Sura ya 37 kati ya 114 · Makkiya

Sura As-Saffat (Waliojipanga Safu)

سُورَةُ الصَّافَّاتِ
Aya 182

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلصَّـٰٓفَّـٰتِ صَفًّۭا
Naapa kwa wanao jipanga kwa safu. [1]
Maelezo ya chini[1] Naapa kwa mataifa katika viumbe vyangu, walio jipanga wenyewe kwa safu zilio sawa katika msimamo wa ibada na ut'iifu.
Kiungo 37:1
2
فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجْرًۭا
Na kwa wenye kukataza mabaya. [2]
Maelezo ya chini[2] Na kwa wanao zuia wanao pindukia mipaka kwa mzuio mkali, nidhamu ibakie, na ulimwengu uhifadhiwe.
Kiungo 37:2
3
فَٱلتَّـٰلِيَـٰتِ ذِكْرًا
Na kwa wenye kusoma Ukumbusho. [3]
Maelezo ya chini[3] Na kwa wenye kusoma Aya, na wanamdhukuru Mwenyezi Mungu kwa dhikri ya Tasbihi, Kumtakasa, na Kumhimidi, kumsifu.
Kiungo 37:3
4
إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَٰحِدٌۭ
Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja. [4]
Maelezo ya chini[4] Hakika Mungu wenu anaye faa kuabudiwa bila ya shaka ni Mmoja tu. Hana mshirika wake, kwa dhati, wala kitendo, wala sifa.
Kiungo 37:4
5
رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ ٱلْمَشَـٰرِقِ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote. [5]
Maelezo ya chini[5] Yeye - peke yake - ndiye Muumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao, na ndiye Mwenye kupanga mambo, na ndiye Mwenye kutawala mashariki za kila chenye mashariki. Mwenyezi Mungu ndiye Muumba mbingu saba na viliomo baina yao, navyo ni hivyo vyombo vya mbinguni na nyota zake. Naye ndiye Mwenye kusimamisha, Mwenye kulinda vile vile juu ya mwahali zinapo chomozea jua na nyota zote. Na Yeye ndiye anaye vionyesha hivyo kila siku katika pahala huko upeo wa macho, kila siku pahala mbali na vilipo dhihiri siku iliyo tangulia. Na hayo ni kwa mwendo wa mpango wa jua maalumu kwa inavyo zunguka dunia juu ya msumari-kati wake kutoka magharibi kwendea mashariki kila siku na wakati huo huo inavyo lizunguka jua katika njia yake katika falaki. Na jua na nyota huonekana na wakaazi wa ardhi kila siku kama zinachomoza mwahala mbali mbali. Na kila ardhi ikigeuza mahala pake katika safari yake katika mbingu linaonekana jua linachomoza pahala pengine. Ukiliangalia jua kwa utulivu kuanzia mwishoni wa mwezi wa Machi, yaani linapo kuwa jua lipo kati ya mstari wa Ikweta mwanzo wa musimu wa Rabii, yaani Spring, kwa nusu ya kaskazini ya dunia, utaliona linachomoza pahala katika mashariki juu ya upeo wa macho. Kwa mwenye kupeleleza kila siku ikipita ataona kuchomoza kwake kunajongelea kaskazini. Na mwishoni mwa mwezi wa Juni utaona linachomozea mwisho wa kukaribia kaskazini. Kisha baada ya hapo utaliona jua linarejea linafuata kugeuka kule kule mpaka mwisho wa Septemba (wakati wa kuwa sawa wakati wa Khariif yaani Autumn) utaliona jua linachomoza pale pale lilipo chomoza mwanzo wa Machi. Kisha litaendelea kuelekea kusini kuchomoza kwake mpaka mwisho wa Desemba linakuwa linachomoza karibu kabisa na kusini. Baada ya hapo huanza tena kurejea kuelekea kaskazini mpaka limalize safari yake ya kufika kati sawa katika Rabii ya pili. Na safari hii yote inachukua siku 365 na robo siku. Na inaonekana kuwa nyota nazo zinachomoza mwahala mbali mbali katika upeo wa macho inapo kuwa dunia imo katika safari yake ya mbinguni, na khasa nyota za buruji (au vituo) 12 vinavyo pitiwa na jua katika mwendo wake wa mwaka.
Kiungo 37:5
6
إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِزِينَةٍ ٱلْكَوَاكِبِ
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. [6]
Maelezo ya chini[6] Sisi tumeipamba hii mbingu ya karibu na watu wa duniani kwa mapambo, nayo ni hizo nyota zinazong'ara, zenye ukubwa mbali mbali, na mwahala pao mbali mbali kwenye anga la ulimwengu kama ionekanavyo kwa macho.
Kiungo 37:6
7
وَحِفْظًۭا مِّن كُلِّ شَيْطَـٰنٍۢ مَّارِدٍۢ
Na kulinda na kila shet'ani a'si. [7]
Maelezo ya chini[7] Na tukaihifadhi hiyo mbingu na kila shetani jabari aliye a'si.
Kiungo 37:7
8
لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍۢ
Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande. [8]
Maelezo ya chini[8] Hao majabari wa kishetani hawawezi kusikiliza yanayo pita katika ulimwengu wa Malaika. Na wao hupopolewa kwa kila kinacho faa cha kuwazuia.
Kiungo 37:8
9
دُحُورًۭا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌۭ وَاصِبٌ
Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu. [9]
Maelezo ya chini[9] Hufukuzwa hao kwa nguvu wasifikilie kuweza kusikiliza khabari za mbinguni. Na Akhera watapata adhabu kali ya kudumu.
Kiungo 37:9
10
إِلَّا مَنْ خَطِفَ ٱلْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُۥ شِهَابٌۭ ثَاقِبٌۭ
Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara. [10]
Maelezo ya chini[10] Isipo kuwa anaye lipata neno moja hivi katika khabari za mbinguni kwa kuibia. Na huyo naye tunamwandama kwa mwenge wa moto unao murika anga kwa mwangaza wake, ukamuunguzilia mbali.
Kiungo 37:10
11
فَٱسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَآ ۚ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّن طِينٍۢ لَّازِبٍۭ
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata. [11]
Maelezo ya chini[11] Ewe Nabii! Hebu waulize hao wanao kanya kufufuliwa wanao ona hayawi hayo: Je! Kwani kuwaumba wao hawa ni kugumu zaidi au kuziumba mbingu, na ardhi, na nyota, na vyenginevyo, tulivyo viumba Sisi?
Kiungo 37:11
12
بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ
Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara. [12]
Maelezo ya chini[12] Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na udongo unao gandana. Basi kwa nini wanaona ajabu kurejezwa tena wao?
Kiungo 37:12
13
وَإِذَا ذُكِّرُوا۟ لَا يَذْكُرُونَ
Na wanapo kumbushwa hawakumbuki. [13]
Maelezo ya chini[13] Na wanapo kabiliwa kwa dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu kufufua, hata hawazishughulikii wakanufaika kwa hizo dalili.
Kiungo 37:13
14
وَإِذَا رَأَوْا۟ ءَايَةًۭ يَسْتَسْخِرُونَ
Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara. [14]
Maelezo ya chini[14] Na wanapo ona ushahidi wa kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu huitana wapate kupita mipaka katika kumkejeli.
Kiungo 37:14
15
وَقَالُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌۭ مُّبِينٌ
Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri. [15]
Maelezo ya chini[15] Na makafiri husema juu ya Ishara zinazo onyesha uweza wa Mwenyezi Mungu: Haya tunayo yaona si chochote ila ni uchawi tu.
Kiungo 37:15
16
أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًۭا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa? [16]
Maelezo ya chini[16] Hivyo sisi tukisha kufa tukawa udongo na mafupa tutatolewa tena makaburini kwetu tuwe wahai?
Kiungo 37:16
17
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ
Hata baba zetu wa zamani? [17]
Maelezo ya chini[17] Sisi tuwe wahai, na pia watafufuliwa baba zetu wa zamani walio kufa kabla yetu, na wakapotea, na wakateketea?
Kiungo 37:17
18
قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَٰخِرُونَ
Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili. [18]
Maelezo ya chini[18] Ewe Nabii! Waambie: Ndio mtafufuliwa nyote, nanyi ni madhalili na wanyonge.
Kiungo 37:18
19
فَإِنَّمَا هِىَ زَجْرَةٌۭ وَٰحِدَةٌۭ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ
Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona! [19]
Maelezo ya chini[19] Kwani hakika kufufuliwa ni Ukelele mmoja tu, mara wote watakuwa wahai wakiyaona waliyo ahidiwa.
Kiungo 37:19
20
وَقَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ ٱلدِّينِ
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo. [20]
Maelezo ya chini[20] Na washirikina watasema: Ee msiba wetu huu! Hii ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo kwa a'mali zilio tendwa!
Kiungo 37:20
21
هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha. [21]
Maelezo ya chini[21] Watajibiwa: Hii ndiyo Siku ya Hukumu na kufarikisha vitendo, mliyo kuwa mkiikadhibisha.
Kiungo 37:21
22
۞ ٱحْشُرُوا۟ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ وَأَزْوَٰجَهُمْ وَمَا كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ
Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu. [22]
Maelezo ya chini[22] Enyi Malaika wangu! Wakusanyeni walio jidhulumu nafsi zao kwa kufuru, pamoja na wake zao wa kikafiri, na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, yakiwa masanamu au watu, na waonyesheni njia ya kwendea Motoni waingie humo.
Kiungo 37:22
23
مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْجَحِيمِ
Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu! [23]
Maelezo ya chini[23] Enyi Malaika wangu! Wakusanyeni walio jidhulumu nafsi zao kwa kufuru, pamoja na wake zao wa kikafiri, na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, yakiwa masanamu au watu, na waonyesheni njia ya kwendea Motoni waingie humo.
Kiungo 37:23
24
وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْـُٔولُونَ
Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa: [24]
Maelezo ya chini[24] Na wazuieni hapo hapo; kwani wao hakika watahojiwa juu ya imani zao na vitendo vyao.
Kiungo 37:24
25
مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ
Mna nini? Mbona hamsaidiani? [25]
Maelezo ya chini[25] Enyi washirikina! Mna nini? Mbona hamsaidiani kama mlivyo kuwa mkisaidiana nyinyi kwa nyinyi duniani?
Kiungo 37:25
26
بَلْ هُمُ ٱلْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ
Bali hii leo, watasalimu amri. [26]
Maelezo ya chini[26] Leo hii hawasaidiani, bali leo wanaongozwa tu, wamekwisha salimu amri.
Kiungo 37:26
27
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍۢ يَتَسَآءَلُونَ
Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. [27]
Maelezo ya chini[27] Watakuwa wakikabiliana kulaumiana na kusutana, na wakiulizana khabari za mwisho wao muovu.
Kiungo 37:27
28
قَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ ٱلْيَمِينِ
Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. [28]
Maelezo ya chini[28] Wanyonge watawaambia walio jipa ukubwa: Nyinyi mlikuwa mkitujia upande tulio udhania ni wa kheri na mafanikio, ili mtugeuze njia tuache Haki twende kwenye upotovu.
Kiungo 37:28
29
قَالُوا۟ بَل لَّمْ تَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ
Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. [29]
Maelezo ya chini[29] Watasema walio jipa ukubwa: Sisi hatukukugeuzeni njia, lakini nyinyi wenyewe mliikataa Imani, na mkaipuuza kwa khiari yenu.
Kiungo 37:29
30
وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَـٰنٍۭ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًۭا طَـٰغِينَ
Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. [30]
Maelezo ya chini[30] Na sisi hatukuwa na madaraka juu yenu hata tuweze kukunyang'anyeni uweza wenu wa kukhiari. Bali nyinyi wenyewe mlikuwa watu mlio iacha Haki.
Kiungo 37:30
31
فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَآ ۖ إِنَّا لَذَآئِقُونَ
Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu. [31]
Maelezo ya chini[31] Basi neno la Mola wetu Mlezi limethibiti juu yetu. Hakika hapana shaka sisi tutaionja adhabu ya Siku ya Kiyama.
Kiungo 37:31
32
فَأَغْوَيْنَـٰكُمْ إِنَّا كُنَّا غَـٰوِينَ
Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. [32]
Maelezo ya chini[32] Tukakuiteni kwenye maasi na upotovu na nyinyi mkaitikia wito wetu. Kazi yetu ni kufanya hila ya kuwaita watu wafuate upotovu tulio nao. Basi hatuna lawama.
Kiungo 37:32
33
فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍۢ فِى ٱلْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ
Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja. [33]
Maelezo ya chini[33] Kwani hakika wafuasi na wenye kufuatwa wote watashiriki pamoja katika adhabu ya Siku ya Kiyama.
Kiungo 37:33
34
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ
Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu. [34]
Maelezo ya chini[34] Hakika mfano wa adhabu hiyo Sisi tunawapa wale walio fanya makosa katika Haki ya Mwenyezi Mungu kwa ushirikina na kutenda maasi.
Kiungo 37:34
35
إِنَّهُمْ كَانُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ
Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna. [35]
Maelezo ya chini[35] Hakika watu hao walikuwa wakiambiwa: La ilaha illa 'Llah, Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakakataa kukiri kwa kiburi na majivuno.
Kiungo 37:35
36
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓا۟ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٍۢ مَّجْنُونٍۭ
Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu? [36]
Maelezo ya chini[36] Na husema: Sisi tuache kuabudu miungu yetu kwa kufuata kauli ya mtunga mashairi aliye zugwa asiye kuwa na akili?
Kiungo 37:36
37
بَلْ جَآءَ بِٱلْحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلْمُرْسَلِينَ
Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume. [37]
Maelezo ya chini[37] Bali Mtume wao amewaletea Tawhidi, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja, ambayo ndiyo wito wa Mitume wote, naye akasadikisha kwa hivyo wito wa hao Mitume.
Kiungo 37:37
38
إِنَّكُمْ لَذَآئِقُوا۟ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَلِيمِ
Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu. [38]
Maelezo ya chini[38] Enyi washirikina! Hakika nyinyi hapana shaka mtaionja adhabu kali ya Akhera.
Kiungo 37:38
39
وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya. [39]
Maelezo ya chini[39] Na hamtapata malipo Akhera ila malipo ya vitendo vyenu vya duniani.
Kiungo 37:39
40
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa. [40]
Maelezo ya chini[40] Ila waja wangu walio safika; hao hawataionja adhabu kwa sababu wao ni watu wa Imani na ut'iifu.
Kiungo 37:40
41
أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ رِزْقٌۭ مَّعْلُومٌۭ
Hao ndio watakao pata riziki maalumu, [41]
Maelezo ya chini[41] Hawa watu wa ikhlasi watapata Akhera riziki maalumu kwa Mwenyezi Mungu.
Kiungo 37:41
42
فَوَٰكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ
Matunda, nao watahishimiwa. [42]
Maelezo ya chini[42] Matunda ya namna mbali mbali. Nao watastareheshwa na kutukuzwa,
Kiungo 37:42
43
فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Katika Bustani za neema. [43]
Maelezo ya chini[43] Katika Bustani zenye neema.
Kiungo 37:43
44
عَلَىٰ سُرُرٍۢ مُّتَقَـٰبِلِينَ
Wako juu ya viti wamekabiliana. [44]
Maelezo ya chini[44] Wakikaa humo juu ya viti wakikabiliana.
Kiungo 37:44
45
يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍۢ مِّن مَّعِينٍۭ
Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem. [45]
Maelezo ya chini[45] Watawazungukia watoto na chombo chenye kinywaji kilicho toka kwenye chemchem zisio katika.
Kiungo 37:45
46
بَيْضَآءَ لَذَّةٍۢ لِّلشَّـٰرِبِينَ
Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao. [46]
Maelezo ya chini[46] Kinywaji chenyewe ni cheupe kinapo changanywa, na kitamu kwa wenye kukinywa.
Kiungo 37:46
47
لَا فِيهَا غَوْلٌۭ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ
Hakina madhara, wala hakiwaleweshi. [47]
Maelezo ya chini[47] Hakiwaumizi kichwa na kuwaletea ghururi, wala kwa kukinywa hicho haiwapotei akili yao kidogo kidogo, yaani hakileweshi.
Kiungo 37:47
48
وَعِندَهُمْ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ عِينٌۭ
Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri. [48]
Maelezo ya chini[48] Na watu hawa wat'iifu walioko Peponi watakuwa nao mahuruleini walio safi, wema, macho yao hayawatazami ila waume zao tu, basi hawayatafuti matamanio maovu, jicho la mwema haliangalii ila mema.
Kiungo 37:48
49
كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌۭ مَّكْنُونٌۭ
Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika. [49]
Maelezo ya chini[49] Hao wanawake wenye macho ya staha ni kama mayai ya mbuni, yaliyo hifadhiwa na mbawa zake. Basi hayaguswi na mikono, wala hayapati vumbi.
Kiungo 37:49
50
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍۢ يَتَسَآءَلُونَ
Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe. [50]
Maelezo ya chini[50] Hao watu wema watakuwa wakiingia kuulizana hali, na walikuwaje duniani?
Kiungo 37:50
51
قَالَ قَآئِلٌۭ مِّنْهُمْ إِنِّى كَانَ لِى قَرِينٌۭ
Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki. [51]
Maelezo ya chini[51] Hapo mmoja wao atasema: Mimi nalikuwa na rafiki katika washirikina, akijadiliana nami katika mambo ya Dini na yaliyo kuja katika Qur'ani.
Kiungo 37:51
52
يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُصَدِّقِينَ
Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki. [52]
Maelezo ya chini[52] Akisema: Ati wewe ni katika hao wanao sadiki kuwa kupo kufufuliwa na kuhisabiwa na kulipwa baada ya kufa?
Kiungo 37:52
53
أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًۭا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ
Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa? [53]
Maelezo ya chini[53] Ati baada ya kwisha teketea, tukawa udongo na mafupa, tutakuja kuwa hai mara nyengine, tuhisabiwe na tulipwe kwa vitendo tulivyo kwisha vitenda?
Kiungo 37:53
54
قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ
Atasema: Je! Nyie mnawaona? [54]
Maelezo ya chini[54] Muumini awaambie wenzie alio kaa nao: Enyi watu wa Peponi, mnawaona watu wa Motoni nipate kumwona rafiki yangu?
Kiungo 37:54
55
فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِى سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ
Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu. [55]
Maelezo ya chini[55] Jicho lake lipige duru kuelekea Motoni, na huko amwone sahibu yake wa zamani yuko katikati akiadhibika kwa Moto.
Kiungo 37:55
56
قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ
Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza. [56]
Maelezo ya chini[56] Akimwona aseme: Wallahi! Ulikaribia kule duniani kunihilikisha lau ningeli kufuata katika ukafiri wako na maasiya yako!
Kiungo 37:56
57
وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّى لَكُنتُ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ
Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa. [57]
Maelezo ya chini[57] Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi kwa hidaya yake na kuniwezesha kwake nikamuamini Mwenyezi Mungu na kufufuka, basi ningeli kuwa mfano wako wewe katika walio hudhurishwa katika hiyo adhabu.
Kiungo 37:57
58
أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ
Je! Sisi hatutakufa, [58]
Maelezo ya chini[58] Je! Sisi tutakaa milele tukineemeka katika Pepo, wala hatufi kabisa isipo kuwa kule kufa kwetu mara ya kwanza duniani, na wala hatuadhibiwi baada ya kwisha ingia Peponi?
Kiungo 37:58
59
إِلَّا مَوْتَتَنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ
Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa. [59]
Maelezo ya chini[59] Je! Sisi tutakaa milele tukineemeka katika Pepo, wala hatufi kabisa isipo kuwa kule kufa kwetu mara ya kwanza duniani, na wala hatuadhibiwi baada ya kwisha ingia Peponi?
Kiungo 37:59
60
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ
Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa. [60]
Maelezo ya chini[60] Hakika haya aliyo tupa Mwenyezi Mungu katika ukarimu wa Peponi bila ya shaka ndiyo kufuzu kukubwa, na kuvuka kukuu na hiyo adhabu tuliyo kuwa tunatahadhari nayo tangu duniani.
Kiungo 37:60
61
لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ ٱلْعَـٰمِلُونَ
Kwa mfano wa haya nawatende watendao. [61]
Maelezo ya chini[61] Ili wapate ukarimu wa Akhera kama walio bahatika kuupata Waumini, basi nawafanye kazi duniani hao wafanyao kazi, ili wapate kama walio pata wao.
Kiungo 37:61
62
أَذَٰلِكَ خَيْرٌۭ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ
Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? [62]
Maelezo ya chini[62] Je! Hiyo riziki maalumu iliyo andaliwa kwa sababu ya watu wa Peponi ni bora, au mti wa Zaqqum ulio andaliwa kwa ajili ya watu wa Motoni?
Kiungo 37:62
63
إِنَّا جَعَلْنَـٰهَا فِتْنَةًۭ لِّلظَّـٰلِمِينَ
Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. [63]
Maelezo ya chini[63] Hakika Sisi tumeujaalia mti huu uwe ni mtihani na adhabu ya Akhera kwa ajili ya washirikina.
Kiungo 37:63
64
إِنَّهَا شَجَرَةٌۭ تَخْرُجُ فِىٓ أَصْلِ ٱلْجَحِيمِ
Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu. [64]
Maelezo ya chini[64] Hakika huo ni mti ulioko katikati ya Jahannamu, umekulia huko Motoni, na umeumbwa kutokana na huko huko.
Kiungo 37:64
65
طَلْعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَـٰطِينِ
Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. [65]
Maelezo ya chini[65] Matunda yake mabaya kuyatazama, yana sura ya kukirihisha, macho hayapendi kuyatazama, kama vichwa vya mashetani ambavyo kwa hakika watu hawajaviona, lakini mtu humpitikia tu katika dhana jinsi ya ubaya wake.
Kiungo 37:65
66
فَإِنَّهُمْ لَـَٔاكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ
Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo. [66]
Maelezo ya chini[66] Na wao watakuwa wanakula matunda ya mti huo, na wajaze matumbo yao kwayo. Kwani hawanacho kinginecho cha kukila.
Kiungo 37:66
67
ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًۭا مِّنْ حَمِيمٍۢ
Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka. [67]
Maelezo ya chini[67] Kisha washirikina hao juu ya kula mti wa Zaqqum watapewa maji yaliyo changanywa, yamoto, ya kuwababua nyuso zao, na kukatakata matumbo yao.
Kiungo 37:67
68
ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى ٱلْجَحِيمِ
Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. [68]
Maelezo ya chini[68] Tena mwisho wao ni Motoni. Wao watakuwa katika adhabu ya milele. Wataletwa kutoka Motoni waje kula mti wa Zaqqum kisha wanyweshe kinywaji hicho, na tena warejeshwe mahala pao katika Jahannamu.
Kiungo 37:68
69
إِنَّهُمْ أَلْفَوْا۟ ءَابَآءَهُمْ ضَآلِّينَ
Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. [69]
Maelezo ya chini[69] Wao waliwakuta baba zao wamepotoka, na wao wakafanya haraka kufuata zile zile nyayo za baba zao. Wakawa mbioni kwendea njia yao, wakifuata tu wala hawachungui, kama walio timuliwa na wakihimizwa wende mbio mbio kuwafuata hao baba zao bila ya kupima wala kuzingatia.
Kiungo 37:69
70
فَهُمْ عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِمْ يُهْرَعُونَ
Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. [70]
Maelezo ya chini[70] Wao waliwakuta baba zao wamepotoka, na wao wakafanya haraka kufuata zile zile nyayo za baba zao. Wakawa mbioni kwendea njia yao, wakifuata tu wala hawachungui, kama walio timuliwa na wakihimizwa wende mbio mbio kuwafuata hao baba zao bila ya kupima wala kuzingatia.
Kiungo 37:70
71
وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. [71]
Maelezo ya chini[71] Na hakika walipotea njia ya sawa na njia ya Imani wengi katika mataifa yaliyo kwisha tangulia kabla ya hawa washirikina wa Makka.
Kiungo 37:71
72
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ
Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. [72]
Maelezo ya chini[72] Na bila ya shaka Sisi tuliyatumia Mitume hayo mataifa yaliyo tangulia ili wawaonye na wawahadharishe na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nao wakawakadhibisha.
Kiungo 37:72
73
فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ
Basi hebu angalia ulikuje mwisho wa walioonywa. [73]
Maelezo ya chini[73] Basi angalia, ewe uliye jaaliwa kuangalia, ulikuwaje mwisho wa walio onywa na Mitume? Bila ya shaka waliteketezwa, wakawa ni mazingatio kwa watu.
Kiungo 37:73
74
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliokhitariwa. [74]
Maelezo ya chini[74] Lakini walikuwapo Waumini ambao aliwakhitari Mwenyezi Mungu wamuabudu Yeye, ili wapate fadhila za ukarimu wake. Basi hao walizipata thawabu zake, na wakaepukana na adhabu yake.
Kiungo 37:74
75
وَلَقَدْ نَادَىٰنَا نُوحٌۭ فَلَنِعْمَ ٱلْمُجِيبُونَ
Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji. [75]
Maelezo ya chini[75] Na hakika Nuhu alitwita alipo kwisha kata tamaa na watu wake, basi na Sisi tukawa ni wabora wa kuitikia wito wake, tulipo muitikia ombi lake, na tukawaangamiza watu wake kwa tofani.
Kiungo 37:75
76
وَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ
Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa. [76]
Maelezo ya chini[76] Na tukamwokoa Nuhu na walio amini pamoja naye, wasizame na kuteketea kwa tofani.
Kiungo 37:76
77
وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلْبَاقِينَ
Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia. [77]
Maelezo ya chini[77] Tukawajaalia vizazi vya Nuhu ndio walio bakia katika ardhi baada ya kuteketea watu wake.
Kiungo 37:77
78
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye. [78]
Maelezo ya chini[78] Na tukamwachilia Nuhu kutajwa kwa wema na watu walio kuja baada yake wakimdhukuru mpaka Siku ya Kiyama.
Kiungo 37:78
79
سَلَـٰمٌ عَلَىٰ نُوحٍۢ فِى ٱلْعَـٰلَمِينَ
Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote! [79]
Maelezo ya chini[79] Maamkio ya Salama na Amani kumuamkia Nuhu kutokana na Malaika, na watu, na majini.
Kiungo 37:79
80
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. [80]
Maelezo ya chini[80] Hakika Sisi huwalipa walio tenda mema mfano wa haya. Basi aliingia katika Jihadi kulinyanyua Neno letu, na akavumilia maudhi kwa ajili yetu.
Kiungo 37:80
81
إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. [81]
Maelezo ya chini[81] Hakika yeye ni miongoni mwa waja wetu walio tuamini, na wakatimiza ahadi yetu, na wakaufikisha Ujumbe wetu.
Kiungo 37:81
82
ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
Kisha tukawazamisha wale wengine. [82]
Maelezo ya chini[82] Kisha tukawazamisha wenginewe katika makafiri wa kaumu yake.
Kiungo 37:82
83
۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبْرَٰهِيمَ
Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake, [83]
Maelezo ya chini[83] Na hakika bila ya shaka Ibrahim alikuwa akifuata ile ile njia yake na mwenendo wake katika kuitia Tawhidi, Imani
Kiungo 37:83
84
إِذْ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلْبٍۢ سَلِيمٍ
Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima. [84]
Maelezo ya chini[84] Alipo mkabili Mola wake Mlezi kwa moyo ulio kuwa nadhifu hauna ushirikina, umemsafia ibada Yeye tu.
Kiungo 37:84
85
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَاذَا تَعْبُدُونَ
Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? [85]
Maelezo ya chini[85] Alipo chukia kuwa baba yake na watu wake wanaabudu masanamu, akawaambia: Ni nini haya masanamu mnayo yaabudu?
Kiungo 37:85
86
أَئِفْكًا ءَالِهَةًۭ دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ
Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu? [86]
Maelezo ya chini[86] Si mnazua uwongo tu ulio wazi kwa haya myatendayo, kwa kuwa mnamuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Na si mnataka kuzua uzushi huu bila ya udhuru wowote ila kupenda kwenu tu?
Kiungo 37:86
87
فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote? [87]
Maelezo ya chini[87] Mnamdhania nini huyo ambaye ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa kwa kuwa Yeye ndiye Muumba walimwengu wote, mtapo kutana naye na hali nyinyi mmemfanyia washirika wenginewe katika ibada?
Kiungo 37:87
88
فَنَظَرَ نَظْرَةًۭ فِى ٱلنُّجُومِ
Kisha akapiga jicho kutazama nyota. [88]
Maelezo ya chini[88] Basi akazitupia jicho nyota kuzitazama ili apate kuona dalili ya Muumba ulimwengu. Akaziona zinageuka, zinabadilika
Kiungo 37:88
89
فَقَالَ إِنِّى سَقِيمٌۭ
Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa! [89]
Maelezo ya chini[89] Akajikhofia nafsi yake asiwe ana upotovu na maradhi ya itikadi.
Kiungo 37:89
90
فَتَوَلَّوْا۟ عَنْهُ مُدْبِرِينَ
Nao wakamwacha, wakampa kisogo. [90]
Maelezo ya chini[90] Watu wake wakamwachilia mbali, na wakapuuza maneno yake.
Kiungo 37:90
91
فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli? [91]
Maelezo ya chini[91] Akayaendea kwa haraka yale masanamu kwa kificho, na akayapa chakula ambacho wale washirikina walikiweka mbele yao ili nao wapate baraka yao kwa mujibu wa madai yao. Akasema kwa maskhara na kejeli: Mbona hamli?
Kiungo 37:91
92
مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ
Mna nini hata hamsemi? [92]
Maelezo ya chini[92] Mna nini hata mmeshindwa kusema lolote, hata ndio au sio?
Kiungo 37:92
93
فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًۢا بِٱلْيَمِينِ
Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia. [93]
Maelezo ya chini[93] Akayaingilia yale masanamu kuyapiga kwa mkono wa kulia, kwa kuwa ndio wenye nguvu, akayabomoa.
Kiungo 37:93
94
فَأَقْبَلُوٓا۟ إِلَيْهِ يَزِفُّونَ
Basi wakamjia upesi upesi. [94]
Maelezo ya chini[94] Walipo baini kwamba kuvunjwa miungu yao ni kwa kitendo cha Ibrahim, basi walimkimbilia ili wamtese kwa alivyo watendea miungu yao.
Kiungo 37:94
95
قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ
Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe [95]
Maelezo ya chini[95] Ibrahim akawaambia kwa kuwahizi: Hivyo nyinyi mnaabudu mawe mliyo yachonga nyinyi wenyewe kwa mikono yenu? Akili zenu zimekwenda wapi?
Kiungo 37:95
96
وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ
Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya! [96]
Maelezo ya chini[96] Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, na akayaumba hata hayo masanamu mnayo yaunda kwa mikono yenu. Basi Yeye peke yake ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa.
Kiungo 37:96
97
قَالُوا۟ ٱبْنُوا۟ لَهُۥ بُنْيَـٰنًۭا فَأَلْقُوهُ فِى ٱلْجَحِيمِ
Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo! [97]
Maelezo ya chini[97] Hoja ilipo wapata wale wanao abudu masanamu, wakaona hawana ila waingie kutumia nguvu; wakaazimia kumchoma moto. Basi waliambizana: Mjengeeni jengo, na mlijaze moto, na mtupeni katikati yake!
Kiungo 37:97
98
فَأَرَادُوا۟ بِهِۦ كَيْدًۭا فَجَعَلْنَـٰهُمُ ٱلْأَسْفَلِينَ
Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini. [98]
Maelezo ya chini[98] Kwa haya walikusudia kumteketeza, lakini Mwenyezi Mungu alimwokoa na ule moto baada ya wao kwisha mtumbukiza humo. Hadhi yake ikawa juu kwa utukufu ule, na Mwenyezi Mungu akawafanya wao ndio watu wa chini.
Kiungo 37:98
99
وَقَالَ إِنِّى ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّى سَيَهْدِينِ
Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa. [99]
Maelezo ya chini[99] Ibrahim alipo kata tamaa nao, kuwa hawaamini tena, alisema: Mimi ninahama kwendea pahala alipo niamrisha Mola wangu Mlezi nende. Mola wangu Mlezi atanihidi aniongoze mpaka nifike pahala pa utulivu, penye amani, na nchi nzuri.
Kiungo 37:99
100
رَبِّ هَبْ لِى مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema. [100]
Maelezo ya chini[100] Ewe Mola wangu Mlezi! Nipe dhuriya walio wema wa vitendo, wasimamie hii kazi ya wito kuwaitia watu kwako Wewe, baada yangu.
Kiungo 37:100
101
فَبَشَّرْنَـٰهُ بِغُلَـٰمٍ حَلِيمٍۢ
Basi tukambashiria mwana aliye mpole. [101]
Maelezo ya chini[101] Malaika wakampa bishara ya kwamba atapata mwana atakaye pambwa kwa akili na upole.
Kiungo 37:101
102
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَـٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَـٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri. [102]
Maelezo ya chini[102] Akazaliwa huyo mwana, na alipo kuwa kijana wa kwenda naye baba yake katika kutafuta haja za maisha, Ibrahim alipewa mtihani kwa ndoto aliyo iota. Ibrahim akasema: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini ufunuo kutokana na Mwenyezi Mungu ananitaka nikuchinje! Basi wewe tazama unaonaje? Yule mwana mwema alisema: Ewe baba yangu! Tekeleza amri ya Mola wako Mlezi. Utaniona mimi katika wanao subiri, Inshallah!
Kiungo 37:102
103
فَلَمَّآ أَسْلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلْجَبِينِ
Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji. [103]
Maelezo ya chini[103] Yule baba na mwanawe walipo iridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu, na akamweka juu ya fungu la mchanga na akamlaza juu yake, kipaji chake kikawa juu ya ardhi, akawa tayari kumchinja.
Kiungo 37:103
104
وَنَـٰدَيْنَـٰهُ أَن يَـٰٓإِبْرَٰهِيمُ
Tulimwita: Ewe Ibrahim!. [104]
Maelezo ya chini[104] Na Mwenyezi Mungu akajua umadhubuti wa Ibrahim na mwanawe katika majaribio, Mwenyezi Mungu alimwita Ibrahim kwa wito wa kirafiki: Ewe Ibrahim! Hakika umeuitikia kwa utulivu huo ufunuo wa ndoto, na wala hukusitasita katika kufuata amri. Basi haya yanakutosha. Sisi tunakupunguzia haya majaribio yetu kuwa ni malipo kwa wema wako, kama tunavyo walipa walio wema kwa wema wao.
Kiungo 37:104
105
قَدْ صَدَّقْتَ ٱلرُّءْيَآ ۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema. [105]
Maelezo ya chini[105] Na Mwenyezi Mungu akajua umadhubuti wa Ibrahim na mwanawe katika majaribio, Mwenyezi Mungu alimwita Ibrahim kwa wito wa kirafiki: Ewe Ibrahim! Hakika umeuitikia kwa utulivu huo ufunuo wa ndoto, na wala hukusitasita katika kufuata amri. Basi haya yanakutosha. Sisi tunakupunguzia haya majaribio yetu kuwa ni malipo kwa wema wako, kama tunavyo walipa walio wema kwa wema wao.
Kiungo 37:105
106
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْبَلَـٰٓؤُا۟ ٱلْمُبِينُ
Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri. [106]
Maelezo ya chini[106] Hakika majaribio haya tuliyo mjaribia Ibrahim na mwanawe bila ya shaka ni majaribio yaliyo dhihirisha undani wa Imani yao na yakini yao kwa Mola Mlezi wa walimwengu.
Kiungo 37:106
107
وَفَدَيْنَـٰهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍۢ
Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu. [107]
Maelezo ya chini[107] Na tukamkomboa kwa mhanga wenye cheo kikubwa, kwa kuwa hayo ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
Kiungo 37:107
108
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye. [108]
Maelezo ya chini[108] Na tukaacha atajike kwa sifa nzuri katika ndimi za walio kuja baada yake.
Kiungo 37:108
109
سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ
Iwe salama kwa Ibrahim!. [109]
Maelezo ya chini[109] Maamkio ya amani na salama kwa Ibrahim!
Kiungo 37:109
110
كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. [110]
Maelezo ya chini[110] Mfano wa malipo kama haya ya kuwakinga na balaa ndivyo tunavyo walipa walio wema katika kufuata amri za Mwenyezi Mungu.
Kiungo 37:110
111
إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. [111]
Maelezo ya chini[111] Hakika Ibrahim ni katika waja wetu wanao ifuata Haki.
Kiungo 37:111
112
وَبَشَّرْنَـٰهُ بِإِسْحَـٰقَ نَبِيًّۭا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema. [112]
Maelezo ya chini[112] Na kwa amri yetu, Malaika walimbashiria kuwa ataruzukiwa mwana, Is-haqa juu ya kukata tamaa na kuwa mkewe ni tasa. Na kwamba yeye hakika atakuwa Nabii miongoni mwa walio wema.
Kiungo 37:112
113
وَبَـٰرَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰٓ إِسْحَـٰقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌۭ وَظَالِمٌۭ لِّنَفْسِهِۦ مُبِينٌۭ
Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi. [113]
Maelezo ya chini[113] Nasi tukamtunukia yeye na mwanawe baraka na kheri duniani na Akhera. Na miongoni mwa vizazi vyao watatokea watakao jifanyia wema nafsi zao kwa Imani na ut'iifu, na watakao jidhulumu kwa upotovu wa ukafiri na maasi.
Kiungo 37:113
114
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ
Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni. [114]
Maelezo ya chini[114] Na bila ya shaka tuliwaneemesha Musa na Haruni kwa kuwapa Unabii na neema kubwa kubwa.
Kiungo 37:114
115
وَنَجَّيْنَـٰهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ
Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa. [115]
Maelezo ya chini[115] Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa iliyo kuwa iwashukie kutokana na Firauni na kaumu yake.
Kiungo 37:115
116
وَنَصَرْنَـٰهُمْ فَكَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ
Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda. [116]
Maelezo ya chini[116] Na Sisi tukawanusuru na adui zao, wakawa wao ndio wenye kushinda.
Kiungo 37:116
117
وَءَاتَيْنَـٰهُمَا ٱلْكِتَـٰبَ ٱلْمُسْتَبِينَ
Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha. [117]
Maelezo ya chini[117] Na tukampa Musa na Haruni Kitabu kilicho wazi chenye kubainisha hukumu za Dini, nacho ni Taurati.
Kiungo 37:117
118
وَهَدَيْنَـٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ
Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. [118]
Maelezo ya chini[118] Na tukawaongoza waifuate Njia iliyo sawa.
Kiungo 37:118
119
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. [119]
Maelezo ya chini[119] Na tukabakisha sifa njema za kutajika wote wawili hao kwa watu wengineo walio kuja baada yao.
Kiungo 37:119
120
سَلَـٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ
Iwe salama kwa Musa na Haruni!. [120]
Maelezo ya chini[120] Maamkio ya Amani na Salama kwa Musa na Haruni.
Kiungo 37:120
121
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. [121]
Maelezo ya chini[121] Hakika mfano wa malipo tuliyo mjazi Musa na Haruni ndivyo tunavyo wajazi wote walio wema.
Kiungo 37:121
122
إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini. [122]
Maelezo ya chini[122] Hakika wawili hao ni katika waja wetu wenye kuifuata Haki.
Kiungo 37:122
123
وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume. [123]
Maelezo ya chini[123] Na hakika Ilyas ni katika hao tulio watuma kwenda waongoa watu wao.
Kiungo 37:123
124
إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?. [124]
Maelezo ya chini[124] Ilyas alipo waambia watu wake, nao walikuwa wakiyaabudu masanamu yao: Je! Mnaendelea juu ya makosa yenu, na wala hamumkhofu Mwenyezi Mungu mkajikinga na adhabu yake?
Kiungo 37:124
125
أَتَدْعُونَ بَعْلًۭا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ ٱلْخَـٰلِقِينَ
Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,. [125]
Maelezo ya chini[125] Mnaliabudu sanamu linalo itwa Baa'li, na mkaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu aliye uumba ulimwengu na akaufanya mzuri uumbaji wake?
Kiungo 37:125
126
ٱللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ
Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?. [126]
Maelezo ya chini[126] Mwenyezi Mungu amekuumbeni na amekuhifadhini nyinyi na baba zenu wa zamani. Yeye basi ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa.
Kiungo 37:126
127
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ
Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;. [127]
Maelezo ya chini[127] Lakini walimkadhibisha, basi jaza yao ni kuhudhurishwa kwenye Moto Siku ya Kiyama.
Kiungo 37:127
128
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. [128]
Maelezo ya chini[128] Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safisha Imani yao. Hao basi ndio wenye kufuzu.
Kiungo 37:128
129
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye. [129]
Maelezo ya chini[129] Na tukamjaalia awe anatajwa kwa wema na ndimi za walio kuja baada yake.
Kiungo 37:129
130
سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِلْ يَاسِينَ
Iwe salama kwa Ilyas. [130]
Maelezo ya chini[130] Salamu juu ya Ilyasi, au juu yake yeye na watu wake, kwa kuwa kawashinda.
Kiungo 37:130
131
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. [131]
Maelezo ya chini[131] Hakika mfano wa malipo tuliyo mlipa Ilyas tunamlipa kila aliye mwema kwa sababu ya wema wake.
Kiungo 37:131
132
إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. [132]
Maelezo ya chini[132] Hakika Ilyas ni katika waja wetu walio amini.
Kiungo 37:132
133
وَإِنَّ لُوطًۭا لَّمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume. [133]
Maelezo ya chini[133] Na hakika Lut'i ni katika Mitume tulio watuma ili afikishe Ujumbe wetu kwa watu.
Kiungo 37:133
134
إِذْ نَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ
Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,. [134]
Maelezo ya chini[134] Kwa hakika Sisi tumemwokoa yeye na ahali zake wote kutokana na adhabu iliyo wasibu watu wake.
Kiungo 37:134
135
إِلَّا عَجُوزًۭا فِى ٱلْغَـٰبِرِينَ
Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma. [135]
Maelezo ya chini[135] Ila mkewe mkongwe. Yeye bila ya shaka aliteketea pamoja na walio teketea.
Kiungo 37:135
136
ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
Kisha tukawaangamiza wale wengineo. [136]
Maelezo ya chini[136] Kisha tukawaangamiza wote isipo kuwa Lut'i na walio muamini.
Kiungo 37:136
137
وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ
Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,. [137]
Maelezo ya chini[137] Na hakika nyinyi, watu wa Makka, mnayapitia majumba ya hao kaumu Lut'i katika safari zenu za kwendea Sham asubuhi au usiku. Je! Mmepotelewa na akili zenu hata hamwezi kuzingatia yaliyo wapitia hao kuwa ni malipo ya ukanushaji wao?
Kiungo 37:137
138
وَبِٱلَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?. [138]
Maelezo ya chini[138] Na hakika nyinyi, watu wa Makka, mnayapitia majumba ya hao kaumu Lut'i katika safari zenu za kwendea Sham asubuhi au usiku. Je! Mmepotelewa na akili zenu hata hamwezi kuzingatia yaliyo wapitia hao kuwa ni malipo ya ukanushaji wao?
Kiungo 37:138
139
وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume. [139]
Maelezo ya chini[139] Na hakika Yunus ni miongoni mwa tulio watuma wawafikishie Ujumbe wetu watu.
Kiungo 37:139
140
إِذْ أَبَقَ إِلَى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ
Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni. [140]
Maelezo ya chini[140] Alipo wahama watu wake bila ya amri ya Mola wake Mlezi, akaliendea jahazi ambalo lilio kwisha sheheni pomoni, akalipanda. Jahazi likapatikana na mambo ikawajibikia lazima mmoja katika abiria atoswe kupunguza shehena yake. Kura ikamuangukia Yunus, akashindwa kwa kura. Akatoswa baharini kwa mujibu wa ada yao zama zile.
Kiungo 37:140
141
فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُدْحَضِينَ
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa. [141]
Maelezo ya chini[141] Alipo wahama watu wake bila ya amri ya Mola wake Mlezi, akaliendea jahazi ambalo lilio kwisha sheheni pomoni, akalipanda. Jahazi likapatikana na mambo ikawajibikia lazima mmoja katika abiria atoswe kupunguza shehena yake. Kura ikamuangukia Yunus, akashindwa kwa kura. Akatoswa baharini kwa mujibu wa ada yao zama zile.
Kiungo 37:141
142
فَٱلْتَقَمَهُ ٱلْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌۭ
Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa. [142]
Maelezo ya chini[142] Samaki akammeza, naye hakika alistahiki lawama kwa kuikimbia kazi yake ya Daa'wa, Wito, kuwaitia watu wafuate Haki, na kuacha kuwasubiria wale walio kwenda kinyume naye..
Kiungo 37:142
143
فَلَوْلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُسَبِّحِينَ
Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,. [143]
Maelezo ya chini[143] Na lau kuwa Yunus hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu, wanao dumu kumdhukuru, angeli kufa ndani ya samaki, wala asingeli toka humo mpaka siku ya kufufuliwa.
Kiungo 37:143
144
لَلَبِثَ فِى بَطْنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa. [144]
Maelezo ya chini[144] Na lau kuwa Yunus hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu, wanao dumu kumdhukuru, angeli kufa ndani ya samaki, wala asingeli toka humo mpaka siku ya kufufuliwa.
Kiungo 37:144
145
۞ فَنَبَذْنَـٰهُ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌۭ
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. [145]
Maelezo ya chini[145] Tukamtupa pahali patupu kwenye nchi pasipo kuwa na miti wala majumba, naye ni mgonjwa kwa yaliyo mpata. Yaliyo mtokea Sayyidna Yunus a.s. ni muujiza. Lakini nayo si muhali kutokea mtu kumezwa na samaki, na akabakia yuhai ndani yake kwa muda fulani. Mawili yaweza kuwa - Kwanza, ni kuwa huyo samaki ni namna asiye kuwa na meno katika kabila ya nyangumi wakubwa kabisa, kama nyangumi wanao onekana sana katika Bahari ya Kati (Mediterranean). Urefu wake huweza kufika Mita 20. Alibaki Yunus katika mpandikizi wa kinywa chake huyo nyangumi mpaka alipo mtema kwenye ufukwe mtupu, kwani koo ya nyangumi ni nyembamba hawezi kupita mtu. Pili, yaweza kuwa huyo samaki ni namna ya wenye meno pia, kama nyangumi wa ambari, na ambaye pia urefu wake hufika mita 20. Hawa mara kadhaa wa kadhaa huonekana katika Bahari ya Kati. Nyangumi hao yawezekana kwa kawaida kuwameza wanyama wakubwa wanao pita urefu wa mita tatu.
Kiungo 37:145
146
وَأَنۢبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةًۭ مِّن يَقْطِينٍۢ
Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye. [146]
Maelezo ya chini[146] Tukauotesha mmea wa kutambaa, usio simama juu ya kigogo, ukamfunika na kumkinga na madhara ya hali ya hewa.
Kiungo 37:146
147
وَأَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ مِا۟ئَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ
Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi. [147]
Maelezo ya chini[147] Hata alipo pata nafuu kutokana na yaliyo msibu, tukamtuma awaendee watu wengi. Wanasema walio waona kuwa wanapata laki moja au zaidi.
Kiungo 37:147
148
فَـَٔامَنُوا۟ فَمَتَّعْنَـٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍۢ
Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda. [148]
Maelezo ya chini[148] Wakauwitikia wito wake, nasi tukawakunjulia neema zetu kwa muda maalumu.
Kiungo 37:148
149
فَٱسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ ٱلْبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلْبَنُونَ
Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?. [149]
Maelezo ya chini[149] Ewe Nabii! Waulize watu wako: Ati Mwenyezi Mungu aliye kuumba ana watoto wa kike kinyume na wao; na wao ndio wana watoto wanaume kinyuma na Yeye?
Kiungo 37:149
150
أَمْ خَلَقْنَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ إِنَـٰثًۭا وَهُمْ شَـٰهِدُونَ
Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?. [150]
Maelezo ya chini[150] Ati tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao hao makafiri waliona kwa macho yao kuumba kwao, na ndio wakasimulia walio yaona?
Kiungo 37:150
151
أَلَآ إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ
Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:. [151]
Maelezo ya chini[151] Ewe mwenye kusikia! Yazingatie maneno yao. Hakika wao kwa uwongo wao wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Na hali Yeye ametakasika na upungufu kama huo wa kuwa mzazi au kuzaliwa. Na hakika bila ya shaka hao ni waongo kwa usemi huo, kwa ushahidi wa dalili nyingi za Upweke wake.
Kiungo 37:151
152
وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ
Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!. [152]
Maelezo ya chini[152] Ewe mwenye kusikia! Yazingatie maneno yao. Hakika wao kwa uwongo wao wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Na hali Yeye ametakasika na upungufu kama huo wa kuwa mzazi au kuzaliwa. Na hakika bila ya shaka hao ni waongo kwa usemi huo, kwa ushahidi wa dalili nyingi za Upweke wake.
Kiungo 37:152
153
أَصْطَفَى ٱلْبَنَاتِ عَلَى ٱلْبَنِينَ
Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?. [153]
Maelezo ya chini[153] Ati Yeye amejichagulia mwenyewe mabinti ambao kwa madai yenu ndio mnawachukia kuliko watoto wa kiume ambao mnawapenda, na hali Yeye ndiye Mwenye kuwaumba wote, watoto wa kike na wa kiume?
Kiungo 37:153
154
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?. [154]
Maelezo ya chini[154] Ni nini lilio kusibuni hata mkakata hukumu bila ya ushahidi? Vipi mnahukumu hivyo na hali ni upotovu ulio wazi?
Kiungo 37:154
155
أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Hamkumbuki?. [155]
Maelezo ya chini[155] Je! Mmesahau dalili za uweza wake na kutakasika kwake, ndio msikumbuke mpaka mkaingia katika upotovu?
Kiungo 37:155
156
أَمْ لَكُمْ سُلْطَـٰنٌۭ مُّبِينٌۭ
Au mnayo hoja iliyo wazi?. [156]
Maelezo ya chini[156] Hebu nyinyi mnazo nguvu za ushahidi wa kubainisha wa kuthibitisha hayo mnayo yadai?
Kiungo 37:156
157
فَأْتُوا۟ بِكِتَـٰبِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli. [157]
Maelezo ya chini[157] Basi leteni hoja zenu, ikiwa mnazo hoja za katika Kitabu cha mbinguni, kama nyinyi ni wakweli katika hayo myasemayo na mnayo yahukumia.
Kiungo 37:157
158
وَجَعَلُوا۟ بَيْنَهُۥ وَبَيْنَ ٱلْجِنَّةِ نَسَبًۭا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ ٱلْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ
Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa. [158]
Maelezo ya chini[158] Wakashikilia katika itikadi zao, na wakazua baina ya Mwenyezi Mungu na majini, ambao hawawaoni, kuwa ati yapo makhusiano ya nasaba. Na bila ya shaka hao majini walikwisha jua kuwa makafiri watahudhurishwa mbele ya Mwenyezi Mungu ili wapate malipo yao yasiyo kimbilika.
Kiungo 37:158
159
سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ
Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia. [159]
Maelezo ya chini[159] Mwenyezi Mungu Mtukufu ametakasika na hizo sifa za kuemewa na za upungufu wanazo mzulia kuwa anazo.
Kiungo 37:159
160
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. [160]
Maelezo ya chini[160] Lakini waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa wakasafishwa hawana makosa ya huo uzushi wa makafiri.
Kiungo 37:160
161
فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ
Basi hakika nyinyi na mnao waabudu. [161]
Maelezo ya chini[161] Enyi makafiri! Hakika nyinyi, na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu - Nyinyi kwa kuwaabudu kwenu badala yake Yeye, hamtampoteza yeyote kwa upotovu wenu. Isipo kuwa yule ambaye tangu hapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua ni katika watu wa Motoni, na huko ataingia.
Kiungo 37:161
162
مَآ أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَـٰتِنِينَ
Hamwezi kuwapoteza. [162]
Maelezo ya chini[162] Enyi makafiri! Hakika nyinyi, na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu - Nyinyi kwa kuwaabudu kwenu badala yake Yeye, hamtampoteza yeyote kwa upotovu wenu.
Kiungo 37:162
163
إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ ٱلْجَحِيمِ
Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni. [163]
Maelezo ya chini[163] Isipo kuwa yule ambaye tangu hapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua ni katika watu wa Motoni, na huko ataingia.
Kiungo 37:163
164
وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٌۭ مَّعْلُومٌۭ
Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu. [164]
Maelezo ya chini[164] Na Malaika kuwania kuwa wao ni waja wa Mwenyezi Mungu, wakasema: Hapana yeyote katika sisi ila ana cheo chake maalumu katika ujuzi, na ibada, na wala hakikiuki hicho.
Kiungo 37:164
165
وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلصَّآفُّونَ
Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu. [165]
Maelezo ya chini[165] Na sisi tumejipanga safu wenyewe katika misimamo ya kutumika daima.
Kiungo 37:165
166
وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلْمُسَبِّحُونَ
Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa. [166]
Maelezo ya chini[166] Na hakika sisi bila ya shaka yoyote ndio wenye kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila lisilo kuwa na maelekeo naye katika kila hali.
Kiungo 37:166
167
وَإِن كَانُوا۟ لَيَقُولُونَ
Na walikuwapo walio kuwa wakisema:. [167]
Maelezo ya chini[167] Na walikuwapo makafiri wa Makka kabla ya kuteuliwa Mtume s.a.w. ambao wakisema:
Kiungo 37:167
168
لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًۭا مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ
Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,. [168]
Maelezo ya chini[168] Lau kuwa sisi tungeli kuwa na Kitabu kama Vitabu vya watu wa zamani, yaani kama Taurati na Injili, nasi bila ya shaka tungeli kuwa waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumsafia ibada Yeye.
Kiungo 37:168
169
لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ
Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi. [169]
Maelezo ya chini[169] Nasi bila ya shaka tungeli kuwa waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumsafia ibada Yeye.
Kiungo 37:169
170
فَكَفَرُوا۟ بِهِۦ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Lakini waliukataa. Basi watakuja jua. [170]
Maelezo ya chini[170] Na Kitabu kikawajia, nao wakakikataa. Basi watakuja jua nini matokeo ya kukataa kwao.
Kiungo 37:170
171
وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلْمُرْسَلِينَ
Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. [171]
Maelezo ya chini[171] Ninaapa! Hukumu yetu kwa Mitume tulio watuma imekwisha tolewa mbele, ya kwamba ushindi na matokeo mema ni yao wao dhidi ya makafiri.
Kiungo 37:171
172
إِنَّهُمْ لَهُمُ ٱلْمَنصُورُونَ
Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa. [172]
Maelezo ya chini[172] Ninaapa! Hukumu yetu kwa Mitume tulio watuma imekwisha tolewa mbele, ya kwamba ushindi na matokeo mema ni yao wao dhidi ya makafiri.
Kiungo 37:172
173
وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ
Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda. [173]
Maelezo ya chini[173] Na kwamba wafuasi wetu na wasaidizi wetu ndio peke yao watakao washinda walio kengeuka.
Kiungo 37:173
174
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍۢ
Basi waachilie mbali kwa mda. [174]
Maelezo ya chini[174] Basi waachilie mbali, nawe ngoja mpaka wakati ujao. Kwani Sisi tutakupa wewe matokeo mema, na manusura, na ushindi.
Kiungo 37:174
175
وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ
Na watazame, nao wataona. [175]
Maelezo ya chini[175] Nawe watazame, na uangalie vyema adhabu gani na mateso yatakayo wapata kwa kwenda kinyume nawe na kukukadhibisha. Basi watakuja ona kwa macho yao zitakavyo shindwa safu zao, na wataona nusura ya Mwenyezi Mungu inavyo wafikia Waumini.
Kiungo 37:175
176
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ
Je! Wanaihimiza adhabu yetu?. [176]
Maelezo ya chini[176] Je! Wamepoteza akili zao nini, hata wakawa wanaihimiza adhabu yetu?
Kiungo 37:176
177
فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلْمُنذَرِينَ
Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa. [177]
Maelezo ya chini[177] Basi adhabu hiyo itakapo teremka kwenye uwanja wao mpana, itakuwa asubuhi ovu kweli hiyo kwa hao walio onywa na adhabu.
Kiungo 37:177
178
وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍۢ
Na waache kwa muda. [178]
Maelezo ya chini[178] Na waachilie mbali mpaka mambo yatakapo waishia.
Kiungo 37:178
179
وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ
Na tazama, na wao wataona. [179]
Maelezo ya chini[179] Na yaangalie yatakayo wafika wao na yatakayo kufika wewe. Wao watakuja yaona hayo wanayo yahimiza.
Kiungo 37:179
180
سُبْحَـٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ
Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia. [180]
Maelezo ya chini[180] Mwenyezi Mungu, aliye kuumba wewe na aliye ziumba nguvu na ushindi, ametakasika na huo uzushi wanao muambatisha naye.
Kiungo 37:180
181
وَسَلَـٰمٌ عَلَى ٱلْمُرْسَلِينَ
Na Salamu juu ya Mitume. [181]
Maelezo ya chini[181] Na salamu zishuke juu ya Mitume wapenzi walio safika.
Kiungo 37:181
182
وَٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. [182]
Maelezo ya chini[182] Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu peke yake, Muumba wa viumbe vyote, na Mwenye kuwaangalia makhaluku wote.
Kiungo 37:182

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure