Sura ya 77 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Mursalat (Zilizotumwa)

سُورَةُ المُرۡسَلَاتِ
Aya 50

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلْمُرْسَلَـٰتِ عُرْفًۭا
Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! [1]
Maelezo ya chini[1] Naapa kwa Aya zilizo tumwa kwa ulimi wa Jibrili kumpelekea Muhammad kwa upole wa kawaida na kheri,
Kiungo 77:1
2
فَٱلْعَـٰصِفَـٰتِ عَصْفًۭا
Na zinazo vuma kwa kasi! [2]
Maelezo ya chini[2] Na kwa Aya zenye kuzitwaa kwa nguvu dini nyengine zote za uwongo zikizipeperushia mbali,
Kiungo 77:2
3
وَٱلنَّـٰشِرَٰتِ نَشْرًۭا
Na zikaeneza maeneo yote! [3]
Maelezo ya chini[3] Na kwa Aya zenye kueneza hikima na uwongofu katika nyoyo za walimwengu kwa uenezi mkubwa mno,
Kiungo 77:3
4
فَٱلْفَـٰرِقَـٰتِ فَرْقًۭا
Na zinazo farikisha zikatawanya! [4]
Maelezo ya chini[4] Na zenye kufarikisha baina ya kweli na uwongo kwa mfarakano ulio wazi kabisa,
Kiungo 77:4
5
فَٱلْمُلْقِيَـٰتِ ذِكْرًا
Na zinazo peleka mawaidha! [5]
Maelezo ya chini[5] Na zenye kuwapa watu mawaidha ya kuwanufaisha,
Kiungo 77:5
6
عُذْرًا أَوْ نُذْرًا
Kwa kuudhuru au kuonya, [6]
Maelezo ya chini[6] Ili iwe ni udhuru kwao na onyo wasiwe na hoja,
Kiungo 77:6
7
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٌۭ
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! [7]
Maelezo ya chini[7] Hakika haya mliyo ahidiwa ya kuja Kiyama kwa yakini yatatimia tu bila ya shaka yoyote.
Kiungo 77:7
8
فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتْ
Wakati nyota zitakapo futwa, [8]
Maelezo ya chini[8] Basi nyota zitapo ondolewa kabisa,
Kiungo 77:8
9
وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتْ
Na mbingu zitakapo pasuliwa, [9]
Maelezo ya chini[9] Na mbingu zitapo pasuka,
Kiungo 77:9
10
وَإِذَا ٱلْجِبَالُ نُسِفَتْ
Na milima itakapo peperushwa, [10]
Maelezo ya chini[10] Na milima ikavurugwa na ikapeperushiwa mbali na upepo,
Kiungo 77:10
11
وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتْ
Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, [11]
Maelezo ya chini[11] Na Mitume wakawekewa wakati maalumu wahudhurie kwa ajili ya kuwatolea ushahidi kaumu zao.
Kiungo 77:11
12
لِأَىِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ
Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? [12]
Maelezo ya chini[12] Kwa ajili ya siku gani yametayarishwa mambo haya makubwa makubwa?
Kiungo 77:12
13
لِيَوْمِ ٱلْفَصْلِ
Kwa siku ya kupambanua! [13]
Maelezo ya chini[13] Kwa ajili ya siku watakapo pambanuliwa baina ya viumbe.
Kiungo 77:13
14
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ
Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? [14]
Maelezo ya chini[14] Na nini cha kukujuvya ina nini hiyo siku ya kupambanua?
Kiungo 77:14
15
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! [15]
Maelezo ya chini[15] Ni maangamio ya milele siku hiyo kwa hao wanao kadhibisha walio waahidi Mitume!
Kiungo 77:15
16
أَلَمْ نُهْلِكِ ٱلْأَوَّلِينَ
Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? [16]
Maelezo ya chini[16] Kwani hatukuwaangamiza mataifa ya zamani yaliyo kadhibisha,
Kiungo 77:16
17
ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ ٱلْـَٔاخِرِينَ
Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? [17]
Maelezo ya chini[17] Na kisha tukawafuatilizia hao wenginewe tukawateketeza hali kadhaalika,
Kiungo 77:17
18
كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ
Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! [18]
Maelezo ya chini[18] Kwa madhambi waliyo yafanya na walivyo mkataa Mwenyezi Mungu?
Kiungo 77:18
19
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [19]
Maelezo ya chini[19] Siku hiyo ni siku ya kuteketezwa walio kadhibisha, kama tulivyo waahidi.
Kiungo 77:19
20
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّآءٍۢ مَّهِينٍۢ
Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? [20]
Maelezo ya chini[20] Kwani hatukukuumbeni kutokana na maji yaliyo dhalili, nayo ni manii,
Kiungo 77:20
21
فَجَعَلْنَـٰهُ فِى قَرَارٍۢ مَّكِينٍ
Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? [21]
Maelezo ya chini[21] Na tukayaweka maji haya katika pahala patulivu,
Kiungo 77:21
22
إِلَىٰ قَدَرٍۢ مَّعْلُومٍۢ
Mpaka muda maalumu? [22]
Maelezo ya chini[22] Mpaka kutimilia kuumbwa kwake na kutengenezwa kwake kwa muda anao ujua Mwenyezi Mungu.
Kiungo 77:22
23
فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ ٱلْقَـٰدِرُونَ
Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. [23]
Maelezo ya chini[23] Nasi tukaweka vipimo katika kuumbwa kwake, na kutengenezwa kwake, na kutoka kwake. Basi wabora wa kupima na kukadiria ni Sisi.
Kiungo 77:23
24
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [24]
Maelezo ya chini[24] Ole wao hao wanao kadhibisha neema za kuumba na kukadiria.
Kiungo 77:24
25
أَلَمْ نَجْعَلِ ٱلْأَرْضَ كِفَاتًا
Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya [25]
Maelezo ya chini[25] Kwani hatukuifanya ardhi kuwa imekusanya juu ya mgongo wake
Kiungo 77:25
26
أَحْيَآءًۭ وَأَمْوَٰتًۭا
Walio hai na maiti? [26]
Maelezo ya chini[26] Viumbe vilivyo hai visio hisabika, na vilio kufa visio kadirika,
Kiungo 77:26
27
وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ شَـٰمِخَـٰتٍۢ وَأَسْقَيْنَـٰكُم مَّآءًۭ فُرَاتًۭا
Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? [27]
Maelezo ya chini[27] Na tukaweka milima iliyo thibiti imara mirefu, na tukakunywesheni maji matamu?
Kiungo 77:27
28
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [28]
Maelezo ya chini[28] Wataangamia siku hiyo hao wanao kadhibisha neema hizi!
Kiungo 77:28
29
ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! [29]
Maelezo ya chini[29] Siku ya kupambanua wataambiwa makafiri: Nendeni huko Motoni mliko kuwa mkikukanusha.
Kiungo 77:29
30
ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ ظِلٍّۢ ذِى ثَلَـٰثِ شُعَبٍۢ
Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! [30]
Maelezo ya chini[30] Nendeni kwenye joto la moshi wa Jahannamu ulio gawika kwa ukubwa wake mapande matatu.
Kiungo 77:30
31
لَّا ظَلِيلٍۢ وَلَا يُغْنِى مِنَ ٱللَّهَبِ
Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. [31]
Maelezo ya chini[31] Hapana cha kujikinga na joto la siku hiyo, wala kivuli hicho hakipunguzi joto la mwako hata kidogo.
Kiungo 77:31
32
إِنَّهَا تَرْمِى بِشَرَرٍۢ كَٱلْقَصْرِ
Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! [32]
Maelezo ya chini[32] Moto huo hutupa macheche yenye ukubwa kama majumba,
Kiungo 77:32
33
كَأَنَّهُۥ جِمَـٰلَتٌۭ صُفْرٌۭ
Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! [33]
Maelezo ya chini[33] Au utaona hayo macheche kama ngamia weusi wenye kuingia rangi ya manjano.
Kiungo 77:33
34
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [34]
Maelezo ya chini[34] Wataangamia siku hiyo wanao kanusha kwamba hizi ndizo sifa za Moto.
Kiungo 77:34
35
هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, [35]
Maelezo ya chini[35] Haya uliyo simuliwa yatatokea katika siku ambayo hawatatamka kitu cha kuwanufaisha,
Kiungo 77:35
36
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. [36]
Maelezo ya chini[36] Wala hawatakuwa na idhini ya kutamka, wala hawatatoa udhuru, kwani hawana udhuru.
Kiungo 77:36
37
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! [37]
Maelezo ya chini[37] Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha siku hii.
Kiungo 77:37
38
هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَـٰكُمْ وَٱلْأَوَّلِينَ
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. [38]
Maelezo ya chini[38] Hii ndiyo siku ya kufafanua baina ya mwenye ukweli, na mwenye uwongo, kwa kuwa kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa anavyo stahiki. Enyi mnao mkadhibisha Muhammad! Tumekujaalieni nyinyi na walio kutangulieni walio kadhibisha mfano wenu,
Kiungo 77:38
39
فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌۭ فَكِيدُونِ
kiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! [39]
Maelezo ya chini[39] Kama mnayo hila ya kujikinga na adhabu basi fanyeni hila hiyo. Basi njooni muepukane na adhabu yangu.
Kiungo 77:39
40
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! [40]
Maelezo ya chini[40] Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha ahadi ya Mwenyezi Mungu.
Kiungo 77:40
41
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى ظِلَـٰلٍۢ وَعُيُونٍۢ
Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, [41]
Maelezo ya chini[41] Hakika wachamngu wenye kujikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika kivuli kikubwa, na chemchem zinazo miminika,
Kiungo 77:41
42
وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ
Na matunda wanayo yapenda, [42]
Maelezo ya chini[42] Na matunda wanayo yaonea ladha, na wanayo yapenda,
Kiungo 77:42
43
كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. [43]
Maelezo ya chini[43] Wataambiwa kwa kuamkiwa na kukirimiwa: Kuleni na mnywe chakula na vinywaji kwa starehe kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kuwa mkivitenda duniani.
Kiungo 77:43
44
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. [44]
Maelezo ya chini[44] Hakika Sisi huwalipa mfano wa malipo hayo matukufu watu wema.
Kiungo 77:44
45
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [45]
Maelezo ya chini[45] Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha Pepo.
Kiungo 77:45
46
كُلُوا۟ وَتَمَتَّعُوا۟ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! [46]
Maelezo ya chini[46] Na makafiri wataambiwa: Kuleni na mjistareheshe kwa starehe isiyo baki muda mrefu, kwani hakika nyinyi ni wakosefu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.
Kiungo 77:46
47
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [47]
Maelezo ya chini[47] Wataangamia siku hiyo wanao ikadhibisha neema.
Kiungo 77:47
48
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرْكَعُوا۟ لَا يَرْكَعُونَ
Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. [48]
Maelezo ya chini[48] Na wakiambiwa: Swalini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na mnyenyekeeni Yeye, hawanyenyekei wala hawaswali; bali hushikilia kiburi chao!
Kiungo 77:48
49
وَيْلٌۭ يَوْمَئِذٍۢ لِّلْمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [49]
Maelezo ya chini[49] Wataangamia siku wanao kadhibisha amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake.
Kiungo 77:49
50
فَبِأَىِّ حَدِيثٍۭ بَعْدَهُۥ يُؤْمِنُونَ
Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? [50]
Maelezo ya chini[50] Basi maneno gani hawa watayaamini ikiwa hawaiamini Qur'ani, na hali hii ni muujiza ulio toka mbinguni?
Kiungo 77:50

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure