Dua za Qur'ani

Dua 41 kutoka Qur'ani

Dua ambazo Qur'ani inafundisha, nyingi zikianza na “Rabbana” (Mola wetu), kila moja ikiwa na maandishi yake ya Kiarabu, tafsiri ya maana na kisomo.

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

Sura zote
1

Kukubaliwa kwa Ibrahim na Ismail

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَٰهِۦمُ ٱلْقَوَاعِدَ مِنَ ٱلْبَيْتِ وَإِسْمَٰعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ (127)
Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi. [127]
Maelezo ya chini[127] Na alipo kuwa Ibrahim na mwanawe Ismail wananyanyua misingi ya Alkaaba na huku wakimwomba Mwenyezi Mungu: Mola Mlezi wetu, Ewe Muumba wetu, na Muanzishi wetu! Tupokelee hii kazi yetu tuifanyayo kwa usafi wa niya kwa ajili yako, kwani Wewe ni Mwenye kusikia maombi yetu, ni Mwenye kujua ukweli wa niya yetu.
Sura Al-Baqara 2:127
2

Kujisalimisha na toba

رَبَّنَا وَٱجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَآ أُمَّةًۭ مُّسْلِمَةًۭ لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ (128)
Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [128]
Maelezo ya chini[128] Mola Mlezi wetu! Tuwezeshe na utujaalie tuwe wenye kukusafia niya Wewe, na miongoni mwa vizazi vyetu wajaalie watoke watu wenye kukusafia Wewe. Na tufundishe njia za ibada yetu kukuabudu Wewe katika Nyumba hii takatifu na pembezoni mwake, na pokea toba yetu tunapo sahau au tunapo kosea. Hakika Wewe ni mwingi wa kupokea toba za waja wako, na Msamehevu kwao kwa fadhila yako na rehema yako.
Sura Al-Baqara 2:128
3

Mema ya dunia na Akhera

وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِى ٱلدُّنْيَا حَسَنَةًۭ وَفِى ٱلْءَاخِرَةِ حَسَنَةًۭ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ (201)
Na katika wao wapo wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto! [201]
Maelezo ya chini[201] Na wapo watu ambao Mwenyezi Mungu amewawezesha nyoyo zao zikapelekea kuomba kheri ya dunia na Akhera, na wakamwomba Mwenyezi Mungu awaepushe na shari na adhabu ya Moto.
Sura Al-Baqara 2:201
4

Subira na uthabiti

وَلَمَّا بَرَزُوا۟ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُوا۟ رَبَّنَآ أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًۭا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَٰفِرِينَ (250)
Na walipo toka kupambana na Jaluti na majeshi yake walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri. [250]
Maelezo ya chini[250] Waumini walipo songa kupigana na Jaluti na jeshi lake walimwelekea Mwenyezi Mungu wakamnyenyekea na kumwomba awajaze subira, awatie nguvu azma zao, naawaweke imara katika uwanja wa vita, na awape ushindi juu ya maadui zao makafiri.
Sura Al-Baqara 2:250
5

Msamaha, rehema na ulinzi

لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا ٱكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَآ إِن نَّسِينَآ أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَآ إِصْرًۭا كَمَا حَمَلْتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦ ۖ وَٱعْفُ عَنَّا وَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَآ ۚ أَنتَ مَوْلَىٰنَا فَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَٰفِرِينَ (286)
Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. [286]
Maelezo ya chini[286] Hakika Mwenyezi Mungu hawakalifishi waja wake ila kwa kadiri wanavyo weza kuyafanya na kuyafuata. Kwa hivyo kila mwenye kukalifishwa atalipwa kwa vitendo vyake - akitenda kheri atapata malipo ya kheri, akitenda shari atapata shari. Basi enyi Waumini! Nyenyekeeni kwa Mwenyezi Mungu mkimuomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Usituadhibu pindi tukiporonyoka tukasahau ulio tuamrisha, au yakatupata ya kutusabibisha kutumbukia makosani. Mola Mlezi wetu! Usituchukulie kwa shida ukatupa sharia nzito nzito kama ulivyo wafanyia Mayahudi kwa sababu ya inda yao na udhalimu wao. Wala usitukalifishe mambo tusiyo yaweza, na utusamehe kwa ukarimu wako, na tughufirie kwa fadhila yako, na uturehemu kwa rehema yako yenye wasaa. Hakika Wewe ni Mola Mlezi wetu. Tunusuru ewe Mola Mlezi, kwa ajili ya kutukuza Neno lako na kuitangaza Dini yako - tuwashinde kaumu ya wapingaji.
Sura Al-Baqara 2:286
6

Mioyo thabiti

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ (8)
(Na hao husema): Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji. [8]
Maelezo ya chini[8] Hao wanazuoni wenye akili husema: Mola wetu Mlezi! Usizifanye nyoyo zetu zikaacha Haki baada ya Wewe kwisha tuongoza kuiendea hiyo Haki. Ewe Mola wetu Mlezi! Tupe rehema kutoka kwako kwa kutuwezesha na kututhibitisha. Hakika Wewe ndiwe Mwenye kunyima na ndiwe Mpaji.
Sura Aal-Imran 3:8
7

Imani na Siku ya Kukusanywa

رَبَّنَآ إِنَّكَ جَامِعُ ٱلنَّاسِ لِيَوْمٍۢ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخْلِفُ ٱلْمِيعَادَ (9)
Mola wetu Mlezi! Wewe ndiye Mkusanyaji wa watu kwa Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake. [9]
Maelezo ya chini[9] Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ndiwe utao wakusanya watu Siku hiyo isiyo na shaka, ili kumlipa kila mmojapo kwa alilo litenda. Kwani Wewe umeahidi hayo, na Wewe hukhalifu miadi yako.
Sura Aal-Imran 3:9
8

Msamaha na kuepushwa na Moto

ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ إِنَّنَآ ءَامَنَّا فَٱغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ (16)
Ambao husema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto, [16]
Maelezo ya chini[16] Malipo haya watayapata wale ambao nyoyo zao zimejaa Imani, na wakatangaza kwa ndimi zao wakisema kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu: Mola Mlezi wetu! Hakika sisi tumeamini kwa kuitikia wito wako. Basi tusamehe dhambi zetu, na utuhifadhi na adhabu ya Moto.
Sura Aal-Imran 3:16
9

Kizazi chema

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُۥ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِى مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةًۭ طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ (38)
Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi. [38]
Maelezo ya chini[38] Zakariya a.s. alipo iona neema ya Mwenyezi Mungu kwa Maryamu alimwelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu akimwomba kwa fadhila yake na ukarimu wake na uwezo wake, naye ampe mtoto mwanamume. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maombi ya mwenye kuomba kwake kwa unyenyekevu. Naye ni Muweza wa kuitikia maombi na hata zinge kuwapo pingamizi za kikawaida kama ukongwe na utasa.
Sura Aal-Imran 3:38
10

Imani na kumfuata Mtume

رَبَّنَآ ءَامَنَّا بِمَآ أَنزَلْتَ وَٱتَّبَعْنَا ٱلرَّسُولَ فَٱكْتُبْنَا مَعَ ٱلشَّٰهِدِينَ (53)
Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanao shuhudia. [53]
Maelezo ya chini[53] Na sisi tunasema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tumekisadiki Kitabu chako ulicho mteremshia Nabii wako, na tunaifuata amri ya Mtume wako, Isa a.s. Basi tuthibitishe kuwa miongoni mwa wenye kumshuhudia Mtume wako katika kufikisha ujumbe, na kuwashuhudia Wana wa Israili katika ukafiri wao na upinzani wao.
Sura Aal-Imran 3:53
11

Msamaha na uthabiti

وَمَا كَانَ قَوْلَهُمْ إِلَّآ أَن قَالُوا۟ رَبَّنَا ٱغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِىٓ أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَٰفِرِينَ (147)
Wala kauli yao haikuwa ila ni kusema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri. [147]
Maelezo ya chini[147] Na kauli yao vilipo kuwa vita vikali haikuwa ila kusema: Mola wetu Mlezi! Tusamehe dhambi zetu kubwa na ndogo. Na tusimamishe imara katika midani za vita, na utunusuru na hawa maadui wa Dini yako, wenye kukukanya Wewe na ujumbe wa Mtume wako.
Sura Aal-Imran 3:147
12

Kutafakari uumbaji

ٱلَّذِينَ يَذْكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَٰمًۭا وَقُعُودًۭا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِى خَلْقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَٰذَا بَٰطِلًۭا سُبْحَٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ (191)
Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa Mbingu na Ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto. [191]
Maelezo ya chini[191] Ni shani ya wenye akili kuwa kila pahali wao wanahudhurisha katika nafsi zao adhama na utukufu wa Mwenyezi Mungu, wakiwa wamesimama au wamekaa au wamejinyoosha kitandani, na wanazingatia uumbaji wa mbingu na ardhi pamoja na viliomo ndani yake, na huku wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuumba haya ila kwa hikima uliyo ikadiria. Na Wewe umetakasika na kila upungufu. Bali umeumba hivi vyote kuwa ni dalili ya kudra yako, na ishara ya upeo wa hikima yako. Utuhifadhi na adhabu ya Moto kwa kutuwezesha kukut'ii.
Sura Aal-Imran 3:191
13

Kuepushwa na Moto

رَبَّنَآ إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ ٱلنَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُۥ ۖ وَمَا لِلظَّٰلِمِينَ مِنْ أَنصَارٍۢ (192)
Mola wetu Mlezi! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na walio dhulumu hawana wasaidizi. [192]
Maelezo ya chini[192] Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Hakika mwenye kustahiki Moto na ukamuingiza, basi umempa hizaya. Na mwenye kudhulumu akastahiki Moto hana wa kumnusuru nao.
Sura Aal-Imran 3:192
14

Imani, msamaha na watu wema

رَّبَّنَآ إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًۭا يُنَادِى لِلْإِيمَٰنِ أَنْ ءَامِنُوا۟ بِرَبِّكُمْ فَـَٔامَنَّا ۚ رَبَّنَا فَٱغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّـَٔاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ ٱلْأَبْرَارِ (193)
Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema. [193]
Maelezo ya chini[193] Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Hakika sisi tumemsikia Mtume wako akiita watu wakuamini Wewe, nasi tukamt'ii na tukamuamini. Ewe Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu makubwa, na tufutie maovu yetu madogo madogo, na baada ya kufa kwetu tujaalie tuwe pamoja na waja wako walio bora.
Sura Aal-Imran 3:193
15

Yaliyoahidiwa kupitia mitume

رَبَّنَا وَءَاتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ ٱلْمِيعَادَ (194)
Mola wetu Mlezi! Na utupe uliyo tuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika Wewe huvunji miadi. [194]
Maelezo ya chini[194] Ewe Muumba wetu, na Mwenye kutusimamia mambo yetu, na Mlinzi wetu! Tupe uliyo tuahidi kwa ndimi za Mitume yako, nayo ni ushindi na kuungwa mkono duniani. Wala usituingize Motoni ukatuhizi Siku ya Kiyama. Shani yako ni kuwa huendi kinyume na miadi yako.
Sura Aal-Imran 3:194
16

Tuandike pamoja na mashahidi

وَإِذَا سَمِعُوا۟ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا۟ مِنَ ٱلْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكْتُبْنَا مَعَ ٱلشَّٰهِدِينَ (83)
NA WANAPO SIKIA yaliyo teremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanachururika machozi kwa sababu ya Haki waliyo itambua. Wanasema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanao shuhudia. [83]
Maelezo ya chini[83] Na pia miongoni mwa Manasara wakiisikia Qur'ani aliyo teremshiwa Mtume huathirika nayo, macho huwatiririka machozi, kwa kuwa wanajua kuwa wanayo yasikia ni kweli tupu, basi nyoyo zao humili kwayo, na ndimi zao huomba dua kumwomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Tumekuamini Wewe na Mitume wako, na Haki ulio wateremshia. Basi ipokee Imani yetu, na utufanye miongoni mwa Umma wa Muhammad ulio wafanya mashahidi na hoja kwa watu wote Siku ya Kiyama.
Sura Al-Maida 5:83
17

Toba ya Adam na Hawa

قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَآ أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلْخَٰسِرِينَ (23)
Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika. [23]
Maelezo ya chini[23] Adam na mkewe wakasema nao wamejuta wananyenyekea: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumejidhulumu nafsi zetu kwa kuvunja amri yako, kuliko pelekea kuondoka kwa neema. Na ikiwa hutusamehe ukhalifu wetu, ukaturehemu kwa fadhila yako, hapana shaka tutakuwa katika wenye kukhasiri.
Sura Al-A'raf 7:23
18

Kulindwa na dhuluma

۞ وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَٰرُهُمْ تِلْقَآءَ أَصْحَٰبِ ٱلنَّارِ قَالُوا۟ رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ (47)
Na yanapo geuzwa macho yao kuelekea watu wa Motoni, watasema: Mola Mlezi wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu walio dhulumu. [47]
Maelezo ya chini[47] Macho ya hao Waumini yakigeukia upande wa watu wa Motoni baada ya wito huo, watasema kwa kitisho watacho kioni cha Moto: Ewe Mola wetu Mlezi! Usitutie pamoja na hawa madhaalimu walio dhulumu nafsi zao, wakadhulumu Haki, na wakawadhulumu watu!
Sura Al-A'raf 7:47
19

Hukumu kwa haki

قَدِ ٱفْتَرَيْنَا عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِى مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ نَجَّىٰنَا ٱللَّهُ مِنْهَا ۚ وَمَا يَكُونُ لَنَآ أَن نَّعُودَ فِيهَآ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَىْءٍ عِلْمًا ۚ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا ٱفْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِٱلْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْفَٰتِحِينَ (89)
Bila ya shaka itakuwa tumemzulia uwongo Mwenyezi Mungu tukirudi katika mila yenu baada ya kwisha tuokoa nayo Mwenyezi Mungu. Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo, ila akitaka Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu. Ujuzi wa Mola Mlezi wetu umeenea katika kila kitu. Kwa Mwenyezi Mungu tunategemea. Ewe Mola Mlezi wetu! Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanao hukumu. [89]
Maelezo ya chini[89] Akaendelea zaidi kuwavunja tamaa yao ya kuwarejeza kwenye mila yao kama walivyo taka. Akasema: Tutakuwa tunamzulia uwongo Mwenyezi Mungu tukiwa katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kesha tuhidi kwenye Njia Iliyo Nyooka. Na haifai sisi kuwa katika mila yenu kwa khiari yetu na kutaka kwetu, ila akipenda Mwenyezi Mungu turejee katika mila yenu. Na hayo hayawi! Kwa sababu Mola Mlezi wetu anatujua vyema, na Yeye hataki turejee kwenye upotovu wenu. Yeye aliye tukuka shani yake amekienea kila kitu kwa ujuzi wake. Anatuongoa kwa upole wake na hikima yake kwenye jambo litalo tuhifadhia Imani yetu. Kwa Yeye peke yake ndio tumesalimisha mambo yetu, na huku tunashikilia yale aliyo tuwajibisha tuyashike. Ewe Mola Mlezi wetu! Tutenge sisi na hao kaumu yetu kwa Haki, kama ilivyo kuwa mwendo wako unavyo amua baina ya wenye kufuata Haki na wakatenda mema, na wale wapotovu waharibifu. Na Wewe kwa kuwa ujuzi wako na uwezo ulivyo enea ndiye Muadilifu na Muweza kuliko mahakimu wote.
Sura Al-A'raf 7:89
20

Kutawakali na ulinzi

فَقَالُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةًۭ لِّلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ (85)
Wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu. Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu. [85]
Maelezo ya chini[85] Waumini wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu peke yake. Kisha wakamwomba Mola wao Mlezi asiwatie katika mitihani na mateso ya makafiri.
وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلْكَٰفِرِينَ (86)
Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri. [86]
Maelezo ya chini[86] Wakamwomba Mola wao Mlezi wakisema: Kwa vile ulivyo tumiminia neema na rehema, na kwa wingi wa rehema yako unayo sifika nayo, tuokoe na hawa watu wanao kataa, wenye kudhulumu.
Sura Yunus 10:85-86
21

Amani kwa Makka na kuepushwa na ibada ya masanamu

وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِيمُ رَبِّ ٱجْعَلْ هَٰذَا ٱلْبَلَدَ ءَامِنًۭا وَٱجْنُبْنِى وَبَنِىَّ أَن نَّعْبُدَ ٱلْأَصْنَامَ (35)
Na Ibrahim alipo sema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu. [35]
Maelezo ya chini[35] Ewe Nabii! Ili watu wako wapate kuzingatia na waache ushirikina wao, wakumbushe kauli ya baba yao Ibrahim baada ya kuijenga Alkaaba. Alisema: Ewe Mola Mlezi! Ujaalie mji huu wenye Alkaaba uwe wa amani, ulindwe na wenye kudhulumu. Na unibaidishe, niwe mbali, mimi na wanangu na ibada ya masanamu.
Sura Ibrahim 14:35
22

Kusimamisha swala na msamaha

رَبِّ ٱجْعَلْنِى مُقِيمَ ٱلصَّلَوٰةِ وَمِن ذُرِّيَّتِى ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَآءِ (40)
Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Swala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. [40]
Maelezo ya chini[40] Ewe Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nitimize Swala kwa inavyo takikana. Na wawezeshe watimilize kadhaalika wale walio wa kheri katika dhuriya zangu. Ewe Mola wetu Mlezi ipokee dua yangu kwa mapokezi ya kukubaliwa.
رَبَّنَا ٱغْفِرْ لِى وَلِوَٰلِدَىَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ ٱلْحِسَابُ (41)
Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu. [41]
Maelezo ya chini[41] Ewe Mola wetu Mlezi! Nisamehe madhambi yaliyo niponyoka, na wasamehe wazazi wangu, na Waumini wote, Siku itapo hakikishwa hisabu, na baadae ikawa malipo.
Sura Ibrahim 14:40-41
23

Kuingia na kutoka kwa ukweli

وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِى مُدْخَلَ صِدْقٍۢ وَأَخْرِجْنِى مُخْرَجَ صِدْقٍۢ وَٱجْعَل لِّى مِن لَّدُنكَ سُلْطَٰنًۭا نَّصِيرًۭا (80)
Na sema: Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazo toka kwako zinisaidie. [80]
Maelezo ya chini[80] Na sema: Ewe Mola Mlezi! Niingize maingizo ya kuridhisha matukufu katika kila unapo niingiza katika jambo au pahala. Na unitoe kwa kutoka kunako ridhisha kutukufu. Na kwa fadhila yako nijaalie nguvu za kunisaidia niwashinde maadui zangu.
Sura Al-Isra 17:80
24

Rehema na uongofu

إِذْ أَوَى ٱلْفِتْيَةُ إِلَى ٱلْكَهْفِ فَقَالُوا۟ رَبَّنَآ ءَاتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةًۭ وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًۭا (10)
Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu. [10]
Maelezo ya chini[10] Taja pale walipo kwenda hao vijana kwenye pango, wakafanya hapo ndipo pahali pa kujificha baada ya kukimbia ushirikina na washirikina kuhifadhi Dini yao. Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Tupe maghfira kutoka kwako, na utulinde na adui yetu, na tusahilishie hidaya na tawfiki katika mambo yetu!
Sura Al-Kahf 18:10
25

Msamaha na rehema

إِنَّهُۥ كَانَ فَرِيقٌۭ مِّنْ عِبَادِى يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلرَّٰحِمِينَ (109)
Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanao rehemu. [109]
Maelezo ya chini[109] Mimi sikukudhulumuni, bali nyinyi mmejidhulumu wenyewe. Kwani Waumini wema katika waja wangu walikuwa wakisema duniani: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.
Sura Al-Muminun 23:109
26

Dua ya msamaha na rehema

وَقُل رَّبِّ ٱغْفِرْ وَٱرْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ ٱلرَّٰحِمِينَ (118)
Nawe sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu. [118]
Maelezo ya chini[118] Na sema, ewe Nabii, ukimlingania Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea: Ewe Mola wangu Mlezi! Nisamehe dhambi zangu, na nirehemu. Kwani Wewe ni Mbora wa wanao rehemu, kwa sababu rehema yako imeenea na ipo karibu kwa watendao mema.
Sura Al-Muminun 23:118
27

Hekima na kuwa pamoja na wema

رَبِّ هَبْ لِى حُكْمًۭا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّٰلِحِينَ (83)
Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. [83]
Maelezo ya chini[83] Ibrahim a.s. akasema kwa kuomba: Mola wangu Mlezi! Nitunukie ukamilifu wa ilimu na vitendo, ili nipate kustahili kuubeba Ujumbe wako na hukummu kwa waja wako, na niwezeshe niungane pamoja na kundi la watendao wema.
وَٱجْعَل لِّى لِسَانَ صِدْقٍۢ فِى ٱلْءَاخِرِينَ (84)
Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye. [84]
Maelezo ya chini[84] Na nijaalie nipate sifa nzuri na kumbusho jema kwa kaumu zitazo kuja baada yangu, mabaki yake yasalie mpaka Siku ya Kiyama.
وَٱجْعَلْنِى مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ (85)
Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. [85]
Maelezo ya chini[85] Na nijaalie katika waja wako ulio watunukia neema za Peponi, kuwa ni malipo kwa sababu ya Imani yao kukuamini Wewe, na ibada yao kukuabudu Wewe.
Sura Ash-Shu'ara 26:83-85
28

Moyo safi Siku ya Kiyama

وَلَا تُخْزِنِى يَوْمَ يُبْعَثُونَ (87)
Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa. [87]
Maelezo ya chini[87] Wala usinitie aibu au hizaya mbele ya watu, Siku watapo tolewa makaburini kwa ajili ya hisabu na malipo.
يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌۭ وَلَا بَنُونَ (88)
Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. [88]
Maelezo ya chini[88] Siku ambayo hapana mtu ataye nafiika kwa mali ayatoe, au kwa wana wamsaidie.
إِلَّا مَنْ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلْبٍۢ سَلِيمٍۢ (89)
Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. [89]
Maelezo ya chini[89] Isipo kuwa aliye kuwa Muumini, na akamkabili Mwenyezi Mungu na moyo ulio mzima, hauna maradhi ya ukafiri, na unaafiki, na riya (kujionesha).
Sura Ash-Shu'ara 26:87-89
29

Kizazi chema kwa Ibrahim

رَبِّ هَبْ لِى مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ (100)
Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema. [100]
Maelezo ya chini[100] Ewe Mola wangu Mlezi! Nipe dhuriya walio wema wa vitendo, wasimamie hii kazi ya wito kuwaitia watu kwako Wewe, baada yangu.
Sura As-Saffat 37:100
30

Msamaha na ufalme kwa Suleiman

قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَهَبْ لِى مُلْكًۭا لَّا يَنۢبَغِى لِأَحَدٍۢ مِّنۢ بَعْدِىٓ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ (35)
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji. [35]
Maelezo ya chini[35] Suleiman alimwomba Mola wake Mlezi kwa kurejea kwake: Mola wangu Mlezi! Nighufirie yaliyo toka kwangu kwa ghafla, na unitunukie ufalme usio elekea yeyote kuupata baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mwingi wa kutunukia, na ndiye Mwingi wa kutoa.
Sura Sad 38:35
31

Rehema, elimu na msamaha

ٱلَّذِينَ يَحْمِلُونَ ٱلْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِۦ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَىْءٍۢ رَّحْمَةًۭ وَعِلْمًۭا فَٱغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا۟ وَٱتَّبَعُوا۟ سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ (7)
Wale wanao beba A'rshi, na wanao izunguka, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walio amini kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.
Sura Ghafir 40:7
32

Kuingia katika bustani za milele

رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّٰتِ عَدْنٍ ٱلَّتِى وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ ءَابَآئِهِمْ وَأَزْوَٰجِهِمْ وَذُرِّيَّٰتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ (8)
Mola wetu Mlezi! Na waingize katika Bustani za Milele ulizo waahidi. Na uwape haya pia wale walio fanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Sura Ghafir 40:8
33

Kulindwa na matokeo mabaya

وَقِهِمُ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ۚ وَمَن تَقِ ٱلسَّيِّـَٔاتِ يَوْمَئِذٍۢ فَقَدْ رَحِمْتَهُۥ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ (9)
Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu kukubwa.
Sura Ghafir 40:9
34

Shukrani na kizazi chema

وَوَصَّيْنَا ٱلْإِنسَٰنَ بِوَٰلِدَيْهِ إِحْسَٰنًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُۥ كُرْهًۭا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًۭا ۖ وَحَمْلُهُۥ وَفِصَٰلُهُۥ ثَلَٰثُونَ شَهْرًا ۚ حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُۥ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةًۭ قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِىٓ أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ ٱلَّتِىٓ أَنْعَمْتَ عَلَىَّ وَعَلَىٰ وَٰلِدَىَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَٰلِحًۭا تَرْضَىٰهُ وَأَصْلِحْ لِى فِى ذُرِّيَّتِىٓ ۖ إِنِّى تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّى مِنَ ٱلْمُسْلِمِينَ (15)
Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. [15]
Maelezo ya chini[15] Na tumemuusia mwanaadamu kwa wazazi wake awafanyie wema mkubwa. Kwani mama yake amechukua mimba yake kwa mashaka, na akamzaa kwa mashaka. Na muda wa kuchukuliwa mimba mpaka kuachishwa ziwa ni miezi thalathini. Muda wote huo mama kapitikiwa na kila namna ya machungu. Mpaka huyo mtu alipo fikilia ukamilifu wa nguvu zake na akili yake, na akafikia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Nijaalie niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nijaalie nitende vitendo vyema utavyo viridhi Wewe, na ujaalie huo wema wapate pia dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako kwa kila dhambi, na mimi ni miongoni wa Waislamu, yaani walio zisalimisha nafsi zao kwako. Uchache wa mimba ni miezi sita, kwa kauli yake Mtukufu: " Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini." Na kauli yake Mtukufu: "Na kumwachisha ziwa kwake ni miaka miwili", na kauli yake Mtukufu: "Na wazazi wa kike huwanyonyesha wana wao miaka miwili kaamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha." Basi ukitoa muda wa kuachisha ziwa kutokana na muda wa mimba na kunyonyesha inabakia muda wa mimba ni miezi sita. Na haya yanawafikiana na iliyo thibiti kwa ilimu za sayansi kwamba mtoto mchanga akizaliwa baada ya mimba ya miezi 6 anaweza kuishi.
Sura Al-Ahqaf 46:15
35

Msamaha kwa waumini

وَٱلَّذِينَ جَآءُو مِنۢ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَٰنِنَا ٱلَّذِينَ سَبَقُونَا بِٱلْإِيمَٰنِ وَلَا تَجْعَلْ فِى قُلُوبِنَا غِلًّۭا لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ رَبَّنَآ إِنَّكَ رَءُوفٌۭ رَّحِيمٌ (10)
Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu. [10]
Maelezo ya chini[10] Na Waumini walio kuja baada ya Wahajiri na Ansari husema: Mola wetu Mlezi! Tusamehe dhambi zetu, sisi na ndugu zetu walio tutangulia katika Imani. Wala usijaalie kuwa katika nyoyo zetu husda kuwahusudu walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe umefika ukomo katika upole na kurehemu.
Sura Al-Hashr 59:10
36

Kutawakali na kurejea

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌۭ فِىٓ إِبْرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذْ قَالُوا۟ لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَٰٓؤُا۟ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ ٱلْعَدَٰوَةُ وَٱلْبَغْضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَحْدَهُۥٓ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمْلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍۢ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ ٱلْمَصِيرُ (4)
Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo. [4]
Maelezo ya chini[4] Nyinyi mna kiigizo kizuri cha kukiiga katika Ibrahim na walio amini pamoja naye, pale walipo waambia watu wao: Hakika sisi tunajitenga nanyi, na tunajitenga na hiyo miungu ya uwongo mnayo iabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Sisi tunakukataeni, na umekwisha dhihiri uadui na kuchukiana baina yetu na nyinyi. Hayo hayataondoka kabisa mpaka mumuamini Mwenyezi Mungu peke yake. Lakini kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Nitakutakia maghfira, na similiki kwa Mwenyezi Mungu kitu chochote - kauli hiyo si ya kufuatwa. Kwani hayo yalikuwa kabla hajajua huyo baba yake kashikilia kuwa adui wa Mwenyezi Mungu wala hageuki. Ilipo dhihiri kwake kuwa hakika huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu alijitenga naye. Enyi waumini! Semeni: Mola wetu Mlezi! Kwako Wewe ndio tunategemea, na kwako Wewe tunarejea, na kwako Wewe ndio mwisho wetu Akhera.
Sura Al-Mumtahina 60:4
37

Kulindwa na fitna na msamaha

رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةًۭ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَٱغْفِرْ لَنَا رَبَّنَآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ (5)
Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa walio kufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [5]
Maelezo ya chini[5] Mola wetu Mlezi! Usitujaalie tukawa katika hali ya kuwa katika fitina za walio kufuru. Na tusamehe madhambi yetu, ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu usiye shindika, Mwenye hikima katika kutasarafu kwake.
Sura Al-Mumtahina 60:5
38

Utukamilishie nuru yetu na utusamehe

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ تُوبُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ تَوْبَةًۭ نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّٰتٍۢ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ يَوْمَ لَا يُخْزِى ٱللَّهُ ٱلنَّبِىَّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَٰنِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَٱغْفِرْ لَنَآ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍۢ قَدِيرٌۭ (8)
Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. [8]
Maelezo ya chini[8] Enyi mlio amini! Rejeeni kwa Mwenyezi Mungu, muache madhambi yenu, mrejee kweli kweli kwa ikhlasi. Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu, na akakutieni Peponi kwenye kupita mito chini ya majumba yake na miti yake, Siku atakayo inyanyua Mwenyezi Mungu hadhi ya Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao hao itakuwa inakwenda mbele yao, nayo itakuwa kuliani mwao, nao watakuwa wakisema kwa kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu: Ewe Bwana wetu, Mwenye kumiliki mambo yetu! Tutimizie nuru yetu, mpaka tuongoke kufikia Peponi. Na tusamehe dhambi zetu. Hakika Wewe ni Mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu.
Sura At-Tahrim 66:8
39

Dua ya Yunus

وَذَا ٱلنُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَٰضِبًۭا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِى ٱلظُّلُمَٰتِ أَن لَّآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبْحَٰنَكَ إِنِّى كُنتُ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ (87)
Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. [87]
Maelezo ya chini[87] Ewe Nabii! Taja kisa cha Yunus, aliye mezwa na samaki..Pale alipoona dhiki kwa vile watu wake walipo puuza wito wake, naye akawahama akenda mbali nao na huku amewakasirikia. Akadhani ya kuwa Mwenyezi Mungu amemruhusu kuwahama, na kwamba haitopita hukumu juu yake. Samaki akammeza, na akaishi katika kiza cha bahari. Akamwita Mola wake Mlezi kwa kumnyenyekea, na kuungama aliyo kuwa nayo, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hapana wa kuabudiwa kwa haki ila Wewe. Ninakutakasa na kila lisio kuelekea Wewe. Ninaungama kuwa hakika mimi nilikuwa miongoni mwa walio dhulumu nafsi zao kwa kutenda yasio kupendeza.
Sura Al-Anbiya 21:87
40

Dua ya Ayubu

۞ وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ (83)
Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu. [83]
Maelezo ya chini[83] Ewe Nabii! Mtaje Ayyubu, pale alipo mwita Mola wake Mlezi, na maradhi yalikwisha mdhoofisha, na akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika nimesibiwa na madhara na yananiuma! Na Wewe ni Mbora wa wanao rehemu..
Sura Al-Anbiya 21:83
41

Dua ya Zakariya

وَزَكَرِيَّآ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥ رَبِّ لَا تَذَرْنِى فَرْدًۭا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْوَٰرِثِينَ (89)
Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi. [89]
Maelezo ya chini[89] Na kitaje kisa cha Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi baada ya kwisha ona uweza wake Subhanahu kwa alivyo mtia katika nafsi yake matarajio ya rehema yake. Alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Usiniache mpweke bila ya kuwa na mrithi, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi. Kwani Wewe ndiye utakaye baki baada ya kumalizika viumbe vyote.
Sura Al-Anbiya 21:89

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure