Sura ya 69 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Haqqa (Tukio la Haki)

سُورَةُ الحَاقَّةِ
Aya 52

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
ٱلْحَآقَّةُ
Tukio la haki. [1]
Maelezo ya chini[1] Kiyama ni Tukio litakalo tukia kwa haki, yaani kwa kweli.
Kiungo 69:1
2
مَا ٱلْحَآقَّةُ
Nini hilo Tukio la haki? [2]
Maelezo ya chini[2] Nini hicho Kiyama kitacho tokea kweli?
Kiungo 69:2
3
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْحَآقَّةُ
Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki? [3]
Maelezo ya chini[3] Na kitu gani kitacho kujuvya ukweli wake, na kitacho kupa sura ya kitisho chake na shida zake?
Kiungo 69:3
4
كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌۢ بِٱلْقَارِعَةِ
Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha. [4]
Maelezo ya chini[4] Kina Thamudi na kina A'di walikanusha Kiyama kinacho wagutua walimwengu wote kwa kitisho chake na shida zake.
Kiungo 69:4
5
فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا۟ بِٱلطَّاغِيَةِ
Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. [5]
Maelezo ya chini[5] Ama Thamudi basi walihilikiwa kwa tukio lilio pindukia mipaka yote kwa ukali wake.
Kiungo 69:5
6
وَأَمَّا عَادٌۭ فَأُهْلِكُوا۟ بِرِيحٍۢ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍۢ
Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika. [6]
Maelezo ya chini[6] Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo ubaridi na mkali,
Kiungo 69:6
7
سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍۢ وَثَمَـٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًۭا فَتَرَى ٱلْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍۢ
Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani. [7]
Maelezo ya chini[7] Mwenyezi Mungu aliwasalitisha nao muda wa masiku saba, na siku nane zilizo fuatana mfululizo, utaona walio patikana na upepo huo wamekuwa maiti kama magogo ya mitende yaliyo kuwa matupu ndani yake. ("Masiku" ni wingi wa "Usiku"; "Siku" wingi wake ni "Siku" vile vile.)
Kiungo 69:7
8
فَهَلْ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٍۢ
Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki? [8]
Maelezo ya chini[8] Je! Unamwona yeyote aliye bakia katika hao?
Kiungo 69:8
9
وَجَآءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُۥ وَٱلْمُؤْتَفِكَـٰتُ بِٱلْخَاطِئَةِ
Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. [9]
Maelezo ya chini[9] Akaja Firauni, na mataifa mengine yaliyo kufuru kabla yake, na wale jamaa walio acha mwendo wa haki na vitendo vya maumbile wakafanya vitendo vichafu kabisa hata miji yao ikapinduliwa juu chini.
Kiungo 69:9
10
فَعَصَوْا۟ رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةًۭ رَّابِيَةً
Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. [10]
Maelezo ya chini[10] Kila umma katika hawa walimuasi Mtume wa Mola wao Mlezi. Naye Mwenyezi Mungu akawashika kwa kuwaadhibu kwa mshiko ulio zidi ukali.
Kiungo 69:10
11
إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلْمَآءُ حَمَلْنَـٰكُمْ فِى ٱلْجَارِيَةِ
Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, [11]
Maelezo ya chini[11] Maji yalipo zidi ukomo wake, na yakapanda juu ya milima katika tukio la tofani ya Nuhu, Sisi tulikupandisheni, yaani kwa kuwapandisha wazee wenu wa asli, katika safina inayo kwenda baharini.
Kiungo 69:11
12
لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةًۭ وَتَعِيَهَآ أُذُنٌۭ وَٰعِيَةٌۭ
Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. [12]
Maelezo ya chini[12] Ili kulifanya tukio hilo la kuwaokoa Waumini na kuwazamisha makafiri liwe zingatio na mawaidha kwenu, na lihifadhiwe na kila sikio lenye kuhifadhi linalo sikia.
Kiungo 69:12
13
فَإِذَا نُفِخَ فِى ٱلصُّورِ نَفْخَةٌۭ وَٰحِدَةٌۭ
. Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, [13]
Maelezo ya chini[13] Litakapo pulizwa barugumu kwa mpulizo mmoja,
Kiungo 69:13
14
وَحُمِلَتِ ٱلْأَرْضُ وَٱلْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةًۭ وَٰحِدَةًۭ
Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, [14]
Maelezo ya chini[14] Na ardhi na milima ikaondolewa pahala ilipo, na ikavunjwa mara moja,
Kiungo 69:14
15
فَيَوْمَئِذٍۢ وَقَعَتِ ٱلْوَاقِعَةُ
Siku hiyo ndio Tukio litatukia. [15]
Maelezo ya chini[15] Siku hiyo ndiyo kitashuka cha kushuka,
Kiungo 69:15
16
وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِىَ يَوْمَئِذٍۢ وَاهِيَةٌۭ
Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. [16]
Maelezo ya chini[16] Na mbingu zitapasuka kwa kuondoka hukumu zake na sharia zake, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu baada ya kuwa madhubuti zenye nguvu.
Kiungo 69:16
17
وَٱلْمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرْجَآئِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍۢ ثَمَـٰنِيَةٌۭ
Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. [17]
Maelezo ya chini[17] Na Malaika pembezoni mwake, na wapo Malaika wanane siku hiyo watakao beba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi, juu ya Malaika hawa wengine.
Kiungo 69:17
18
يَوْمَئِذٍۢ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌۭ
Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. [18]
Maelezo ya chini[18] Siku hiyo ndio mtaletwa kwa ajili ya kuhisabiwa. Wala haifichikani siri yenu yoyote mliyo kuwa mkiificha.
Kiungo 69:18
19
فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقْرَءُوا۟ كِتَـٰبِيَهْ
Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! [19]
Maelezo ya chini[19] Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwatangazia furaha yake walio karibu naye: Chukueni msome kitabu changu!
Kiungo 69:19
20
إِنِّى ظَنَنتُ أَنِّى مُلَـٰقٍ حِسَابِيَهْ
Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. [20]
Maelezo ya chini[20] Mimi nilikuwa na yakini tangu duniani kuwa nitapata hisabu yangu, basi nikajitayarisha nafsi yangu kwa mkutano huu.
Kiungo 69:20
21
فَهُوَ فِى عِيشَةٍۢ رَّاضِيَةٍۢ
Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, [21]
Maelezo ya chini[21] Basi huyo atakuwa katika maisha yaliyo enea kupendeza.
Kiungo 69:21
22
فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍۢ
Katika Bustani ya juu, [22]
Maelezo ya chini[22] Katika Bustani ya pahali na daraja ya juu.
Kiungo 69:22
23
قُطُوفُهَا دَانِيَةٌۭ
Matunda yake yakaribu. [23]
Maelezo ya chini[23] Matunda yake yakaribu kwa kuyachuma. (kuyatunda).
Kiungo 69:23
24
كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَآ أَسْلَفْتُمْ فِى ٱلْأَيَّامِ ٱلْخَالِيَةِ
Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. [24]
Maelezo ya chini[24] Kuleni na mnywe kwa kula na kunywa kusio na karaha, wala maudhi, kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kwisha vitanguliza katika siku za duniani zilizo pita.
Kiungo 69:24
25
وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى لَمْ أُوتَ كِتَـٰبِيَهْ
Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! [25]
Maelezo ya chini[25] Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto atasema kwa majuto na huzuni: Laiti kuwa sikupewa kitabu changu,
Kiungo 69:25
26
وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ
Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. [26]
Maelezo ya chini[26] Wala sikuijua hisabu yangu!
Kiungo 69:26
27
يَـٰلَيْتَهَا كَانَتِ ٱلْقَاضِيَةَ
Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. [27]
Maelezo ya chini[27] Laiti kuwa kule kufa niliko kwisha kufa kungeli kuwa ndio kumalizika kwangu kwa mwisho, wala nisingeli fufuliwa tena!
Kiungo 69:27
28
مَآ أَغْنَىٰ عَنِّى مَالِيَهْ ۜ
Mali yangu hayakunifaa kitu. [28]
Maelezo ya chini[28] Hapana chochote nilicho kimiliki duniani kilicho nifaa.
Kiungo 69:28
29
هَلَكَ عَنِّى سُلْطَـٰنِيَهْ
Madaraka yangu yamenipotea. [29]
Maelezo ya chini[29] Uzima wangu umenipotea, na nguvu zangu zimenitoka.
Kiungo 69:29
30
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ
(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! [30]
Maelezo ya chini[30] Wataambiwa walinzi wa Jahannamu: Mshikeni, na mfungeni mikono yake kwenye shingo yake.
Kiungo 69:30
31
ثُمَّ ٱلْجَحِيمَ صَلُّوهُ
Kisha mtupeni Motoni! [31]
Maelezo ya chini[31] Kisha msimtie popote ila ndani ya Moto wa Jahannamu,
Kiungo 69:31
32
ثُمَّ فِى سِلْسِلَةٍۢ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًۭا فَٱسْلُكُوهُ
Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! [32]
Maelezo ya chini[32] Kisha mfungeni kwenye mnyororo mrefu kabisa.
Kiungo 69:32
33
إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ ٱلْعَظِيمِ
Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, [33]
Maelezo ya chini[33] Hakika huyo alikuwa hamsadiki Mwenyezi Mungu Mtukufu,
Kiungo 69:33
34
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ
Wala hahimizi kulisha masikini. [34]
Maelezo ya chini[34] Wala hamhimizi yoyote kuwalisha masikini.
Kiungo 69:34
35
فَلَيْسَ لَهُ ٱلْيَوْمَ هَـٰهُنَا حَمِيمٌۭ
Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, [35]
Maelezo ya chini[35] Basi hii leo huyu kafiri hana jamaa wa kumtetea,
Kiungo 69:35
36
وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍۢ
Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. [36]
Maelezo ya chini[36] Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni, ambao kwa hakika ni mchanganyiko wa damu na usaha.
Kiungo 69:36
37
لَّا يَأْكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلْخَـٰطِـُٔونَ
Chakula hicho hawakili ila wakosefu. [37]
Maelezo ya chini[37] Hawakili chakula hicho ila wakosefu walio kusudia kufanya maasi yao, na wakakamia kuendelea nayo.
Kiungo 69:37
38
فَلَآ أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ
Basi naapa kwa mnavyo viona, [38]
Maelezo ya chini[38] Basi naapa kwa mnavyo viona katika vinavyo onekana,
Kiungo 69:38
39
وَمَا لَا تُبْصِرُونَ
Na msivyo viona, [39]
Maelezo ya chini[39] Basi naapa kwa mnavyo viona katika vinavyo onekana, na msivyo viona katika ulimwengu wa ghaibu,
Kiungo 69:39
40
إِنَّهُۥ لَقَوْلُ رَسُولٍۢ كَرِيمٍۢ
Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. [40]
Maelezo ya chini[40] Kwamba hakika Qur'ani bila ya shaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ulimi wa Mjumbe mwenye cheo cha juu.
Kiungo 69:40
41
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍۢ ۚ قَلِيلًۭا مَّا تُؤْمِنُونَ
Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. [41]
Maelezo ya chini[41] Wala Qur'ani si maneno ya mtunga mashairi kama mnavyo dai. Ama nyinyi ni chache mno imani yenu ya kuwa Qur'ani inatoka kwa Mwenyezi Mungu.
Kiungo 69:41
42
وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍۢ ۚ قَلِيلًۭا مَّا تَذَكَّرُونَ
Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. [42]
Maelezo ya chini[42] Wala Qur'ani haisemi kwa maneno ya kumunyia munyia kama wanenavyo makuhani mlio wazoea. Ni uchache mno kukumbuka kwenu na kuzingatia khitilafu zilioko baina ya Qur'ani na maneno ya makuhani.
Kiungo 69:42
43
تَنزِيلٌۭ مِّن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [43]
Maelezo ya chini[43] Hii ni uteremsho unao toka kwa Mwenye kuwaangalia walimwengu wote kwa kuwaumba na kuwalea.
Kiungo 69:43
44
وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ ٱلْأَقَاوِيلِ
Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, [44]
Maelezo ya chini[44] Na lau kuwa angeli dai kitu chochote ambacho tusicho kisema
Kiungo 69:44
45
لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِٱلْيَمِينِ
Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, [45]
Maelezo ya chini[45] Basi bila ya shaka tungeli mshika akitoe kama mtu anavyo mkamata mtu kwa mkono wa kulia akammaliza hapo hapo.
Kiungo 69:45
46
ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ ٱلْوَتِينَ
Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo! [46]
Maelezo ya chini[46] Kisha bila ya shaka tungeli mkata mshipa wake wa moyo, afe saa ile ile. (Biblia inasema katika Kumbukumbu la Torati 18.20 "Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.")
Kiungo 69:46
47
فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَـٰجِزِينَ
Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia. [47]
Maelezo ya chini[47] Na hapana yeyote katika nyinyi, hata ange kuwa na nguvu namna gani, angeli weza kuzuia adhabu yetu isimfikilie.
Kiungo 69:47
48
وَإِنَّهُۥ لَتَذْكِرَةٌۭ لِّلْمُتَّقِينَ
Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu. [48]
Maelezo ya chini[48] Na hakika Qur'ani ni mawaidha kwa wanao fuata amri za Mwenyezi Mungu, na wanaepuka makatazo yake.
Kiungo 69:48
49
وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ
Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha. [49]
Maelezo ya chini[49] Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba kati yenu wapo wanao ikanusha Qur'ani.
Kiungo 69:49
50
وَإِنَّهُۥ لَحَسْرَةٌ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ
Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa. [50]
Maelezo ya chini[50] Na kwamba hakika hiyo bila ya shaka ni sababu ya majuto ya wanao ikataa, wakati watapo iona adhabu yao, na neema za wenye kusadiki.
Kiungo 69:50
51
وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلْيَقِينِ
Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. [51]
Maelezo ya chini[51] Na hakika Qur'ani bila ya shaka ni Haki iliyo thibiti, isiyo na shaka yoyote.
Kiungo 69:51
52
فَسَبِّحْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلْعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. [52]
Maelezo ya chini[52] Basi mtakase Mola wako Mlezi, na dumisha kudhukuru jina lake.
Kiungo 69:52

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure