Sura ya 91 kati ya 114 · Makkiya

Sura Ash-Shams (Jua)

سُورَةُ الشَّمۡسِ
Aya 15

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلشَّمْسِ وَضُحَىٰهَا
Naapa kwa jua na mwangaza wake! [1]
Maelezo ya chini[1] Naapa kwa jua na mwangaza wake na kuchomoza kwake na kwa joto lake!
Kiungo 91:1
2
وَٱلْقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا
Na kwa mwezi unapo lifuatia! [2]
Maelezo ya chini[2] Na kwa mwezi unapo lifuata na likawa nyuma yake kwa kutoa mwangaza baada ya kuchwa jua,
Kiungo 91:2
3
وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا
Na kwa mchana unapo lidhihirisha! [3]
Maelezo ya chini[3] Na kwa mchana unapo lidhihirisha jua, likaonekana wazi halikufichikana.
Kiungo 91:3
4
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰهَا
Na kwa usiku unapo lifunika! [4]
Maelezo ya chini[4] Na kwa usiku unapo lifunika jua, ukawa mwangaza wake hauonekani.
Kiungo 91:4
5
وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! [5]
Maelezo ya chini[5] Na kwa mbingu na kwa Mweza Mtukufu aliye inyanyua na akaijenga kwa hikima yake.
Kiungo 91:5
6
وَٱلْأَرْضِ وَمَا طَحَىٰهَا
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! [6]
Maelezo ya chini[6] Na kwa ardhi na kwa Mweza Mtukufu aliye ikunjua kwa kila upande, na akaitengeneza kwa ajili ya utulivu, na akaifanya kama tandiko.
Kiungo 91:6
7
وَنَفْسٍۢ وَمَا سَوَّىٰهَا
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! [7]
Maelezo ya chini[7] Na kwa nafsi, na aliye iumba na akaiweka sawa, kwa kuipa nguvu,
Kiungo 91:7
8
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَىٰهَا
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake! [8]
Maelezo ya chini[8] Akaifunza jema na baya, na akaipa uweza wa kutenda itakayo katika hayo,
Kiungo 91:8
9
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّىٰهَا
Hakika amefanikiwa aliye itakasa! [9]
Maelezo ya chini[9] Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake kwa ut'iifu na vitendo vya kheri.
Kiungo 91:9
10
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا
Na hakika amekhasiri aliye iviza. [10]
Maelezo ya chini[10] Na hakika amekhasiri mwenye kuzificha fadhila zake, na akayaua matayarisho aliyo umbwa nayo ya kutenda kheri.
Kiungo 91:10
11
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَىٰهَآ
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, [11]
Maelezo ya chini[11] Kina Thamudi walimkanusha Nabii wao kwa upotovu wao na jeuri zao,
Kiungo 91:11
12
إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشْقَىٰهَا
Alipo simama mwovu wao mkubwa, [12]
Maelezo ya chini[12] Alipo gutuka mwovu wao mkubwa kabisa kutaka kumchinja ngamia.
Kiungo 91:12
13
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقْيَـٰهَا
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. [13]
Maelezo ya chini[13] Saleh, Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawaambia: Mwachilieni huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ale maridhawa katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, na tahadharini msimzuie maji katika siku yake aliyo wekewa.
Kiungo 91:13
14
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمْ فَسَوَّىٰهَا
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. [14]
Maelezo ya chini[14] Wakamkadhibisha Mtume wao katika hilo onyo lake, wakamchinja. Mola wao Mlezi akazibomoa nyumba zao kwa sababu ya dhambi zao; akazisawazisha na ardhi!
Kiungo 91:14
15
وَلَا يَخَافُ عُقْبَـٰهَا
Wala Yeye haogopi matokeo yake. [15]
Maelezo ya chini[15] Wala Yeye Mwenyezi Mungu hakhofu matokeo ya adhabu hiyo, kwani hiyo ni malipo ya haki kwa yale waliyo yatenda.
Kiungo 91:15

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure