya chini[39] Zenye kung'ara na kufurahi kwa neema za Mwenyezi Mungu.
Kiungo 80:39
40
وَوُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌۭ
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, [40]
Maelezo ya chini[40] Na nyuso nyengine siku hii zina vumbi zimesawijika.
Kiungo 80:40
41
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ
Giza totoro litazifunika, [41]
Maelezo ya chini[41] Zimegubikwa na kiza na weusi.
Kiungo 80:41
42
أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَفَرَةُ ٱلْفَجَرَةُ
Hao ndio makafiri watenda maovu [42]
Maelezo ya chini[42] Wenye nyuso hizi ni makafiri wapotovu, ambao walio kuwa hawabali maasi waliyo kuwa wakiyatenda.
Kiungo 80:42

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure