Sura ya 76 kati ya 114 · Madaniya

Sura Al-Insan (Mwanadamu)

سُورَةُ الإِنسَانِ
Aya 31

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
هَلْ أَتَىٰ عَلَى ٱلْإِنسَـٰنِ حِينٌۭ مِّنَ ٱلدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْـًۭٔا مَّذْكُورًا
Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa. [1]
Maelezo ya chini[1] Hakika kimempitia mwanaadamu kipindi cha zama kabla hajapuliziwa roho, naye hata bado hakuwa ni kitu cha kutajika kwa jina lake, wala hajuulikani nini atakuwa.
Kiungo 76:1
2
إِنَّا خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍۢ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَـٰهُ سَمِيعًۢا بَصِيرًا
Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona. [2]
Maelezo ya chini[2] Hakika Sisi tumemuumba mwanaadamu naye ana sifa namna mbali mbali, kwa ajili ya kumtia mtihanini, majaribioni, baadaye. Kwa hivyo tukamjaalia awe anasikia na anaona, ili apate kuzisikia Aya na azione Ishara.
Kiungo 76:2
3
إِنَّا هَدَيْنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًۭا وَإِمَّا كَفُورًا
Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru. [3]
Maelezo ya chini[3] Hakika Sisi tumembainishia Njia ya Uwongofu, ama awe Muumini au awe kafiri.
Kiungo 76:3
4
إِنَّآ أَعْتَدْنَا لِلْكَـٰفِرِينَ سَلَـٰسِلَا۟ وَأَغْلَـٰلًۭا وَسَعِيرًا
Hakika HaSisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali. [4]
Maelezo ya chini[4] Hakika Sisi tumewawekea tayari makafiri minyororo kuwafungia miguu yao, pingu za kuwafungia mikono na shingo, na moto unao waka.
Kiungo 76:4
5
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍۢ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا
Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri! [5]
Maelezo ya chini[5] Hakika walio kuwa wakweli katika Imani yao watakunywa mvinyo iliyo changanywa na maji ya kafuri.
Kiungo 76:5
6
عَيْنًۭا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ ٱللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًۭا
Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. [6]
Maelezo ya chini[6] Hiyo ni chemchem wanayo inywa waja wa Mwenyezi Mungu, na wanaipitisha watakapo kwa sahala.
Kiungo 76:6
7
يُوفُونَ بِٱلنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًۭا كَانَ شَرُّهُۥ مُسْتَطِيرًۭا
Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana, [7]
Maelezo ya chini[7] Wanatekeleza yaliyo wajibikia , na wanaikhofu Siku kubwa hiyo ambayo madhara yake yataenea kote kote,
Kiungo 76:7
8
وَيُطْعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسْكِينًۭا وَيَتِيمًۭا وَأَسِيرًا
Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. [8]
Maelezo ya chini[8] Na huwalisha chakula mafakiri wasio weza kazi, na watoto walio fiwa na wazee wao, na wafungwa wasio miliki kitu, ijapo kuwa wao wenyewe hao watoaji wanakipenda hicho wanacho kitoa, na wanakihitajia.
Kiungo 76:8
9
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ ٱللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَآءًۭ وَلَا شُكُورًا
Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. [9]
Maelezo ya chini[9] Na hujiambia nafsi zao: Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya kutaka thawa;bu za Mwenyezi Mungu. Sisi hatutaki kwenu malipo au zawadi, wala hatutaki kushukuriwa na kusifiwa.
Kiungo 76:9
10
إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًۭا قَمْطَرِيرًۭا
Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. [10]
Maelezo ya chini[10] Hakika sisi tunakhofu kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku ya kumletea msiba atakaye kuwapo siku hiyo, na siku ya watu kukunja nyuso zao na vipaji vyao.
Kiungo 76:10
11
فَوَقَىٰهُمُ ٱللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمِ وَلَقَّىٰهُمْ نَضْرَةًۭ وَسُرُورًۭا
Basi Mwenyezi Mungu atwalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. [11]
Maelezo ya chini[11] Basi Mwenyezi Mungu akawalinda na shida za siku hiyo, na badala ya mkunjo wa wenye maasi, akawapa nyuso za kupendeza, na ukunjufu na furaha katika nyoyo zao,
Kiungo 76:11
12
وَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُوا۟ جَنَّةًۭ وَحَرِيرًۭا
Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri. [12]
Maelezo ya chini[12] Na akawajazi kwa ile subira yao Pepo imeenea furaha, na nguo zake ni hariri laini.
Kiungo 76:12
13
مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًۭا وَلَا زَمْهَرِيرًۭا
Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. [13]
Maelezo ya chini[13] Wakiegemea huko Peponi juu ya makochi, hawaoni joto la jua, wala shida ya baridi.
Kiungo 76:13
14
وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَـٰلُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًۭا
Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini. [14]
Maelezo ya chini[14] Na Pepo ambayo vivuli vya miti yake vimeenea kote kote, na matunda yake mepesi kuyachuma.
Kiungo 76:14
15
وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِـَٔانِيَةٍۢ مِّن فِضَّةٍۢ وَأَكْوَابٍۢ كَانَتْ قَوَارِيرَا۠
Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae, [15]
Maelezo ya chini[15] Na wakiwazungukia watumishi wao kwa bilauri za kunywea zilio fanywa kwa fedha, lakini unaona kiliomo ndani kama kwamba ni kigae,
Kiungo 76:15
16
قَوَارِيرَا۟ مِن فِضَّةٍۢ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًۭا
Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo. [16]
Maelezo ya chini[16] Na vinapimwa vinywaji kwa kadiri wanavyo penda wanywaji.
Kiungo 76:16
17
وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًۭا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا
Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi. [17]
Maelezo ya chini[17] Na watu wema hupewa kunywa huko Peponi mvinyo inayo fanana na sharubati ya tangawizi kwa utamu.
Kiungo 76:17
18
عَيْنًۭا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًۭا
Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil. [18]
Maelezo ya chini[18] Hiyo ni kutokana na chemchem ya Peponi inayo itwa Salsabil, kwa sababu ya wepesi wa unywaji wake na uzuri wake.
Kiungo 76:18
19
۞ وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَٰنٌۭ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًۭا مَّنثُورًۭا
Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa. [19]
Maelezo ya chini[19] Na watakuwa wanawazunguka vijana ambao hawabadiliki hali yao, kwa furaha na sururi. Ukiwaona wanapo zunguka kwa wepesi na uchangamfu, utawadhania kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao, kama lulu zilizo tandazwa mbele yako zinang'ara.
Kiungo 76:19
20
وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًۭا وَمُلْكًۭا كَبِيرًا
Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa. [20]
Maelezo ya chini[20] Na ukitazama popote katika hiyo Pepo utaona neema kubwa, na ufalme ulio tanda.
Kiungo 76:20
21
عَـٰلِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌۭ وَإِسْتَبْرَقٌۭ ۖ وَحُلُّوٓا۟ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍۢ وَسَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًۭا طَهُورًا
Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. [21]
Maelezo ya chini[21] Juu yao zipo nguo za hariri nyepesi za kijani, na nguo za hariri nzito. Na mapambo yao yaliomo mikononi mwao ni vikuku vya fedha. Na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji kingine kilio safi, hakina uchafu wala najisi.
Kiungo 76:21
22
إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَآءًۭ وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا
Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa. [22]
Maelezo ya chini[22] Hakika neema hizi ameziandaa kwa kukulipeni kwa vitendo vyenu. Na hizo juhudi zenu duniani ni zenye kusifika kwa Mwenyezi Mungu, na zinampendeza, na zimekubaliwa.
Kiungo 76:22
23
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ ٱلْقُرْءَانَ تَنزِيلًۭا
Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo. [23]
Maelezo ya chini[23] Hakika Sisi, kwa rehema yetu na hikima yetu, tumekuteremshia wewe Qur'ani kwa njia ya kukutuza moyo wako, na uweze daima kuihifadhi, basi huto isahau kabisa.
Kiungo 76:23
24
فَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ ءَاثِمًا أَوْ كَفُورًۭا
Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru. [24]
Maelezo ya chini[24] Basi subiri, uivumilie hikima ya Mola wako Mlezi kwa kuakhirisha kushinda kwako kuwashinda maadui zako, na wewe ukapata mitihani kwa maudhi yao. Wala usiwat'ii washirikina, wingi wa madhambi, walio zama katika ukafiri.
Kiungo 76:24
25
وَٱذْكُرِ ٱسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةًۭ وَأَصِيلًۭا
Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni; [25]
Maelezo ya chini[25] Na dumisha kumkumbuka na kumtaja Mola wako Mlezi, na sali alfajiri mapema, na adhuhuri, na alasiri jioni,
Kiungo 76:25
26
وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَٱسْجُدْ لَهُۥ وَسَبِّحْهُ لَيْلًۭا طَوِيلًا
Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu. [26]
Maelezo ya chini[26] Na usiku sali magharibi na isha. Na fanya ibada za usiku kwa muda mrefu.
Kiungo 76:26
27
إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ يُحِبُّونَ ٱلْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَآءَهُمْ يَوْمًۭا ثَقِيلًۭا
Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito. [27]
Maelezo ya chini[27] Hakika hawa makafiri wanaipenda dunia, na wanaifadhilisha kuliko Akhera. Na wanaiacha migongoni mwao siku yenye misiba mikubwa, na vitisho vikali. Wala wao hawajui nini cha kuwaokoa wao na hayo!
Kiungo 76:27
28
نَّحْنُ خَلَقْنَـٰهُمْ وَشَدَدْنَآ أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَآ أَمْثَـٰلَهُمْ تَبْدِيلًا
Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao. [28]
Maelezo ya chini[28] Sisi tumewaumba wao, na tumefanya kwa hikima kuumbwa kwao. Na tukitaka tutawateketeza wao na tutawaleta mfano ya wao badala yao, ambao hao watakuja kumt'ii Mwenyezi Mungu kinyume na wao.
Kiungo 76:28
29
إِنَّ هَـٰذِهِۦ تَذْكِرَةٌۭ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًۭا
Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi. [29]
Maelezo ya chini[29] Hakika Sura hii ni mawaidha kwa walimwengu wote. Basi mwenye kutaka atafuata njia ya Imani na uchamngu kwendea kwa Mola wake Mlezi imfikishe kwenye maghfira yake na Pepo yake.
Kiungo 76:29
30
وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًۭا
Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima. [30]
Maelezo ya chini[30] Wala nyinyi hamwezi kutaka kitu chochote ila wakati anapo taka Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzijua hali zenu, Mwenye hikima kwa anayo yataka na akayakhiari.
Kiungo 76:30
31
يُدْخِلُ مَن يَشَآءُ فِى رَحْمَتِهِۦ ۚ وَٱلظَّـٰلِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًۢا
Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu. [31]
Maelezo ya chini[31] Humuingiza amtakaye katika Pepo yake. Basi kuingia Peponi ni kwa fadhila na rehema ya Mwenyezi Mungu. Naye amewadhalilisha wenye kudhulumu, amewatengenezea adhabu iliyo chungu.
Kiungo 76:31

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure