Sura ya 26 kati ya 114 · Makkiya

Sura Ash-Shu'ara (Washairi)

سُورَةُ الشُّعَرَاءِ
Aya 227

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
طسٓمٓ
T'aa Siin Miim. (T'.S.M.) . [1]
Maelezo ya chini[1] Harufi hizi na mfano wa hizi ndizo zikakusanyika kuifanya Qur'ani kuwa ni muujiza ulio washinda watu kuiga mfano wake, ijapo kuwa hizo harufi ndizo wanazo zitamka. Basi mwenye kuitilia shaka hii Qur'ani kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu au la, basi na alete mfano wake. Na hatoweza.
Kiungo 26:1
2
تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُبِينِ
Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. [2]
Maelezo ya chini[2] Maneno haya niliyo kufunulia ni Aya za Kitabu chenye kuweka wazi hukumu zote ziliomo ndani yake.
Kiungo 26:2
3
لَعَلَّكَ بَـٰخِعٌۭ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ
Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini. [3]
Maelezo ya chini[3] Ewe Nabii! Hebu jionee huruma nafsi yako. Usijikere kwa kuhuzunukia inadi ya watu wako, na kuto amini kwao.
Kiungo 26:3
4
إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ءَايَةًۭ فَظَلَّتْ أَعْنَـٰقُهُمْ لَهَا خَـٰضِعِينَ
Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao. [4]
Maelezo ya chini[4] Sisi tunaweza kuwaletea muujiza wa kuwalazimisha Imani, wat'ii kwa unyenyekevu amri yake, na yatimie unayo yatarajia. Lakini hatuwaletei, kwa sababu mwendo wetu ni kuwaongoza watu waamini bila ya kuwalazimisha, ili isikosekane hikima ya kujaribiwa kwa mitihani, na yanayo kuja baada yake ya thawabu na adhabu.
Kiungo 26:4
5
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍۢ مِّنَ ٱلرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهُ مُعْرِضِينَ
Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao. [5]
Maelezo ya chini[5] Wala Mwenyezi Mungu hawaletei watu wako kwa ufunuo wake ya kuwakumbusha Dini ya Haki kuwa ni rehema kwao, ila wao huzua upya upinzani na ukafiri kuukataa. Kwani njia ya uwongofu imekwisha zibwa mbele yao.
Kiungo 26:5
6
فَقَدْ كَذَّبُوا۟ فَسَيَأْتِيهِمْ أَنۢبَـٰٓؤُا۟ مَا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. [6]
Maelezo ya chini[6] Hawa hakika wamekadhibisha Haki uliyo ileta, na wakaifanyia maskhara. Lakini wewe wasubirie. Wataona matokeo ya maskhara yao ya kuangamiza.
Kiungo 26:6
7
أَوَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلْأَرْضِ كَمْ أَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍۢ كَرِيمٍ
Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri? [7]
Maelezo ya chini[7] Hivyo hao wanatenda watendavyo katika ukafiri wao na kukadhibisha kwao wala hawaangalii baadhi ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu katika hii hii ardhi? Lau kuwa wanaangalia kwa kuzingatia wangeli ongoka. Hebu wazingatie hii mimea ya kila namna yenye manufaa tunayo itoa Sisi kwenye ardhi, na wala hawezi hayo isipo kuwa Mungu Mmoja Muweza.
Kiungo 26:7
8
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. [8]
Maelezo ya chini[8] Hakika katika kutoka kwa hii mimea ni dalili kubwa ya kuwepo Muumba Muweza. Lakini wengi wa watu si wenye kuamini.
Kiungo 26:8
9
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [9]
Maelezo ya chini[9] Hakika Mwenye kumiliki mambo yako, na Mwenye kukulinda, ndiye atakaye waadhibu hao wanao kadhibisha, na ndiye Mwenye kuwafadhili Waumini kwa rehema.
Kiungo 26:9
10
وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱئْتِ ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu, [10]
Maelezo ya chini[10] Ewe Muhammad! Watajie watu wako kisa cha Musa pale Mola wako Mlezi alipo mwita: Ewe Musa! Nenda kwa Utume kwa watu walio dhulumu nafsi zao kwa ukafiri, na wakawadhulumu Wana wa Israili kwa kuwafanya watumwa na kuwauwa watoto wao wanaume.
Kiungo 26:10
11
قَوْمَ فِرْعَوْنَ ۚ أَلَا يَتَّقُونَ
Watu wa Firauni. Hawaogopi? [11]
Maelezo ya chini[11] Nenda kwa kaumu ya Firauni; kwani hao wamepita mipaka katika dhulma yao. Ama ajabu ya watu hawa! Hawaogopi nini litalo wafika kwa vitendo vyao hivi, wakatahadhari?
Kiungo 26:11
12
قَالَ رَبِّ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ
Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe. [12]
Maelezo ya chini[12] Musa akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi nina khofu wasije kuukataa ujumbe wangu kwa kiburi na inda.
Kiungo 26:12
13
وَيَضِيقُ صَدْرِى وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِى فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَـٰرُونَ
Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun. [13]
Maelezo ya chini[13] Na mimi nimejaa dhiki kwa kuwa wataniambia mwongo, na ulimi wangu si mkunjufu wa kuweza kuhojiana nao kama ninavyo penda. Basi mtume Jibril ende kwa ndugu yangu aje kuniunga mkono katika hii kazi yangu.
Kiungo 26:13
14
وَلَهُمْ عَلَىَّ ذَنۢبٌۭ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ
Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa. [14]
Maelezo ya chini[14] Na watu hawa wana kisasi juu yangu. Kwani mimi nilimuuwa mtu katika wao. Basi nina khofu watakuja niuwa kwa kisasi kabla sijatimiza kazi yangu. Hayo yananizidisha khofu.
Kiungo 26:14
15
قَالَ كَلَّا ۖ فَٱذْهَبَا بِـَٔايَـٰتِنَآ ۖ إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ
Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. [15]
Maelezo ya chini[15] Mwenyezi Mungu akamwambia: Hawatokuuwa. Na kwa mintarafu ya Haruni nimekukubalia ombi lako. Basi nendeni nanyi mmejizatiti na miujiza yetu. Mimi niko pamoja nanyi kwa ulinzi. Nayasikia yanayo jiri baina yenu na Firauni. Nyinyi mtapata ushindi, na kuungwa mkono.
Kiungo 26:15
16
فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولُ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [16]
Maelezo ya chini[16] Muelekeeni Firauni na mwambieni: Sisi ni Watume wawili tumetumwa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Kiungo 26:16
17
أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
Waachilie Wana wa Israili wende nasi. [17]
Maelezo ya chini[17] Anakwambia Mola Mlezi wa walimwengu wote: Waachilie huru Wana wa Israili, wende nasi.
Kiungo 26:17
18
قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًۭا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ
(Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? [18]
Maelezo ya chini[18] Firauni akamwambia Musa kwa kumsimbulia, naye alimtambua walipo ingia na wakakadimisha Ujumbe wao, kwani alilelewa mle mle katika kasri lake: Hatukukulea sisi ulipo kuwa mtoto? Na ukaishi chini ya ulezi wetu kwa miaka mingi katika umri wako?
Kiungo 26:18
19
وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ ٱلَّتِى فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani? [19]
Maelezo ya chini[19] Na ukatenda makosa yako ya jinaya maovu kumuuwa mtu katika kaumu yangu, na ukazikanusha neema zangu nilizo kufanyia, hukuwahifadhi raia zangu, ukaushambulia ungu wetu kwa kudai kuwa wewe ati ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Kiungo 26:19
20
قَالَ فَعَلْتُهَآ إِذًۭا وَأَنَا۠ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ
(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea. [20]
Maelezo ya chini[20] Musa akasema: Niliyafanya uliyo yataja kwa kutojua yanayo faa kutambulikana kwa akili nayo ni jambo la kuuwa. Basi hapana masimbulizi juu yangu.
Kiungo 26:20
21
فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِى رَبِّى حُكْمًۭا وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
Basi nilikukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi, akanitunukia hukumu, na akanijaali niwe miongoni mwa Mitume. [21]
Maelezo ya chini[21] Nikakukimbieni nilipo khofu kuwa mtakuja niuwa kwa jinaya hii ambayo sikuukusudia. Mola wangu Mlezi akanitunukia fahamu na ilimu, kwa fadhila zake na neema zake, na akanifanya mmoja katika Mitume.
Kiungo 26:21
22
وَتِلْكَ نِعْمَةٌۭ تَمُنُّهَا عَلَىَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili? [22]
Maelezo ya chini[22] Musa akaashiria sifa katika sifa ovu kabisa za Firauni, nayo ni kuwa kawafanya watumwa Wana wa Israili, na akiwauwa watoto wao wanaume. Na akakataa kukuita kule kulelewa kwake katika jumba la Firauni kuwa ni neema, kwani yaliyo sabibisha hayo ni yale aliyo kwisha yataja, ndio yeye alitupwa mtoni aokoke asiuliwe. Akaishia kwenye jumba la Firauni. Na lau kuwa si hivyo basi angeli lelewa na wazazi wake.
Kiungo 26:22
23
قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote? [23]
Maelezo ya chini[23] Firauni akasema: Na nini hizo sifa za Mola Mlezi wa walimwengu wote ambaye unakithiri kumtaja, na wewe unadai kuwa ni Mtume wake, na hali sisi hatujui lolote khabari zake?
Kiungo 26:23
24
قَالَ رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini. [24]
Maelezo ya chini[24] Musa akasema: Yeye huyo ndiye Mwenye kuzimiliki mbingu na ardhi na kila kilio baina yao. Ikiwa nyinyi mna yakini ya ukweli wa jawabu hii basi mtanafiika, na mtaongoka, na mtajua kuwa ufalme wa Firauni wa kujidai haufui dafu mbele ya Ufalme wake Mwenyezi Mungu. Kwani ufalme wa Firauni haupindukii hata eneo moja katika hii dunia.
Kiungo 26:24
25
قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُۥٓ أَلَا تَسْتَمِعُونَ
(Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi? [25]
Maelezo ya chini[25] Firauni kuonyesha mastaajabu kwa wale walio mzunguka kwa kuwa Musa katika jawabu yake alipo mtaja Mola wake Mlezi na akadhukuru Ufalme wake hakuugusia hata kidogo ufalme wa Firauni, alisema: Mwayasikiaje maneno ya Musa?
Kiungo 26:25
26
قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ
(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza. [26]
Maelezo ya chini[26] Musa akiendelea na usemi wake bila ya kujali hasira za Firauni na uchafu wa maneno yake, akasema: Ndiye huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliye kuumbeni nyinyi na baba zenu walio tangulia. Na miongoni mwa hao walikuwako walio dai ungu kama unavyo dai wewe. Na wao wameteketea. Na wewe utateketea, na hayo unayo yadai yatapotelea mbali. Kwani Mungu wa kweli hafi.
Kiungo 26:26
27
قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِىٓ أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌۭ
(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. [27]
Maelezo ya chini[27] Firauni akwaambia watu wake yale yanayo mtibuwa roho na kumghadhibisha, akautaja Utume wa Musa ni kwao wao, wala si kwake yeye, na akambandikiza wazimu, kwa kuwa ati akiulizwa kitu hujibu kingine, na anamsifu Mola Mlezi kwa sifa za kiajabu ajabu. Na kwa hivyo Firauni anawahimiza wamkadhibishe.
Kiungo 26:27
28
قَالَ رَبُّ ٱلْمَشْرِقِ وَٱلْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ
. (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini. [28]
Maelezo ya chini[28] Musa akasema: Ikiwa nyinyi mna akili, basi uaminini Ujumbe wangu. Kwani kuchomoza jua na kuchwa kwake kwa mpango madhubuti ni dalili wazi ya Mwenye kuumba. Kwa hivyo basi ni nyinyi ndio mnastahiki kuambiwa wendawazimu.
Kiungo 26:28
29
قَالَ لَئِنِ ٱتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِى لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ ٱلْمَسْجُونِينَ
(Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani. [29]
Maelezo ya chini[29] Firauni akamwambia Musa: Ukimfuata mungu yeyote badala yangu mimi, utakuwa mmoja katika wanao ijua hali yao mbaya katika magereza yangu. Na yeye Firauni kaangukia kitisho hichi baada ya kushindwa kuondoa athari za kazi za Muumbaji.
Kiungo 26:29
30
قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَىْءٍۢ مُّبِينٍۢ
Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi? [30]
Maelezo ya chini[30] Musa akasema kwa upole kwa kutumai asaa akaamini: Utanitia gerezani hata nikikuletea ushahidi mkubwa wa ukweli wa haya niyasemayo?
Kiungo 26:30
31
قَالَ فَأْتِ بِهِۦٓ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli. [31]
Maelezo ya chini[31] Firauni akasema: Ulete ushahidi utao onyesha Unabii wako kama wewe kweli unasema kweli katika wito wako. Kasema hayo kwa tamaa ya kuwa huenda akapata kipengee cha udhaifu katika hoja zake.
Kiungo 26:31
32
فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعْبَانٌۭ مُّبِينٌۭ
Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri. [32]
Maelezo ya chini[32] Musa akaitupa fimbo yake mbele yao. Ikageuka nyoka kweli kweli, si kitu cha uwongo cha uchawi kinacho fanana na nyoka.
Kiungo 26:32
33
وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِىَ بَيْضَآءُ لِلنَّـٰظِرِينَ
Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao. [33]
Maelezo ya chini[33] Musa akautoa mkono wake kutoka mfukoni mwake. Hiyo ni Ishara ya pili. Nao ukawa mweupe, bila ya maradhi, hata wakashangaa watazamaji kwa kumetuka kwake.
Kiungo 26:33
34
قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُۥٓ إِنَّ هَـٰذَا لَسَـٰحِرٌ عَلِيمٌۭ
(Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu. [34]
Maelezo ya chini[34] Firauni akawaambia watu wake: Hakika Musa ni mchawi bingwa katika uchawi wake. Kasema hayo kwa kuchelea watu wake wasiifuate Haki waliyo iona kwa Musa.
Kiungo 26:34
35
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِۦ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ
Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani? [35]
Maelezo ya chini[35] Tena Firauni akasema: Mchawi huyu anataka kunifanyia kahari apate kukutoeni katika hii nchi yenu. Na haya ni uchochezi dhidi ya Musa, kwani katika la dhiki mno katika hayo yaliyo dhiki ni mtu kuiacha nchi yake, na khasa ikiwa kwa kahari. Naye akataka mawazo ya wale walio kuwa wanamuabudu. Kasahau ungu wake kwa nguvu za Ishara za Musa.
Kiungo 26:35
36
قَالُوٓا۟ أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَٱبْعَثْ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَـٰشِرِينَ
Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo. [36]
Maelezo ya chini[36] Watu wake wakamwambia: Akhirisha kukata shauri yao hawa, na uwatume askari wende wawakusanye wachawi katika raia zako. Kwani uchawi hupingwa kwa uchawi.
Kiungo 26:36
37
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍۢ
Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu. [37]
Maelezo ya chini[37] Watakuletea wengi, na wote wamebobea kwa uchawi, na wamemshinda Musa kwa ufundi na ustadi. Wamekusudia kwa haya kumpunguzia dukuduku lake Firauni.
Kiungo 26:37
38
فَجُمِعَ ٱلسَّحَرَةُ لِمِيقَـٰتِ يَوْمٍۢ مَّعْلُومٍۢ
Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu. [38]
Maelezo ya chini[38] Wakakusanywa wachawi kutoka kila upande wa nchi. Wakawekewa wakati wa mchana siku ya Sikukuu kukutana na Musa.
Kiungo 26:38
39
وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ
Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika? [39]
Maelezo ya chini[39] Na watu wakahimizana kuhudhuria siku hiyo waone ramsa wakiambizana: Mtakusanyika? Yaani ndio: Mkusanyike!
Kiungo 26:39
40
لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ ٱلسَّحَرَةَ إِن كَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ
Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda. [40]
Maelezo ya chini[40] Wakatangaza matarajio yao ya kushinda wachawi, ili wapate kuthibiti katika dini yao, na pia ndio kampeni ya nguvu na juhudi apate kushindwa Musa.
Kiungo 26:40
41
فَلَمَّا جَآءَ ٱلسَّحَرَةُ قَالُوا۟ لِفِرْعَوْنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ ٱلْغَـٰلِبِينَ
Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda? [41]
Maelezo ya chini[41] Walipo kuja wachawi kwa Firauni walimwambia: Je! Tutapata kwako ujira mkubwa pindi tukishinda?
Kiungo 26:41
42
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ إِذًۭا لَّمِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ
Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele. [42]
Maelezo ya chini[42] Firauni akasema: Naam, mtapata mnacho kisema. Na juu ya huo ujira mkubwa mtakuwa watu wa karibu kwangu, watu wa cheo na madaraka.
Kiungo 26:42
43
قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلْقُوا۟ مَآ أَنتُم مُّلْقُونَ
Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa. [43]
Maelezo ya chini[43] Ulipo fika wakati ulio wekwa katika siku iliyo pangwa Musa aliwaambia wachawi: Tupeni huo uchawi mnao taka kuutupa.
Kiungo 26:43
44
فَأَلْقَوْا۟ حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا۟ بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ ٱلْغَـٰلِبُونَ
Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda. [44]
Maelezo ya chini[44] Wakazitupa kamba zao na fimbo zao, na watu wakazugwa wakaona kama ni nyoka wanakwenda. Wakaapa kwa utukufu wa Firauni na nguvu zake hapana shaka hawa leo watashinda
Kiungo 26:44
45
فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ
Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua. [45]
Maelezo ya chini[45] Musa tena akatupa fimbo yake. Mara ikawa joka kubwa likaingia kuvimeza vile walivyo vizua kwa uchawi, navyo ni kamba na fimbo, wakidanganya kuwa ni nyoka wanao kwenda.
Kiungo 26:45
46
فَأُلْقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سَـٰجِدِينَ
Hapo wachawi walipinduka wakasujudu. [46]
Maelezo ya chini[46] Wachawi wakaanguka wakasujudu kumsujudia Mwenyezi Mungu, walipo yakinika kuwa mambo ya Musa si uchawi.
Kiungo 26:46
47
قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote. [47]
Maelezo ya chini[47] Wakasema ili kutia mkazo kule kusujudu kwao kwa kauli yao: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Kiungo 26:47
48
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ
Mola Mlezi wa Musa na Harun. [48]
Maelezo ya chini[48] Na wakabainisha kuwa hakika Mola Mlezi wa walimwengu wote walio muamini ndiye: Mola Mlezi wa Musa na Harun.
Kiungo 26:48
49
قَالَ ءَامَنتُمْ لَهُۥ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِى عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَـٰفٍۢ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ
(Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote. [49]
Maelezo ya chini[49] Firauni kwa kukasarika kuwa wale wachawi wamemuamini Musa bila ya yeye kuwapa ruhusa, aliwatishia ya kwamba yeye ndiye mwalimu wao aliye wafunza fani za uchawi, na watakuja jua adhabu itakayo wateremkia. Akawaambia: Nitakata mikono yenu na miguu yenu mbali mbali, nitakata wa kulia huu kwa wa kushoto huu, na kinyume cha hayo. Na nyote nitakutundikeni juu ya misalaba.
Kiungo 26:49
50
قَالُوا۟ لَا ضَيْرَ ۖ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ
Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. [50]
Maelezo ya chini[50] Wachawi wakasema: Hapana la kutudhuru sisi kwa adhabu unazo tutishia, kwani sisi ni wenye kurejea kwenye malipo ya Mola wetu Mlezi. Na Yeye ndiye mbora wa kulipa na mbora wa kuadhibu.
Kiungo 26:50
51
إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَـٰيَـٰنَآ أَن كُنَّآ أَوَّلَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini. [51]
Maelezo ya chini[51] Hakika sisi tunataraji Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu tuliyo yafanya zamani, kwa kuwa sisi ndio wa mwanzo wa Waumini katika kaumu yako.
Kiungo 26:51
52
۞ وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِىٓ إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa. [52]
Maelezo ya chini[52] Na Mwenyezi Mungu alimpa wahyi Musa a.s. atoke usiku usiku pamoja na Waumini miongoni mwa Wana wa Israili, ilipo kuwa tena haiwi kumsubirisha Musa. Mpango ukawa wa makundi mawili kwamba atangulie Musa na kaumu yake, na Firauni afuatie na kaumu yake, mpaka waingie katika maingilio ya njia ya baharini, na Mwenyezi Mungu awateketeze.
Kiungo 26:52
53
فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَـٰشِرِينَ
Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo. [53]
Maelezo ya chini[53] Firauni akawatuma askari wake katika miji ya mamlaka yake, wawakusanye wenye maguvu katika kaumu yake, alipo jua kuwa Musa kesha toka na Wana wa Israili, ili awazuie lile walilo kusudia.
Kiungo 26:53
54
إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَشِرْذِمَةٌۭ قَلِيلُونَ
(Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo. [54]
Maelezo ya chini[54] Firauni akasema: Hakika hawa Wana wa Israili walio kimbia na Musa ni taifa dogo kwa nguvu zao. Idadi yao ni chache. Anasema hayo kutia mori katika nyoyo za askari wake.
Kiungo 26:54
55
وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَآئِظُونَ
Nao wanatuudhi. [55]
Maelezo ya chini[55] Na wao juu ya hivyo, wanatutibua roho kwa kuvunja amri yetu na kutoka bila ya idhini yetu.
Kiungo 26:55
56
وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَـٰذِرُونَ
Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari. [56]
Maelezo ya chini[56] Na sisi ni wengi. Miongoni mwa ada zetu ni kuchukua hadhari, na kuwa macho, na kupania.
Kiungo 26:56
57
فَأَخْرَجْنَـٰهُم مِّن جَنَّـٰتٍۢ وَعُيُونٍۢ
Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem, [57]
Maelezo ya chini[57] Tukawatoa Firauni na askari wake kwenye nchi yao iliyo fanana na mabustani yapitiwayo na mito kati yao, wakaangamia kwa kujitenga kwao na Haki, na kuchochewa kutaka kumfuatia Musa, kama ilivyo kuja katika Aya tatu zilizo tangulia.
Kiungo 26:57
58
وَكُنُوزٍۢ وَمَقَامٍۢ كَرِيمٍۢ
Na makhazina, na vyeo vya hishima, [58]
Maelezo ya chini[58] Tukawatoa, kadhaalika, kwenye khazina za dhahabu na fedha, na majumba waliyo kuwa wakiyakalia, wakineemeka kwa uzuri wake na ubora wa starehe zake.
Kiungo 26:58
59
كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَـٰهَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili. [59]
Maelezo ya chini[59] Ni kutoka kama huku kwa ajabu tulivyo kueleza ndivyo tulivyo watoa, na tukawapa ufalme huo na kila namna ya neema zilizo kuwamo Wana wa Israili, baada ya kuwa masikini hawana mbele wala nyuma.
Kiungo 26:59
60
فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ
Basi wakawafuata lilipo chomoza jua. [60]
Maelezo ya chini[60] Firauni na watu wake wakakaza mwendo ili wapate kuwawahi Wana wa Israili. Wakawakuta wakati wa kuchomoza jua.
Kiungo 26:60
61
فَلَمَّا تَرَٰٓءَا ٱلْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَـٰبُ مُوسَىٰٓ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ
Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana! [61]
Maelezo ya chini[61] Walipo onana makundi mawili, watu wa Musa walisema: Hakika Firauni na watu wake watatupata. Basi tutaangamia.
Kiungo 26:61
62
قَالَ كَلَّآ ۖ إِنَّ مَعِىَ رَبِّى سَيَهْدِينِ
(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! [62]
Maelezo ya chini[62] Musa akasema: Hakika mimi ninao uangalizi wa Mwenyezi Mungu unao nifuata kwa kunihifadhi. Na Yeye ataniongoza kwenye Njia ya uwokovu. Amesema hayo ili awatuze kuwa watasalimika, na iwe mbali na mawazo yao fikra ya kutisha kwamba takuja patikana. .
Kiungo 26:62
63
فَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضْرِب بِّعَصَاكَ ٱلْبَحْرَ ۖ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍۢ كَٱلطَّوْدِ ٱلْعَظِيمِ
Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. [63]
Maelezo ya chini[63] Tukamuamrisha Musa kwa wahyi, ufunuo, aipige bahari kwa fimbo yake. Ikapasuka bahari njia kumi na mbili kwa mujibu wa idadi ya mataifa ya Wana wa Israili. Kila njia katika hizo njia ilikuwa na kizuizi cha maji yaliyo nyanyuka kama mlima ulio simama imara.
Kiungo 26:63
64
وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ ٱلْـَٔاخَرِينَ
Na tukawajongeza hapo wale wengine. [64]
Maelezo ya chini[64] Tukawajongeza Firauni na kaumu yake mpaka wakaingia kwenye zile njia nyuma ya Musa na kaumu yake.
Kiungo 26:64
65
وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجْمَعِينَ
Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote. [65]
Maelezo ya chini[65] Tukamwokoa Musa na walio kuwa pamoja naye kwa hifadhi ya bahari nayo imeshikamana, mpaka wakamalizika kuvuka.
Kiungo 26:65
66
ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
Kisha tukawazamisha hao wengine. [66]
Maelezo ya chini[66] Kisha tukamzamisha Firauni pamoja na walio kuwa pamoja naye kwa kuwafudikiza kwa maji pale walipo wafuata.
Kiungo 26:66
67
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini. [67]
Maelezo ya chini[67] Hakika katika vituko hivi vya ajabu vya kiungu pana funzo la kuzingatia kwa atakaye kunafiika. Lakini watu wengi si wenye kusadiki.
Kiungo 26:67
68
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [68]
Maelezo ya chini[68] Hakika Muumba wako na Mlezi wako ndiye huyo Mwenye nguvu katika kuwaadhibu wanao kanusha, Mwenye kuwaneemesha kwa rehema Waumini.
Kiungo 26:68
69
وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَٰهِيمَ
Na wasomee khabari za Ibrahim. [69]
Maelezo ya chini[69] Ewe Mtume! Na wasomee makafiri hadithi ya Ibrahim , Alayhi Ssalaam.
Kiungo 26:69
70
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَا تَعْبُدُونَ
Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini? [70]
Maelezo ya chini[70] Alipo mwambia baba yake: Mnaabudu kitu gani hichi, ambacho hakifai kuabudiwa? Anakusudia kwa hayo kuyakebehi masanamu.
Kiungo 26:70
71
قَالُوا۟ نَعْبُدُ أَصْنَامًۭا فَنَظَلُّ لَهَا عَـٰكِفِينَ
Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea. [71]
Maelezo ya chini[71] Wakasema kujibu kwa njia ya kujitapa: Tunaabudu masanamu, nasi tunadumu daima dawamu tukiyaabudu, kwa kuyaadhimisha na kuyatukuza!
Kiungo 26:71
72
قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ
Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita? [72]
Maelezo ya chini[72] Ibrahim akasema: Kwani yanasikia madua yenu? Au yanakuitikieni mnapo yaomba? Kwa hayo anakusudia kuwanabihisha upotovu wa mwendo wao.
Kiungo 26:72
73
أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ
Au yanakufaeni, au yanakudhuruni? [73]
Maelezo ya chini[73] Au yanakuleteeni manufaa mnapo yat'ii? Au yanakupatilizeni kwa madhara mkiyaasi?
Kiungo 26:73
74
قَالُوا۟ بَلْ وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ
Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo. [74]
Maelezo ya chini[74] Wakasema: Hawafanyi lolote katika hayo. Lakini sisi tumewakuta baba zetu wakiyaabudu mfano wa ibada yetu. Basi sisi tukawafwata kwa waliyo kuwa wakiyafanya.
Kiungo 26:74
75
قَالَ أَفَرَءَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ
Je! Mmewaona hawa mnao waabudu- [75]
Maelezo ya chini[75] Ibrahim akasema kwa kuwasusuika: Je! Mlifikiri hata mkalijua jambo lolote lilio kupelekeeni kudumu na kuyaabudu hayo masanamu?
Kiungo 26:75
76
أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلْأَقْدَمُونَ
Nyinyi na baba zenu wa zamani? [76]
Maelezo ya chini[76] Nyinyi na baba zenu wa zamani - ati haya yanastahiki kuabudiwa au la? Lau mngeli zingatia mngeli jua kuwa hakika nyinyi mko katika upotovu ulio wazi.
Kiungo 26:76
77
فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّۭ لِّىٓ إِلَّا رَبَّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [77]
Maelezo ya chini[77] Kwani hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni maaadui kwangu mimi na kwenu. Basi mimi siwaabudu hao. Lakini ninaye muabudu na najijongeza kwake ni Muumba wa walimwengu wote, na Mwenye kumiliki mambo yao, na Mwenye kuwalinda.
Kiungo 26:77
78
ٱلَّذِى خَلَقَنِى فَهُوَ يَهْدِينِ
Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa, [78]
Maelezo ya chini[78] Ambae ndiye aliye nizua kabla sijawa chochote akaniumba kwa bora ya umbo, na akanitunukia uwongofu wa kunifikishia kwenye mafanikio yangu ya duniani na Akhera.
Kiungo 26:78
79
وَٱلَّذِى هُوَ يُطْعِمُنِى وَيَسْقِينِ
Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha. [79]
Maelezo ya chini[79] Na Yeye ndiye aliye nineemesha kwa vyakula na vinywaji, na akaniwezesha kuvipata na kunafiika kwavyo, ili kuhifadhi uhai wangu.
Kiungo 26:79
80
وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ
Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha. [80]
Maelezo ya chini[80] Na yakinishukia maradhi ni Yeye ndiye anaye niponesha, kwa kunisahilishia sababu za kupona na kuniwezesha kuzipata.
Kiungo 26:80
81
وَٱلَّذِى يُمِيتُنِى ثُمَّ يُحْيِينِ
Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha. [81]
Maelezo ya chini[81] Na Yeye ndiye atanifisha ikifika ajali yangu, na tena atanihuisha mara nyengine kwa ajili ya hisabu na malipo.
Kiungo 26:81
82
وَٱلَّذِىٓ أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِى خَطِيٓـَٔتِى يَوْمَ ٱلدِّينِ
Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo. [82]
Maelezo ya chini[82] Na Yeye ndiye ninaye mtumai kunighufiria na kuyasemehe makosa yangu madogo madogo ya kujikwaa duniani, utapo fika wakati wa hisabu.
Kiungo 26:82
83
رَبِّ هَبْ لِى حُكْمًۭا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّـٰلِحِينَ
Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. [83]
Maelezo ya chini[83] Ibrahim a.s. akasema kwa kuomba: Mola wangu Mlezi! Nitunukie ukamilifu wa ilimu na vitendo, ili nipate kustahili kuubeba Ujumbe wako na hukummu kwa waja wako, na niwezeshe niungane pamoja na kundi la watendao wema.
Kiungo 26:83
84
وَٱجْعَل لِّى لِسَانَ صِدْقٍۢ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye. [84]
Maelezo ya chini[84] Na nijaalie nipate sifa nzuri na kumbusho jema kwa kaumu zitazo kuja baada yangu, mabaki yake yasalie mpaka Siku ya Kiyama.
Kiungo 26:84
85
وَٱجْعَلْنِى مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ
Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. [85]
Maelezo ya chini[85] Na nijaalie katika waja wako ulio watunukia neema za Peponi, kuwa ni malipo kwa sababu ya Imani yao kukuamini Wewe, na ibada yao kukuabudu Wewe.
Kiungo 26:85
86
وَٱغْفِرْ لِأَبِىٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ
Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu. [86]
Maelezo ya chini[86] Na mjaalie baba yangu astahili msamaha kwa kumwezesha kuwa Muislamu. Na yeye alikuwa kamuahidi kusilimu siku alio achana naye, kwani yeye huyo baba alikuwa ameitupa kando njia ya uwongofu na uwongozi.
Kiungo 26:86
87
وَلَا تُخْزِنِى يَوْمَ يُبْعَثُونَ
Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa. [87]
Maelezo ya chini[87] Wala usinitie aibu au hizaya mbele ya watu, Siku watapo tolewa makaburini kwa ajili ya hisabu na malipo.
Kiungo 26:87
88
يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌۭ وَلَا بَنُونَ
Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. [88]
Maelezo ya chini[88] Siku ambayo hapana mtu ataye nafiika kwa mali ayatoe, au kwa wana wamsaidie.
Kiungo 26:88
89
إِلَّا مَنْ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلْبٍۢ سَلِيمٍۢ
Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. [89]
Maelezo ya chini[89] Isipo kuwa aliye kuwa Muumini, na akamkabili Mwenyezi Mungu na moyo ulio mzima, hauna maradhi ya ukafiri, na unaafiki, na riya (kujionesha).
Kiungo 26:89
90
وَأُزْلِفَتِ ٱلْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ
Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu. [90]
Maelezo ya chini[90] Na Pepo itajongezwa, na itakaribishwa pahala pa watu wema. Basi wataiendea wale walio jikinga na ukafiri na maasi, na wakaikubali Imani na ut'iifu duniani.
Kiungo 26:90
91
وَبُرِّزَتِ ٱلْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu. [91]
Maelezo ya chini[91] Na Moto utaletwa mbele ya walio iacha Dini ya Haki, mpaka ndimi zake zikaribie kuwanyakua, nao watakuwa majutoni.
Kiungo 26:91
92
وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ
Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu [92]
Maelezo ya chini[92] Wakaambiwa kwa kuwatahayarisha: Iko wapi hiyo miungu yenu mliyo kuwa mkiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu?
Kiungo 26:92
93
مِن دُونِ ٱللَّهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ
Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe? [93]
Maelezo ya chini[93] Badala ya Mwenyezi Mungu, na mnadai kuwa ati ndio itakuombeeni hii leo? Je! Inakufaeni kitu kwa kukunusuruni, au hata inajifaa wenyewe kujisaidia? Hapana lolote. Kwani wao na miungu yao ni kuni za Moto.
Kiungo 26:93
94
فَكُبْكِبُوا۟ فِيهَا هُمْ وَٱلْغَاوُۥنَ
Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu, [94]
Maelezo ya chini[94] Watatumbukizwa katika Jahannamu kifudifudi, wakipinduliwa pinduliwa mpaka waishie ndani kabisa shimoni, wao na walio wapoteza na wakawatia katika madhambi na upotovu.
Kiungo 26:94
95
وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ
Na majeshi ya Ibilisi yote. [95]
Maelezo ya chini[95] Na pamoja nao watakuwapo wasaidizi wa Ibilisi walio kuwa wakiwapambia shari na madhambi, au wale watu na majini walio wakiwafuata katika maasi.
Kiungo 26:95
96
قَالُوا۟ وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ
Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo: [96]
Maelezo ya chini[96] Watasema huku wakiungama makosa yao, na huku wanagombana na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu:
Kiungo 26:96
97
تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِى ضَلَـٰلٍۢ مُّبِينٍ
Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri, [97]
Maelezo ya chini[97] Wallahi! Hakika sisi tulikuwa katika dunia yetu tumepotea kweli, na wajinga wa kutupwa, na tumeiacha Haki ambayo haina kificho ndani yake.
Kiungo 26:97
98
إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote. [98]
Maelezo ya chini[98] Pale tulipo kufanyeni nyinyi tulio kuabuduni badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ati ni sawa sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote katika kustahiki kuabudiwa, juu ya kuwa hamjiwezi wala hamfai kwa lolote.
Kiungo 26:98
99
وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلْمُجْرِمُونَ
Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote. [99]
Maelezo ya chini[99] Wala hapana walio tutia katika hilaki hii ila wakosefu walio tupotoa tukaiwacha Njia Iliyo Nyooka.
Kiungo 26:99
100
فَمَا لَنَا مِن شَـٰفِعِينَ
Basi hatuna waombezi. [100]
Maelezo ya chini[100] Basi hapana wa kuombwa akaja kutuvua na adhabu hii kama tulivyo dhania pale kwanza.
Kiungo 26:100
101
وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍۢ
Wala rafiki wa dhati. [101]
Maelezo ya chini[101] Wala hapana rafiki wa kuwaonea uchungu kwa hali yao, licha ya kuwaokoa.
Kiungo 26:101
102
فَلَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةًۭ فَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini. [102]
Maelezo ya chini[102] Basi hapo ndio wanajitamania nafsi zao lau wangeli rejea duniani wapate kuwa Waumini ili waokoke.
Kiungo 26:102
103
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. [103]
Maelezo ya chini[103] Na hakika katika khabari za Ibrahim zilizo tajwa yapo mawaidha na mazingatio kwa mwenye kutaka mawaidha na akazingatia. Na wala si wengi katika watu wako wanao somewa khabari hizi wenye kuitikia wito wako.
Kiungo 26:103
104
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [104]
Maelezo ya chini[104] Na hakika hapana shaka Mola wako Mlezi ni Muweza wa kuwaadhibu wanao kadhibisha, naye ni Mfadhili wa watu wema kwa neema nyingi.
Kiungo 26:104
105
كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ ٱلْمُرْسَلِينَ
Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume. [105]
Maelezo ya chini[105] Na Mwenyezi Mungu ametaja khabari za Nuhu kwa kauli yake: Kaumu ya Nuhu iliukanusha Utume wake, wakamrudishia mwenyewe. Kwa kitendo hicho ikawa wamewakadhibisha Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa wito wao ni mmoja katika asli yake na lengo lake.
Kiungo 26:105
106
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?. [106]
Maelezo ya chini[106] Waliukanusha Utume huu pale alipo waambia ndugu yao Nuhu - ndugu kwa makhusiano ya nasaba si kwa Dini - akiwahadharisha: Hamumchi Mwenyezi Mungu, mkaacha kuabudu wenginewe?
Kiungo 26:106
107
إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌۭ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. [107]
Maelezo ya chini[107] Hakika mimi ni Mtume, nimetumwa kwenu nikuongoeni kwenye Njia ya wongofu, na ni muaminifu wa kufikisha huu Ujumbe.
Kiungo 26:107
108
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. [108]
Maelezo ya chini[108] Basi mkhofuni Mwenyezi Mungu, na fuateni amri yangu katika hayo ninayo kuitieni kwayo ya kumuamini Mwenyezi Mungu wa pekee na kumt'ii.
Kiungo 26:108
109
وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [109]
Maelezo ya chini[109] Na wala sitaki kwenu ujira kwa ajili ya ninayo kupeni ya nasaha na wito. Na sina malipo ila kwa Mwenye kuwaumba viumbe wote, Aliye miliki mambo yao.
Kiungo 26:109
110
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. [110]
Maelezo ya chini[110] Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na fuateni ninayo kuamrisheni.
Kiungo 26:110
111
۞ قَالُوٓا۟ أَنُؤْمِنُ لَكَ وَٱتَّبَعَكَ ٱلْأَرْذَلُونَ
Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?. [111]
Maelezo ya chini[111] Watu wa Nuhu, huku wakiukataa wito wake, walisema: Hatutokuwa na imani nawe maadamu wanakufuata watu duni kabisa, wasio kuwa na hadhi wala mali.
Kiungo 26:111
112
قَالَ وَمَا عِلْمِى بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?. [112]
Maelezo ya chini[112] Nuhu akasema: Kitu gani cha kunijuvya uchache wa hadhi yao na mali yao? Nikitakacho mimi kwao ni Imani yao bila ya kutafuta kuzijua kazi zao.
Kiungo 26:112
113
إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّى ۖ لَوْ تَشْعُرُونَ
Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!. [113]
Maelezo ya chini[113] Hapana wa kuwalipa kwa vitendo vyao na kazi zao ila Mola wangu Mlezi; kwani Yeye ndiye anaye yajua vyema ya undani wao. Kama nyinyi ni watu watambuzi mngeli tambua hayo.
Kiungo 26:113
114
وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. [114]
Maelezo ya chini[114] Wala mimi siye wa kuwafukuza watu wanao uamini wito wangu vyovyote itavyo kuwa hali yao ya ufakiri au utajiri, kwa sababu ati ya kukubalieni nyinyi kwa mtakalo ili ndio mpate kuniamini.
Kiungo 26:114
115
إِنْ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٌۭ مُّبِينٌۭ
Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri. [115]
Maelezo ya chini[115] Mimi si chochote ila ni Mtume niliye toka kwa Mwenyezi Mungu kuwaonya walio wajibikiwa kwa onyo lilio wazi, kwa ushahidi wa kutenganisha baina ya kweli na uwongo, bila ya farka yoyote baina ya mtukufu na mnyonge. Basi vipi itanifalia mimi kuwafukuza Waumini kwa sababu ya ufakiri wao?
Kiungo 26:115
116
قَالُوا۟ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَـٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمَرْجُومِينَ
Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. [116]
Maelezo ya chini[116] Wakasema: Ewe Nuhu! Ikiwa hutoacha huu wito wako basi jua yakini tutakupopoa mawe. Yaani wanakusudia kwa haya kumtishia kumuuwa.
Kiungo 26:116
117
قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِى كَذَّبُونِ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. [117]
Maelezo ya chini[117] Nuhu kuonyesha kushikilia watu wake kuukadhibisha wito wake, alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha! Kuthibitisha kuwa wanastahiki maapizo yake.
Kiungo 26:117
118
فَٱفْتَحْ بَيْنِى وَبَيْنَهُمْ فَتْحًۭا وَنَجِّنِى وَمَن مَّعِىَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. [118]
Maelezo ya chini[118] Basi tuhukumie baina yangu na wao, kwa hukumu ya kuwaangamiza wanao pinga Upweke wako, na wakamkadhibisha Mtume wako! Na niokoe mimi na Waumini walio pamoja nami na adhabu ya uasi wao.
Kiungo 26:118
119
فَأَنجَيْنَـٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ
Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. [119]
Maelezo ya chini[119] Ndio hivyo tukamwokoa yeye pamoja na walio amini katika safina iliyo pakia pomoni wao hao pamoja na mahitaji yao, kwa kuitikia dua yake.
Kiungo 26:119
120
ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ ٱلْبَاقِينَ
Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia. [120]
Maelezo ya chini[120] Baada ya kuokoka kwa Nuhu na walio amini, Mwenyezi Mungu aliwazamisha walio baki katika kaumu ya Nuhu walio kuwa hawakuamini.
Kiungo 26:120
121
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [121]
Maelezo ya chini[121] Hakika katika yaliyo simuliwa na Qur'ani juu ya khabari za Nuhu ni hoja ya kuthibitisha ukweli wa Mitume na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na katika watu walio somewa hadithi hizi si wengi walio amini.
Kiungo 26:121
122
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Kina A'd waliwakanusha Mitume. [122]
Maelezo ya chini[122] Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu za kumuadhibu kila jabari mwenye inda, Mwenye kuwaneemesha wachamngu kwa kila namna ya fadhila.
Kiungo 26:122
123
كَذَّبَتْ عَادٌ ٱلْمُرْسَلِينَ
Kina A'd waliwakanusha Mitume. [123]
Maelezo ya chini[123] Kabila ya A'di ilimkanusha Mtume wao Hud a.s. Na kwa hivyo wakawa ndio wamewakadhibisha Mitume wote, kwa kuwa wito wao ni mmoja katika asli yake na lengo lake.
Kiungo 26:123
124
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu? [124]
Maelezo ya chini[124] Alipo waambia ndugu yao Hud: Hamumwogopi Mwenyezi Mungu, mkamsafia ibada?
Kiungo 26:124
125
إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌۭ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. [125]
Maelezo ya chini[125] Hakika mimi nimetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili nikuongoeni mfuate uwongozi, na ni mwenye kuulinda ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Naufikisha ujumbe huo kama alivyo niamrisha Mola wangu Mlezi.
Kiungo 26:125
126
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. [126]
Maelezo ya chini[126] Basi ifuateni amri ya Mwenyezi Mungu. Na ikhofuni adhabu yake. Na t'iini ninayo kuamrisheni yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu.
Kiungo 26:126
127
وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [127]
Maelezo ya chini[127] Wala kwa hii nasaha yangu na uwongozi wangu sitaki kwenu ujira. Sina malipo isipo kuwa kwa Muumba wa viumbe vyote.
Kiungo 26:127
128
أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةًۭ تَعْبَثُونَ
Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi? [128]
Maelezo ya chini[128] Je! Mnasimamisha juu ya kila pahala palipo nyanyuka katika nchi jengo refu kwa ajili ya kujifakhirisha, na mnakutana humo kwa mambo ya upuuzi na fisadi? Mwenyezi Mungu Subhanahu anataka kwa haya kuwazindua watende yatakayo wanufaisha, na anawatahayarisha kwa kuacha kwao Imani na vitendo vyema.
Kiungo 26:128
129
وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمْ تَخْلُدُونَ
Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele! [129]
Maelezo ya chini[129] Na mnajenga majumba ya fakhari na imara, na mahodhi ya maji, kwa kutaraji kuishi milele katika dunia hii, kama kwamba hamtakufa.
Kiungo 26:129
130
وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ
Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari. [130]
Maelezo ya chini[130] Na mnapo ingia kutesa, mnapita kiasi katika uasi na uvamizi wa jeuri, mnauwa, na mnapiga kwa chuki bila ya huruma.
Kiungo 26:130
131
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. [131]
Maelezo ya chini[131] Mwogopeni Mwenyezi Mungu katika kutumia nguvu, Na fuateni amri yangu katika ninayo kuitieni. Kwani hayo hakika ndiyo yatakayo kukufaeni na ndiyo yatakayo dumu zaidi.
Kiungo 26:131
132
وَٱتَّقُوا۟ ٱلَّذِىٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعْلَمُونَ
Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua. [132]
Maelezo ya chini[132] Na tahadharini na ghadhabu za Mwenyezi Mungu aliye kukunjulieni neema zake, kwa mnayo yajua yaliyo mbele yenu ya vipawa vyake vya namna mbali mbali.
Kiungo 26:132
133
أَمَدَّكُم بِأَنْعَـٰمٍۢ وَبَنِينَ
Amekupeni wanyama wa kufuga na wana. [133]
Maelezo ya chini[133] Kama alivyo kupeni mifugo kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, na wana wenye nguvu, wakukulindieni mifugo yenu, na kukusaidieni katika shida za maisha.
Kiungo 26:133
134
وَجَنَّـٰتٍۢ وَعُيُونٍ
Na mabustani na chemchem. [134]
Maelezo ya chini[134] Na mabustani yenye matunda, na chemchem zenye kutiririka maji mnayo yahitajia.
Kiungo 26:134
135
إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍۢ
Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa. [135]
Maelezo ya chini[135] Mimi nina khofu asije Mwenyezi Mungu akakuteremshieni adhabu kali hapa duniani, na Akhera akakutieni katika Moto wa Jahannamu kwa sababu ya ujabari wenu na starehe alizo kustarehesheni Mwenyezi Mungu.
Kiungo 26:135
136
قَالُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْنَآ أَوَعَظْتَ أَمْ لَمْ تَكُن مِّنَ ٱلْوَٰعِظِينَ
Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha. [136]
Maelezo ya chini[136] Wakasema kwa kumkejeli: Ni sawa kwetu, ukitupa waadhi na kutuonya au ukawa si katika wenye kutoa waadhi.
Kiungo 26:136
137
إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلْأَوَّلِينَ
Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani. [137]
Maelezo ya chini[137] Haya uliyo tuletea si lolote ila ni uwongo na upotovu wa watu wa zamani. Wao wamezoea kuzua kama hivyo. Kwa hivyo sisi hatutaacha tuliyo kuwa nayo.
Kiungo 26:137
138
وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ
Wala sisi hatutaadhibiwa. [138]
Maelezo ya chini[138] Wala sisi hatutaadhibiwa kwa vitendo tuvitendavyo.
Kiungo 26:138
139
فَكَذَّبُوهُ فَأَهْلَكْنَـٰهُمْ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. [139]
Maelezo ya chini[139] Basi wakaendelea kushikilia kumkanusha. Mwenyezi Mungu akawafanyia haraka kuwateketeza. Hakika katika hayo aliyo wateremshia Mwenyezi Mungu kina A'di kwa kuwa ni malipo kwa ukanushi wao, ni hoja inayo juulisha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na si wengi katika wanao somewa khabari za A'adi walio Waumini.
Kiungo 26:139
140
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [140]
Maelezo ya chini[140] Na Mola wako Mlezi ndiye Mtenda nguvu wa kuwashinda hao majabari, Mwenye kuwarehemu Waumini.
Kiungo 26:140
141
كَذَّبَتْ ثَمُودُ ٱلْمُرْسَلِينَ
Kina Thamud waliwakanusha Mitume. [141]
Maelezo ya chini[141] Kabila ya Thamud ilimkanusha Swaleh katika Ujumbe wake na wito wake, na kwa hivyo ikawa wamewakanusha Mitume wote, kwa kuwa asli ya Ujumbe ni moja, na lengo ni moja.
Kiungo 26:141
142
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ صَـٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao Swaleh: Je! Hamumchimngu? [142]
Maelezo ya chini[142] Ewe Mtume! Watajie watu wako, wakati ule kina Thamud walipo ambiwa na ndugu yao kwa uzao na uwananchi, si kwa dini, Swaleh: Hamumwogopi Mwenyezi Mungu, mkamuaabudu Yeye tu?
Kiungo 26:142
143
إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌۭ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. [143]
Maelezo ya chini[143] Hakika mimi nimetumwa na Mwenyezi Mungu kwenu kwa mambo yenye kheri yenu na mafanikio yenu. Na mimi ni mwenye kuuhifadhi Ujumbe huu kama nilivyo upokea kwa Mwenyezi Mungu.
Kiungo 26:143
144
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. [144]
Maelezo ya chini[144] Kwa hivyo tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na nifuateni kwa haya ninayo kuitieni kwayo kutokana na amri zake.
Kiungo 26:144
145
وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [145]
Maelezo ya chini[145] Wala sitaki kwenu ujira wowote kwa hii nasaha yangu na uwongozi wangu. Ujira wangu uko kwa Mwenye kumiliki walimwengu wote.
Kiungo 26:145
146
أَتُتْرَكُونَ فِى مَا هَـٰهُنَآ ءَامِنِينَ
Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa? [146]
Maelezo ya chini[146] Lilio wazuia ni kule kuamini kwao kwamba ati wataselelea katika zile starehe, watasalimika na adhabu, na kutoweka, na mauti,
Kiungo 26:146
147
فِى جَنَّـٰتٍۢ وَعُيُونٍۢ
Katika mabustani, na chemchem? [147]
Maelezo ya chini[147] Katika mabustani ya matunda, na chemchem zenye kutoa maji matamu,
Kiungo 26:147
148
وَزُرُوعٍۢ وَنَخْلٍۢ طَلْعُهَا هَضِيمٌۭ
Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva. [148]
Maelezo ya chini[148] Na konde zilizo wiva, na mitende ambayo mazao yake yamedhihiri mapevu na laini.
Kiungo 26:148
149
وَتَنْحِتُونَ مِنَ ٱلْجِبَالِ بُيُوتًۭا فَـٰرِهِينَ
Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi. [149]
Maelezo ya chini[149] Na mnachonga milimani majumba kwa ufundi na ustadi katika hayo mnayo yaunda.
Kiungo 26:149
150
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. [150]
Maelezo ya chini[150] Basi iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuto mshukuru kwenu kwa neema zake; na pokeeni nasiha yangu na muitende.
Kiungo 26:150
151
وَلَا تُطِيعُوٓا۟ أَمْرَ ٱلْمُسْرِفِينَ
Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka,. [151]
Maelezo ya chini[151] Wala msiit'ii amri ya walio pindukia mipaka kwa ushirikina na kufuata pumbao na matamanio.
Kiungo 26:151
152
ٱلَّذِينَ يُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ
Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi. [152]
Maelezo ya chini[152] Ambao wanapitisha maisha yao katika ardhi kwa uharibifu, wala hawafanyi ya maslaha ya kutengeneza nchi.
Kiungo 26:152
153
قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلْمُسَحَّرِينَ
Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa. [153]
Maelezo ya chini[153] Wakasema: Wewe si chochote isipo kuwa miongoni mwa walio rogwa kikweli mpaka zikapotea akili zao. Na katika jawabu hii mna ukali na usafihi.
Kiungo 26:153
154
مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌۭ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. [154]
Maelezo ya chini[154] Wewe si chochote ila ni mmoja unaye fanana na sisi kwa ubinaadamu, basi yawaje uwe bora kuliko sisi kwa Unabii na Utume? Na ukiwa wewe ni mkweli katika madai yako basi lete muujiza wa kuonyesha uthibitisho wa Utume wako.
Kiungo 26:154
155
قَالَ هَـٰذِهِۦ نَاقَةٌۭ لَّهَا شِرْبٌۭ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍۢ مَّعْلُومٍۢ
Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu. [155]
Maelezo ya chini[155] Saleh akawaambia - alipo pewa na Mwenyezi Mungu ngamia jike kuwa ni muujiza wake: Huyu hapa ngamia jike wa Mwenyezi Mungu, amekutoleeni kuwa ni Ishara. Yeye ana sehemu yake ya maji katika siku moja; siku hiyo msinywe nyinyi. Na nyinyi mna sehemu yenu siku nyengine. Kunyweni siku hiyo.
Kiungo 26:155
156
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٍۢ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍۢ
Wala ms!imguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa. [156]
Maelezo ya chini[156] Wala msimletee madhara yoyote huyu ngamia, msije mkahiliki kwa adhabu kubwa.
Kiungo 26:156
157
فَعَقَرُوهَا فَأَصْبَحُوا۟ نَـٰدِمِينَ
Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta. [157]
Maelezo ya chini[157] Wakamchinja ngamia, kinyume na walivyo wafikiana na Swaleh. Kwa hivyo wakastahiki kuwashukia adhabu, wakawa ni wenye kujuta kwa kitendo chao hicho.
Kiungo 26:157
158
فَأَخَذَهُمُ ٱلْعَذَابُ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. [158]
Maelezo ya chini[158] Basi ikawateketeza adhabu aliyo waahidi Swaleh, wala majuto hayakuwakinga na adhabu ya ukosefu wao. Hakika katika kusimulia kisa chao pana dalili ya kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu kuwateketeza makafiri na kuwaokoa Waumini. Na si wengi katika watu wako wenye kuamini.
Kiungo 26:158
159
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [159]
Maelezo ya chini[159] Na hakika bila ya shaka aliye kuumba ndiye Yeye Muweza wa kuwateketeza wapinzani, na Mfadhili wa kuwaokoa wachamngu.
Kiungo 26:159
160
كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ ٱلْمُرْسَلِينَ
Watu wa Luut'i waliwakanusha Mitume. [160]
Maelezo ya chini[160] Alipo waita Luut'i watu wake wamuabudu Mwenyezi Mungu pekee, na waache ushirikina, waliwakanusha Mitume wote.
Kiungo 26:160
161
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao, Luut'i: Je! Hamumchimngu?. [161]
Maelezo ya chini[161] Ewe Mtume! Watajie watu wako pale Lut'i alipo waambia watu wake, naye ni ndugu yao na shemeji yao:
Kiungo 26:161
162
إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌۭ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu. [162]
Maelezo ya chini[162] Hakika mimi nimetumwa kwenu na Mwenyezi Mungu nikuleteeni Dini ya Haki. Nami ni muaminifu wa kuifikisha Dini hii.
Kiungo 26:162
163
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi. [163]
Maelezo ya chini[163] Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na ifuateni amri yangu kwa ninayo kuitieni.
Kiungo 26:163
164
وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [164]
Maelezo ya chini[164] Wala mimi sitaki kwenu ujira kwa uwongofu na uwongozi ninao kuitieni. Sina ujira ila kwa Mwenye kumiliki viumbe vyote na Mlezi wao.
Kiungo 26:164
165
أَتَأْتُونَ ٱلذُّكْرَانَ مِنَ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?. [165]
Maelezo ya chini[165] Lut'i alisema: Nyinyi mnastarehea kuwaingilia wanaume mkaacha wanawake? Kwa hayo anakusudia kuyakanya yale waliyo yazoea ya vitendo vichafu. "Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?" Yaani kazi ya liwat'i, ambayo tangu asli yake ni ukosefu muovu, unao chusha hata kuusikia, kinyume na maumbile, unao mteremsha mwanaadamu chini kabisa. Na lau kuwa unaenea basi huharibu sunna ya kuoa, nayo ni sunna ya maumbile, hata uzazi ukatike na ulimwengu usite kuendelea. Na kwa liwat'i huenea maradhi kama yanavyo enea kwa uzinzi kama tego, kisonono, donda ndugu, maradhi ya ngozi kama ukurutu, na hutokea ishara za kudhoofika nyama za nyuma hata ikawa mtu hawezi kujizuia kutokwa na choo ovyo. Na nyuma kwake mtu huchanua kukawa kama mdomo wa tarumbeta. Na huko nyuma hujaa vijidudu vya maradhi na hivyo humuambukiza mwenye kumuingilia na yeye hivyo vijidudu vikenda mletea maradhi mengine ya njia za mkojo. Na huenda huyo mwenye kufanywa mambo hayo akawa mpumbavu hafai kitu, ikiwa kaanza tangu utotoni. Na huenda akajidai kuonesha ujanadume mwingi kuliko kiasi kwa kutaka kuficha upungufu wake wa uume. (Karibuni imedhihiri kuwa maradhi ya khatari kabisa ya AIDS [Ukimwi] yameenea zaidi sana kwa watendao kitendo hichi na watumiao madawa ya ulevi, ijapo kuwa na wazinzi nao hupata!). Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameukemea ukosefu huu katika Aya kadhaa wa kadhaa, na akabainisha hikima ya Mwenye kuhukumu kwa kuharimisha huku, kwa kusema: " Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!"
Kiungo 26:165
166
وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُم مِّنْ أَزْوَٰجِكُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ عَادُونَ
Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!. [166]
Maelezo ya chini[166] Na mnaacha aliyo kuumbieni Mwenyezi Mungu ya kustarehe na wake zenu walio halali yenu? Ama hakika nyinyi ni watu mlio pindukia mipaka ya udhalimu katika kufanya maasi.
Kiungo 26:166
167
قَالُوا۟ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَـٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُخْرَجِينَ
Wakasema: Ewe Luut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!. [167]
Maelezo ya chini[167] Walikasirika kwa kule kuwakataza na kuwakemea kwa sababu ya jambo ovu na wakasema: Kama hukuacha kutukebehi tutakutoa mji kwa izara kubwa.
Kiungo 26:167
168
قَالَ إِنِّى لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلْقَالِينَ
Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu. [168]
Maelezo ya chini[168] Lut'i akasema: Hakika mimi nakichukia mno hichi kitendo chenu, wala sitoacha kabisa kukipinga na kukikebehi.
Kiungo 26:168
169
رَبِّ نَجِّنِى وَأَهْلِى مِمَّا يَعْمَلُونَ
Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo. [169]
Maelezo ya chini[169] Na akamwomba Mola wake Mlezi amwokoe yeye na ahali zake na wayatendayo wale wajinga, baada ya kwisha kata tamaa kuwa hawamsikilizi.
Kiungo 26:169
170
فَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ
Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,. [170]
Maelezo ya chini[170] Mwenyezi Mungu akamuitikia ombi lake, akamwokoa yeye na wale walio fuata wito wake, kwa kuwatoa wote majumbani mwao wakati wa kuteremka adhabu kuwashukia wenye kukanusha.
Kiungo 26:170
171
إِلَّا عَجُوزًۭا فِى ٱلْغَـٰبِرِينَ
Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma. [171]
Maelezo ya chini[171] Ila mkewe kizee aliye baki, na hakutoka nao. Yeye akaangamia kwa kufuru zake na ukhaini wake, kwa kuwaunga mkono wakosefu.
Kiungo 26:171
172
ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
Kisha tukawaangamiza wale wengine. [172]
Maelezo ya chini[172] Kisha Mwenyezi Mungu akawahiliki makafiri watendao uovu kwa hilaki kali na mbaya.
Kiungo 26:172
173
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًۭا ۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلْمُنذَرِينَ
Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa. [173]
Maelezo ya chini[173] Na Mwenyezi Mungu aliwateremshia wale watu wapotovu mawe kutoka mbinguni, yakawateketeza. Na ilikuwa mvua ya kutisha kwa wingi wake na namna yake. Basi mvua ovu ya walio kwisha onywa ni mvua hiyo, kwani iliteremka kwa uangamizi mkubwa mno!
Kiungo 26:173
174
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini. [174]
Maelezo ya chini[174] Hakika adhabu ile iliyo wateremkia watu wale hapana shaka ni hoja yenye kuonyesha utimilivu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Wala si wengi katika watu wako wenye kusadiki hayo.
Kiungo 26:174
175
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. [175]
Maelezo ya chini[175] Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kusifika kwa rehema iliyo kamilika. Huwapa adhabu watendao dhambi, na huwalipa wema Waumini.
Kiungo 26:175
176
كَذَّبَ أَصْحَـٰبُ لْـَٔيْكَةِ ٱلْمُرْسَلِينَ
Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume. [176]
Maelezo ya chini[176] Hichi kisa cha Shuaibu pamoja na Watu wa Al Aykat, Machakani, nao ni msitu wenye miti mizuri, karibu na Madian. Kikundi cha watu waliteremkia hapo na wakakaa. Mwenyezi Mungu akawapelekea Shuaibu kama alivyo wapelekea watu wa Madian. Wakamkadhibisha katika wito wake. Na kwa hivi wakawa wamekanusha risala za Mitume wote.
Kiungo 26:176
177
إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?. [177]
Maelezo ya chini[177] Ewe Muhammad! Watajie watu wako pale Shuaibu alipo waambia watu wa Machakani: Je! Hamumkhofu Mwenyezi Mungu mkamuamini? Wakaingia kumkadhibisha.
Kiungo 26:177
178
إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌۭ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. [178]
Maelezo ya chini[178] Hakika mimi nimetumwa na Mola Mlezi wa walimwengu wote nikuongoeni na nikuongozeni. Nami ni muaminifu wa kuufikisha ujumbe wake kwenu.
Kiungo 26:178
179
فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. [179]
Maelezo ya chini[179] Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na nit'iini kwa kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na kuziokoa nafsi zenu na madhambi.
Kiungo 26:179
180
وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [180]
Maelezo ya chini[180] Na mimi kwa hivi kukuongozeni na kukufunzeni sikutakini ujira wowote. Mimi sina malipo kaamili kwa sababu ya kazi yangu ila kutokana na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Kiungo 26:180
181
۞ أَوْفُوا۟ ٱلْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُخْسِرِينَ
Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja. [181]
Maelezo ya chini[181] Shuaibu akawaamrisha kutimiza vipimo kwa ukamilifu wanapo pima, kwani ilikuwa ada yao kupunguza kwa pishi na mizani, kupunguza haki za watu kwa kuwapunja na kuwapimia kasoro.
Kiungo 26:181
182
وَزِنُوا۟ بِٱلْقِسْطَاسِ ٱلْمُسْتَقِيمِ
Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;. [182]
Maelezo ya chini[182] Na wapimieni watu kwa mizani ya sawa sawa, ili wachukue haki yao kwa uadilifu ulio nyooka.
Kiungo 26:182
183
وَلَا تَبْخَسُوا۟ ٱلنَّاسَ أَشْيَآءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ
Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi. [183]
Maelezo ya chini[183] Wala msiwapunguzie watu haki zao, wala msipite katika nchi mkifisidi kwa kuuwa, na uharamia, na kufanya madhambi, na kufuata pumbao.
Kiungo 26:183
184
وَٱتَّقُوا۟ ٱلَّذِى خَلَقَكُمْ وَٱلْجِبِلَّةَ ٱلْأَوَّلِينَ
Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia. [184]
Maelezo ya chini[184] Na tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu aliye kuumbeni, na akaumba kaumu zenye nguvu na takaburi zilizo tangulia.
Kiungo 26:184
185
قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلْمُسَحَّرِينَ
Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa. [185]
Maelezo ya chini[185] Wakasema: Wewe si chochote ila ni mtu aliye sibiwa na uchawi mkali na ikapotea akili yake.
Kiungo 26:185
186
وَمَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌۭ مِّثْلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ
Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo. [186]
Maelezo ya chini[186] Na wewe si chochote ila ni mmoja wetu sawa na sisi kwa utu. Basi vipi ujipe ubora kuliko sisi kwa Utume? Nasi tunaamini kuwa wewe ni mwongo wa kubobea.
Kiungo 26:186
187
فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًۭا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. [187]
Maelezo ya chini[187] Basi hebu tuangushie vipande vya adhabu kutoka mbinguni ikiwa ni katika wasemao kweli kwa huu ujumbe wako! Na chini ya shauri hii kwa hakika pana kila namna ya ubishi.
Kiungo 26:187
188
قَالَ رَبِّىٓ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ
Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda. [188]
Maelezo ya chini[188] Shuaibu akasema: Mola wangu Mlezi ni Mjuzi, upeo wa kujua, wa maasi yote myatendayo, na adhabu mnayo stahiki. Yeye atakuteremshieni hayo kwa wakati wake alio ukadiria. Na huu ndio hadi ya mwisho wa kumwachilia Mwenyezi Mungu kila kitu, na kuwatisha hao makafiri.
Kiungo 26:188
189
فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمْ عَذَابُ يَوْمِ ٱلظُّلَّةِ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ
Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa. [189]
Maelezo ya chini[189] Lakini wao waliendelea kumkadhibisha. Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa adhabu ya joto kuu mno. Wakawa wanatapa tapa hawana pa kukimbilia. Walipo pata kiwingu cha kuwapa kivuli kukinga mwako wa jua walijikusanya chini yake. Mwenyezi Mungu akawateremshia moto, ukawateketeza wote katika siku ya kitisho kikubwa mno.
Kiungo 26:189
190
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. [190]
Maelezo ya chini[190] Hakika adhabu iliyo wateremkia watu wa Machakani kuwa ni malipo ya uasi wao, ni dalili ya ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na hawakuwa wengi wa watu wako wenye kusadiki.
Kiungo 26:190
191
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [191]
Maelezo ya chini[191] Na hakika Mola wako Mlezi hapana shaka ndiye Yeye aliye tengeka kwa Nguvu na Ushindi, Mwenye kuwaneemesha Waumini kwa rehema nyingi.
Kiungo 26:191
192
وَإِنَّهُۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [192]
Maelezo ya chini[192] Na hakika hii Qur'ani iliyo tajwa ndani yake visa vya kweli imeteremshwa kutoka kwa Mwenye kuumba walimwengu wote, Mwenye kumiliki mambo yao, na Mlezi wao. Basi khabari zake ni za kweli. Na hukumu yake inatimizwa mpaka Siku ya Kiyama.
Kiungo 26:192
193
نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلْأَمِينُ
Ameuteremsha Roho muaminifu,. [193]
Maelezo ya chini[193] Ameiteremsha Roho muaminifu, naye ni Jibril a.s.,
Kiungo 26:193
194
عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلْمُنذِرِينَ
Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,. [194]
Maelezo ya chini[194] Juu ya moyo wako ulio tulia kuihifadhi na kuifahamu, na idhibitike katika moyo wako iwe madhubuti isisahaulike, ili upate kuwaonya wakhalifu kwa adhabu ziliomo ndani yake.
Kiungo 26:194
195
بِلِسَانٍ عَرَبِىٍّۢ مُّبِينٍۢ
Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi. [195]
Maelezo ya chini[195] Jibril amekuteremshia kwa lugha ya Kiarabu, yenye maana wazi, yenye hoja zilizo dhaahiri kwa wanayo hitajia ya kutengeneza mambo yao ya dunia na Dini.
Kiungo 26:195
196
وَإِنَّهُۥ لَفِى زُبُرِ ٱلْأَوَّلِينَ
Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale. [196]
Maelezo ya chini[196] Na hakika kuitaja Qur'ani na kueleza kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu kumteremshia Muhammad s.a.w. yametajwa katika Vitabu vya Manabii walio tangulia.
Kiungo 26:196
197
أَوَلَمْ يَكُن لَّهُمْ ءَايَةً أَن يَعْلَمَهُۥ عُلَمَـٰٓؤُا۟ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?. [197]
Maelezo ya chini[197] Je! Hawa wenye inda wanaikataa Qur'ani na hali wao wanayo hoja inayo onyesha ukweli wa Muhammad s.a.w., nayo ni ilimu ya wanazuoni wa Wana wa Issraili juu ya Qur'ani kama ilivyo katika vitabu vyao?
Kiungo 26:197
198
وَلَوْ نَزَّلْنَـٰهُ عَلَىٰ بَعْضِ ٱلْأَعْجَمِينَ
Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,. [198]
Maelezo ya chini[198] Na lau tungeli mteremshia mtu asiye kuwa Mwaarabu, anaye weza kusema Kiarabu lakini si kwa ufasihi, wasingeli waza kumtuhumu kuwa kaizua.
Kiungo 26:198
199
فَقَرَأَهُۥ عَلَيْهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ مُؤْمِنِينَ
Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini. [199]
Maelezo ya chini[199] Na angeli wasomea baraabara kinyume na ada bado wangeli mkanusha, na wakapatia kisababu kwa ukafiri wao.
Kiungo 26:199
200
كَذَٰلِكَ سَلَكْنَـٰهُ فِى قُلُوبِ ٱلْمُجْرِمِينَ
Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu. [200]
Maelezo ya chini[200] Sisi tumekutia huko kukanusha katika nyoyo za wakosefu; na tumekuthibitisha kama tulivyo kuthibitisha katika nyoyo za wenye sifa kama zao.
Kiungo 26:200
201
لَا يُؤْمِنُونَ بِهِۦ حَتَّىٰ يَرَوُا۟ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ
Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu. [201]
Maelezo ya chini[201] Basi hapana njia ya wao kuacha tabia yao ya ukafiri mpaka wateseke kwa hiyo adhabu kali walio ahidiwa.
Kiungo 26:201
202
فَيَأْتِيَهُم بَغْتَةًۭ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari. [202]
Maelezo ya chini[202] Itawateremkia adhabu kwa ghafla bila ya kuitaraji, wala wao hawajui kama inakuja.
Kiungo 26:202
203
فَيَقُولُوا۟ هَلْ نَحْنُ مُنظَرُونَ
Na watasema: Je, tutapewa muhula?. [203]
Maelezo ya chini[203] Watasema itapo teremka hiyo adhabu: Je, tutapewa muhula? Haya ni kwa majuto kwa kupitiwa na Imani na kutaka waakhirishiwe adhabu. Lakini hawajibiwi.
Kiungo 26:203
204
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ
Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?. [204]
Maelezo ya chini[204] Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa Makka wameghurika na kuchelewesha kwangu kuwaadhibu, basi ndio wanaihimiza? Anakusudia Subhanahu Aliye takasika kuzisafihi akili zao kwa sababu ya kuhimiza kwao adhabu juu ya kuwaonya na kuwatisha.
Kiungo 26:204
205
أَفَرَءَيْتَ إِن مَّتَّعْنَـٰهُمْ سِنِينَ
Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka,. [205]
Maelezo ya chini[205] Je, umefikiri ukajua, kama Sisi tuliwastarehesha kwa uhai kwa muda wa miaka mingi pamoja na maisha mema?
Kiungo 26:205
206
ثُمَّ جَآءَهُم مَّا كَانُوا۟ يُوعَدُونَ
Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,. [206]
Maelezo ya chini[206] Kisha ikawateremkia adhabu iliyo ahidiwa.
Kiungo 26:206
207
مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يُمَتَّعُونَ
Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?. [207]
Maelezo ya chini[207] Kustarehe kwao kwa umri mrefu na maisha mema hakutowakinga hata chembe na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwani adhabu ya Mwenyezi Mungu itakuja tu, kama si leo kesho. Wala hapana kheri katika neema ambayo khatima yake ni adhabu.
Kiungo 26:207
208
وَمَآ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ
Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji. [208]
Maelezo ya chini[208] Na mwendo wetu kwa kaumu zote ni kuwa hatuuteketezi umma ila baada ya kuwatumia Mitume wa kuwaonya kwa kufuata hoja,
Kiungo 26:208
209
ذِكْرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ
Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu. [209]
Maelezo ya chini[209] Wakumbuke na wazingatie. Wala si shani yetu kudhulumu hata tuuadhibu umma kabla ya kuwaletea Mtume.
Kiungo 26:209
210
وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ ٱلشَّيَـٰطِينُ
Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo, [210]
Maelezo ya chini[210] Qur'ani inakataa waliyo yasema makafiri wa Makka ya kwamba Muhammad anafuata majini, nao ndio wanampa Qur'ani. Qur'ani inasema: Mashetani hawakuiteremsha hii Qur'ani.
Kiungo 26:210
211
وَمَا يَنۢبَغِى لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ
Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi. [211]
Maelezo ya chini[211] Wala haiwafalii wao kuiteremsha, na hawawezi kufanya hivyo.
Kiungo 26:211
212
إِنَّهُمْ عَنِ ٱلسَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ
Hakika hao wametengwa na kusikia. [212]
Maelezo ya chini[212] Kwani hao hakika wanazuiwa wasiisikie Qur'ani pale inapo funuliwa kwa Muhammad s.a.w.
Kiungo 26:212
213
فَلَا تَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَتَكُونَ مِنَ ٱلْمُعَذَّبِينَ
Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa. [213]
Maelezo ya chini[213] Basi wewe muelekee Mwenyezi Mungu ukiendelea na usafi wako wa ibada, wala usishughulike na fisadi za madai ya washirikina na mwendo wao muovu. Na hivi kutakiwa Mtume s.a.w. awe na ikhlasi ya namna hii ni wito kwa jamii ya watu waliomo katika umma wake.
Kiungo 26:213
214
وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ ٱلْأَقْرَبِينَ
Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. [214]
Maelezo ya chini[214] Watie khofu ya adhabu ya shirki na maasi walio karibu nawe katika jamaa zako.
Kiungo 26:214
215
وَٱخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini. [215]
Maelezo ya chini[215] Na kuwa mpole kwa wanao itikia wito wako wa Imani.
Kiungo 26:215
216
فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّى بَرِىٓءٌۭ مِّمَّا تَعْمَلُونَ
Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda. [216]
Maelezo ya chini[216] Pindi wakikuasi na wasikufuate basi jitenge nao, na jitenge na vitendo vyao vya ushirikina na maasi yote.
Kiungo 26:216
217
وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱلْعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ
Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [217]
Maelezo ya chini[217] Na tegemeza mambo yako kwa Mwenye nguvu, Mwenye uweza wa kuwatenda nguvu adui zako kwa utukufu wake, na kukunusuru wewe na kumnusuru kila mwenye kufanya a'mali yake kwa usafi wa niya.
Kiungo 26:217
218
ٱلَّذِى يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ
Ambaye anakuona unapo simama, [218]
Maelezo ya chini[218] Ambaye anakuona pale unapo simama kwa ibada za usiku na vitendo vyote vya kheri.
Kiungo 26:218
219
وَتَقَلُّبَكَ فِى ٱلسَّـٰجِدِينَ
Na mageuko yako kati ya wanao sujudu. [219]
Maelezo ya chini[219] Na anaona mwendo wako kati ya wanao sali, kwa kusimama, na kukaa, na kurukuu na kusujudu, pale unapo waongoza katika Swala.
Kiungo 26:219
220
إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ
Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. [220]
Maelezo ya chini[220] Hakika Yeye Subhanahu ndiye Mwenye kusikia dua zako na dhikri zako, ndiye Mjuzi wa kujua niya yako na vitendo vyako. Ni kama kwamba Subhanahu anamwambia: Usichukue taklifu kubwa bila ya kiasi katika mashaka ya ibada, kwani uyatendayo yote nayaona na nayasikia Mimi.
Kiungo 26:220
221
هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَـٰطِينُ
Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani? [221]
Maelezo ya chini[221] Washirikina walisema: Mashetani ndio wanamsomea Qur'ani Muhammad. Qur'ani ikawajibu: Nikupeni khabari watu gani Mashetani ndio wanawateremkia, na wakawashawishi?
Kiungo 26:221
222
تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍۢ
Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi. [222]
Maelezo ya chini[222] Wanamteremkia kila mwenye kubeba dhambi za namna mbaya kabisa za uwongo, na madhambi ya kuchusha kabisa. Nao ni hao makohani mafisadi ambao tabia zao na tabia za Mashetani ni jinsi moja na zimewafikiana.
Kiungo 26:222
223
يُلْقُونَ ٱلسَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَـٰذِبُونَ
Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo. [223]
Maelezo ya chini[223] Hao hutega masikio yao kwa Mashetani, na kwao wakapata mambo ya dhana dhana tu. Na wengi wao ni waongo, na huzidisha tena juu ya kauli walizo zipata kwa Mashetani.
Kiungo 26:223
224
وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلْغَاوُۥنَ
Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata. [224]
Maelezo ya chini[224] Makafiri wanasema: Hii Qur'ani ni mashairi, na Muhammad ni mtungaji mashairi. Mwenyezi Mungu ameyavunja haya kwa kuthibitisha kuwa hakika Qur'ani imejaa hikima na hukumu. Mpango wake unapingana na mpango wa mashairi ambao unategemea juu ya kweli na uwongo. Na amebainisha kwamba hali ya Muhammad s.a.w. inapingana na hali ya watungaji mashairi. Yeye anasema kwa hikima, wao wanasema kwa udanganyifu. Na hii ndiyo hali ya wengi katika watungaji mashairi.
Kiungo 26:224
225
أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِى كُلِّ وَادٍۢ يَهِيمُونَ
Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde? [225]
Maelezo ya chini[225] Kwani huwaoni vile wanavyo tangatanga katika mabonde ya maneno wala hawaongoki kwenye Haki?
Kiungo 26:225
226
وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ
Na kwamba wao husema wasiyo yatenda? [226]
Maelezo ya chini[226] Na kwamba wao husema kwa ndimi zao wasio yaambatisha na vitendo vyao?
Kiungo 26:226
227
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَذَكَرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًۭا وَٱنتَصَرُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا ظُلِمُوا۟ ۗ وَسَيَعْلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ أَىَّ مُنقَلَبٍۢ يَنقَلِبُونَ
Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka. [227]
Maelezo ya chini[227] Lakini walio hidika kwa hidaya ya Mwenyezi Mungu, na wakatenda mema mpaka zikatua katika nafsi zao sifa bora, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi mpaka ikathibiti khofu katika nyoyo zao, hawa basi huyafanya mashairi kama dawa ilio sibu kwa ugonjwa wake. Na hupambana kwa ajili ya kuiwania Dini yao na kusimamisha Haki, inapo kuwa Haki inafanyiwa jeuri. Na walio dhulumu nafsi zao kwa shirki na kumkejeli Mtume kwa mashairi, watatafuta wapi pa kuikimbia shari na hilaki wanayo iendea.
Kiungo 26:227

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure