Sura ya 75 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Qiyama (Kiyama)

سُورَةُ القِيَامَةِ
Aya 40

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
لَآ أُقْسِمُ بِيَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ
Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! [1]
Maelezo ya chini[1] Ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa Siku ya Kiyama, na hiyo ni kweli iliyo thibiti;
Kiungo 75:1
2
وَلَآ أُقْسِمُ بِٱلنَّفْسِ ٱللَّوَّامَةِ
Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! [2]
Maelezo ya chini[2] Na ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa nafsi inayo mlaumu mtu kwa dhambi zake na upungufu wake, ya kwamba bila ya shaka yoyote mtafufuliwa baada ya kukusanywa mafupa yenu yaliyo tawanyika.
Kiungo 75:2
3
أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَـٰنُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُۥ
Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? [3]
Maelezo ya chini[3] Hivyo mtu anadhani baada ya kuwa Sisi tulimuumba naye hakuwa kitu chochote, tutakuja shindwa kuyakusanya mafupa yake yaliyooza na yakatapanyika?
Kiungo 75:3
4
بَلَىٰ قَـٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّىَ بَنَانَهُۥ
Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! [4]
Maelezo ya chini[4] Hasha! Sisi tuna uweza wa kuviweka sawa hata vifupa vya vidole vyake vilivyo vurugika, wachilia mbali mafupa yake makubwa makubwa ya mwili wake.
Kiungo 75:4
5
بَلْ يُرِيدُ ٱلْإِنسَـٰنُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُۥ
Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake. [5]
Maelezo ya chini[5] Hivyo mtu anakanya kufufuliwa? Anataka abakie katika uasi wake katika siku zote zilizo mbakilia katika umri wake ulio salia?
Kiungo 75:5
6
يَسْـَٔلُ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلْقِيَـٰمَةِ
Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? [6]
Maelezo ya chini[6] Anauliza kwa kuona haiwezi kutokea saa ya Kiyama: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
Kiungo 75:6
7
فَإِذَا بَرِقَ ٱلْبَصَرُ
Basi jicho litapo dawaa! [7]
Maelezo ya chini[7] Jicho litapo tahayari kwa kufazaika na kushtuka,
Kiungo 75:7
8
وَخَسَفَ ٱلْقَمَرُ
Na mwezi utapo patwa! [8]
Maelezo ya chini[8] Na mwangaza wa mwezi ukapotea,
Kiungo 75:8
9
وَجُمِعَ ٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ
Na likakusanywa jua na mwezi! [9]
Maelezo ya chini[9] Na jua likakusanyika na mwezi kuchomoza magharibi,
Kiungo 75:9
10
يَقُولُ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ ٱلْمَفَرُّ
Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? [10]
Maelezo ya chini[10] Mtu hapo atasema: Yako wapi makimbilio kuikimbia hii adhabu?
Kiungo 75:10
11
كَلَّا لَا وَزَرَ
La! Hapana pa kukimbilia! [11]
Maelezo ya chini[11] Huachi, ewe mtu, kutafuta makimbilio? Leo huna pa kukimbilia wewe,
Kiungo 75:11
12
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمُسْتَقَرُّ
Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. [12]
Maelezo ya chini[12] ila kwa Mola wako Mlezi peke yake, ndipo penye matulivu ya waja, Peponi au Motoni.
Kiungo 75:12
13
يُنَبَّؤُا۟ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. [13]
Maelezo ya chini[13] Siku hiyo mtu ataambiwa vitendo vyake alivyo vitanguliza na alivyo viakhirisha.
Kiungo 75:13
14
بَلِ ٱلْإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ بَصِيرَةٌۭ
Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. [14]
Maelezo ya chini[14] Bali mtu yeye mwenyewe ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake inayo mkazania kwa anayo yatenda na anayo yaacha.
Kiungo 75:14
15
وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ
Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. [15]
Maelezo ya chini[15] Na ijapo kuwa atajitolea chungu nzima ya udhuru na akazieneza, hawezi kabisa kuepukana na hoja hizo.
Kiungo 75:15
16
لَا تُحَرِّكْ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِۦٓ
Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. [16]
Maelezo ya chini[16] Usiuharikishe ulimi wako kwa kuisoma Qur'ani na kujaribu kuihifadhi kwa haraka pale unapo teremshiwa kwa Wahyi.
Kiungo 75:16
17
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُۥ وَقُرْءَانَهُۥ
Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. [17]
Maelezo ya chini[17] Hakika ni juu yetu Sisi kuikusanya hiyo katika kifua chako, na kuithibitisha katika ulimi wako.
Kiungo 75:17
18
فَإِذَا قَرَأْنَـٰهُ فَٱتَّبِعْ قُرْءَانَهُۥ
Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. [18]
Maelezo ya chini[18] Akikusomea Mjumbe wetu (Jibril) basi nawe ifuatilize kama unavyo isikia.
Kiungo 75:18
19
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُۥ
Kisha ni juu yetu kuubainisha. [19]
Maelezo ya chini[19] Kisha baada ya hayo ni juu yetu kuibainisha ikiingia tatizo lolote juu yako.
Kiungo 75:19
20
كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ ٱلْعَاجِلَةَ
Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani, [20]
Maelezo ya chini[20] Wacheni kukanya kufufuliwa, na hilo ni jambo la kweli. Lakini nyinyi mnaipenda dunia na starehe zake,
Kiungo 75:20
21
وَتَذَرُونَ ٱلْـَٔاخِرَةَ
Na mnaacha maisha ya Akhera. [21]
Maelezo ya chini[21] Na mnaiacha Akhera na neema zake.
Kiungo 75:21
22
وُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍۢ نَّاضِرَةٌ
Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, [22]
Maelezo ya chini[22] Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani.
Kiungo 75:22
23
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌۭ
Zinamwangallia Mola wao Mlezi. [23]
Maelezo ya chini[23] Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani.
Kiungo 75:23
24
وَوُجُوهٌۭ يَوْمَئِذٍۭ بَاسِرَةٌۭ
Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. [24]
Maelezo ya chini[24] Na nyuso nyengine zitakuwapo zimenuna, zimekunjana mno, zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo.
Kiungo 75:24
25
تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌۭ
Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. [25]
Maelezo ya chini[25] Zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo.
Kiungo 75:25
26
كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِىَ
La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo, [26]
Maelezo ya chini[26] Mna nini na kuipenda dunia ambayo mnaifariki roho inapo fika katika mafupa ya kooni,
Kiungo 75:26
27
وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍۢ
Na pakasemwa: Nani wa kumganga? [27]
Maelezo ya chini[27] Na walio hudhuria wakasema: Yupo wa kumganga huyu kwa haya aliyo nayo?
Kiungo 75:27
28
وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلْفِرَاقُ
Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; [28]
Maelezo ya chini[28] Akayakinisha yule yaliyo mfika mauti kama lililo mshukia ni kuiacha dunia inayo pendwa, na imekwisha mfika shida yake kikomo cha mwisho.
Kiungo 75:28
29
وَٱلْتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ
Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, [29]
Maelezo ya chini[29] Na muundi wa mguu umekwisha ambatana na wa pili wakati wa kutoka roho.
Kiungo 75:29
30
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمَسَاقُ
Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! [30]
Maelezo ya chini[30] Kwa Mola wako Mlezi tu siku hiyo ndio machungio ya waja, ama Peponi au Motoni.
Kiungo 75:30
31
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ
Kwa sababu hakusadiki, wala hakuswali. [31]
Maelezo ya chini[31] Binaadamu amekanya kufufuliwa, na kwa hivyo hakumsadiki Mtume wala Qur'ani. Wala hakumtimizia Mwenyezi Mungu faridha za Swala.
Kiungo 75:31
32
وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Bali alikanusha, na akageuka. [32]
Maelezo ya chini[32] Lakini aliikadhibisha Qur'ani, akaipuuza Imani,
Kiungo 75:32
33
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ
Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. [33]
Maelezo ya chini[33] Na akatoka kwenda kwa watu wake wa nyumbani kwa maringo na kujitapa.
Kiungo 75:33
34
أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ
Ole wako, ole wako! [34]
Maelezo ya chini[34] Ewe unaye kadhibisha, utaangamia!
Kiungo 75:34
35
ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰٓ
Kisha Ole wako, ole wako! [35]
Maelezo ya chini[35] Tena utaangamia! Na tena utaangamia, na utaangamia!
Kiungo 75:35
36
أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَـٰنُ أَن يُتْرَكَ سُدًى
Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? [36]
Maelezo ya chini[36] Hivyo anadhani huyu mtu anaye kanya kufufuliwa kuwa ataachwa hivi hivi akiringa tu katika maisha yake, na akisha kufa iwe basi, wala asifufuliwe akahisabiwa kwa vitendo vyake?
Kiungo 75:36
37
أَلَمْ يَكُ نُطْفَةًۭ مِّن مَّنِىٍّۢ يُمْنَىٰ
Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa? [37]
Maelezo ya chini[37] Kwani yeye mtu hakuwa ni tone tu ya manii, ilio jaaliwa kuwemo katika tumbo la uzazi?
Kiungo 75:37
38
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةًۭ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ
Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. [38]
Maelezo ya chini[38] Kisha hiyo tone ikawa kipande cha damu iliyo ganda, na Mwenyezi Mungu akaiumba, akaisawazisha mpaka ikawa na umbo zuri?
Kiungo 75:38
39
فَجَعَلَ مِنْهُ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ
Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. [39]
Maelezo ya chini[39] Akajaalia namna mbili, mwanamume na mwanamke?
Kiungo 75:39
40
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحْـِۧىَ ٱلْمَوْتَىٰ
Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu? [40]
Maelezo ya chini[40] Je! Huyo Muumba wa mwanzo aliye fanya yote haya, basi si muweza wa kuwahuisha maiti baada ya kuyakusanya mafupa yao?
Kiungo 75:40

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure