Sura ya 53 kati ya 114 · Makkiya
Sura An-Najm (Nyota)
سُورَةُ النَّجۡمِ
Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ
Naapa kwa nyota inapo tua! [1]
Maelezo ya chini
[1] Ninaapa kwa nyota inapo tua kwa kuchwa, ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.
Kiungo
53:1
2
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. [2]
Maelezo ya chini
[2] ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.
Kiungo
53:2
3
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلْهَوَىٰٓ
Wala hatamki kwa matamanio. [3]
Maelezo ya chini
[3] Wala halitoki katika anayo yatamka ya Qur'ani kwa mapendo ya nafsi yake.
Kiungo
53:3
4
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْىٌۭ يُوحَىٰ
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; . [4]
Maelezo ya chini
[4] Hii Qur'ani anayo itamka si chochote ila ni Wahyi (Ufunuo) ulio toka kwa Mwenyezi Mungu anamfunulia yeye.
Kiungo
53:4
5
عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلْقُوَىٰ
Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu! [5]
Maelezo ya chini
[5] Aliye mfundisha ufunuo huu ni mwenye nguvu nyingi.
Kiungo
53:5
6
ذُو مِرَّةٍۢ فَٱسْتَوَىٰ
Mwenye kutua, akatulia! [6]
Maelezo ya chini
[6] Ambaye ametua akili zake na maoni yake, akasimama sawa sawa katika sura yake;
Kiungo
53:6
7
وَهُوَ بِٱلْأُفُقِ ٱلْأَعْلَىٰ
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho. [7]
Maelezo ya chini
[7] Naye yuko upande wa juu katika mbingu upeo wa macho wa mwenye kuangalia.
Kiungo
53:7
8
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ
Kisha akakaribia na akateremka. [8]
Maelezo ya chini
[8] Kisha Jibrili alimkaribia, na akazidi kukaribia,
Kiungo
53:8
9
فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi. [9]
Maelezo ya chini
[9] hata akawa ukaribu wake ni kiasi ya mipinde miwili, bali karibu kuliko hivyo.
Kiungo
53:9
10
فَأَوْحَىٰٓ إِلَىٰ عَبْدِهِۦ مَآ أَوْحَىٰ
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia. [10]
Maelezo ya chini
[10] Jibrili akamfunulia mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, alicho mfunulia, nao ufunuo huo ni jambo lenye shani kubwa na athari ya mbali kabisa.
Kiungo
53:10
11
مَا كَذَبَ ٱلْفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ
Moyo haukusema uwongo uliyo yaona. [11]
Maelezo ya chini
[11] Moyo wa Muhammad haukukanya yale macho yake yaliyo yaona.
Kiungo
53:11
12
أَفَتُمَـٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ
Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona? [12]
Maelezo ya chini
[12] Hivyo nyinyi mnamkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na mnabishana naye kwa aliyo yaona kwa macho yake?
Kiungo
53:12
13
وَلَقَدْ رَءَاهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ
Na akamwona mara nyingine, [13]
Maelezo ya chini
[13] Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine,
Kiungo
53:13
14
عِندَ سِدْرَةِ ٱلْمُنتَهَىٰ
Penye Mkunazi wa mwisho. [14]
Maelezo ya chini
[14] Katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho".
Kiungo
53:14
15
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلْمَأْوَىٰٓ
Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa. [15]
Maelezo ya chini
[15] Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa.
Kiungo
53:15
16
إِذْ يَغْشَى ٱلسِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ
Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika. [16]
Maelezo ya chini
[16] Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa.
Kiungo
53:16
17
مَا زَاغَ ٱلْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka. [17]
Maelezo ya chini
[17] Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.
Kiungo
53:17
18
لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِ ٱلْكُبْرَىٰٓ
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi. [18]
Maelezo ya chini
[18] Hakika ameona mengi katika Ishara za Mwenyezi Mungu na maajabu yake makubwa makubwa.
Kiungo
53:18
19
أَفَرَءَيْتُمُ ٱللَّـٰتَ وَٱلْعُزَّىٰ
Je! Mmemuona Lata na Uzza? [19]
Maelezo ya chini
[19] Je! Mmeyajua hayo, na mkayafikiri ya kina Lata na Uzza?
Kiungo
53:19
20
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلْأُخْرَىٰٓ
Na Manaat, mwingine wa tatu? [20]
Maelezo ya chini
[20] Na Manata, huyo mwengine wa tatu, mlio wafanya kuwa ni miungu wa kuwaabudu?
Kiungo
53:20
21
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلْأُنثَىٰ
Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake? [21]
Maelezo ya chini
[21] Mkagawa, nyinyi muwe na watoto wa kiume, na mkamfanyia Mwenyezi Mungu awe na watoto wa kike!
Kiungo
53:21
22
تِلْكَ إِذًۭا قِسْمَةٌۭ ضِيزَىٰٓ
Huo ni mgawanyo wa dhulma! [22]
Maelezo ya chini
[22] Huo basi ni ugawaji wa dhulma, mnamgawia Mwenyezi Mungu kile mnacho kichukia nyinyi wenyewe!
Kiungo
53:22
23
إِنْ هِىَ إِلَّآ أَسْمَآءٌۭ سَمَّيْتُمُوهَآ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَـٰنٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهْوَى ٱلْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلْهُدَىٰٓ
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi. [23]
Maelezo ya chini
[23] Hayo masanamu yenu si chochote ila ni majina tu yasiyo na maana yoyote ya kiungu. Mmeyatunga nyinyi na baba zenu kwa kufuata pumbao lenu la upotovu. Mwenyezi Mungu hakuteremsha nayo hoja yoyote ya kusadikisha huo uzushi wenu mnao wadaia. Na hawa hawafuati ila ni dhana tu, na kipendacho nyoyo zao zilio potoka na kuacha maumbile yaliyo sawa. Na hakika yalikwisha wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi yenye uwongofu, laiti wangeli ufuata huo!
Kiungo
53:23
24
أَمْ لِلْإِنسَـٰنِ مَا تَمَنَّىٰ
Ati mtu anakipata kila anacho kitamani? [24]
Maelezo ya chini
[24] Mwanaadamu hapati kila anacho kitamani, ya kupata uombezi wa haya masanamu au mengineyo anayo yatamani kwa nafsi yake.
Kiungo
53:24
25
فَلِلَّهِ ٱلْـَٔاخِرَةُ وَٱلْأُولَىٰ
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera. [25]
Maelezo ya chini
[25] Kwani mambo yote, ya duniani na Akhera, ni ya Mwenyezi Mungu peke yake.
Kiungo
53:25
26
۞ وَكَم مِّن مَّلَكٍۢ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ لَا تُغْنِى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعْدِ أَن يَأْذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرْضَىٰٓ
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia. [26]
Maelezo ya chini
[26] Na malaika wengi wa mbinguni, juu ya ubora wa vyeo vyao, haufai kitu uombezi wao isipo kuwa baada ya kupewa idhini huyo mwombezi na Mwenyewe Mtukufu, na kumridhia huyo mwenye kuombewa.
Kiungo
53:26
27
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ تَسْمِيَةَ ٱلْأُنثَىٰ
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike. [27]
Maelezo ya chini
[27] Hakika hao wasio iamini Akhera ndio bila ya shaka wanao sema kuwa Malaika ni wanawake. Wanasema: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu!
Kiungo
53:27
28
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ ۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغْنِى مِنَ ٱلْحَقِّ شَيْـًۭٔا
Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki. [28]
Maelezo ya chini
[28] Na kwa kauli hii hawana ujuzi wowote. Hawafuati kitu ila dhana zao tu zilio potoka, na dhana haifai kitu mbele ya haki.
Kiungo
53:28
29
فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا
Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia. [29]
Maelezo ya chini
[29] Basi jitenge nao hao makafiri walio ipuuza Qur'ani na ikawa hamu yao si chochote ila uhai wa duniani tu, wakiyakataa yenye maslaha nao.
Kiungo
53:29
30
ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱهْتَدَىٰ
Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka. [30]
Maelezo ya chini
[30] Hayo wanayo yafuata katika itikadi zao, na vitendo vyao ndio ukomo walio yafikilia katika ilimu. Hakika Mola wako Mlezi anamjua vyema anaye shikilia upotovu, na anamjua vyema aliye elekea kupokea uwongofu.
Kiungo
53:30
31
وَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ لِيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَسَـٰٓـُٔوا۟ بِمَا عَمِلُوا۟ وَيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ بِٱلْحُسْنَى
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema. [31]
Maelezo ya chini
[31] Na ni vya Mwenyezi Mungu pekee vyote viliomo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba na kuvidabiri, ili awalipe walio potea wenye kufanya viovu vitendo vyao, na awalipe walio hidika watu wema kwa malipo yaliyo mema.
Kiungo
53:31
32
ٱلَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَـٰٓئِرَ ٱلْإِثْمِ وَٱلْفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌۭ فِى بُطُونِ أُمَّهَـٰتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوٓا۟ أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu. [32]
Maelezo ya chini
[32] Wema hao ndio wale wanao jitenga na madhambi yenye adhabu kubwa kubwa, na yanayo chukiza mno. Lakini Mwenyezi Mungu husamehe dhambi ndogo ndogo. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkuu wa kughufiria, naye anajua vyema hali zenu. Kwani Yeye ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu katika hali zenu mbali mbali za kukua na kugeuka. Basi msikae mkijisifu nafsi zenu kuwa mmesafika kwa kujigamba na kujifakhari. Na Yeye ndiye Mjuzi mkubwa kabisa wa kila mwenye kumcha na akajisafisha nafsi yake kweli kweli kwa uchamngu wake.
Kiungo
53:32
33
أَفَرَءَيْتَ ٱلَّذِى تَوَلَّىٰ
Je! Umemwona yule aliye geuka? [33]
Maelezo ya chini
[33] Je! Umezingatia ukamwona anaye puuza kuifuata Haki,
Kiungo
53:33
34
وَأَعْطَىٰ قَلِيلًۭا وَأَكْدَىٰٓ
Na akatoa kidogo, kisha akajizuia? [34]
Maelezo ya chini
[34] Na akatoa kidogo katika mali, na khalafu akakata kabisa kutoa?
Kiungo
53:34
35
أَعِندَهُۥ عِلْمُ ٱلْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? [35]
Maelezo ya chini
[35] Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali?
Kiungo
53:35
36
أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِى صُحُفِ مُوسَىٰ
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? [36]
Maelezo ya chini
[36] Kwani huyo hakuambiwa yaliomo katika Vitabu vya Musa
Kiungo
53:36
37
وَإِبْرَٰهِيمَ ٱلَّذِى وَفَّىٰٓ
Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi? [37]
Maelezo ya chini
[37] Na Ibrahim, aliye fika ukomo wa kutimiza aliyo agana na Mwenyezi Mungu,
Kiungo
53:37
38
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌۭ وِزْرَ أُخْرَىٰ
Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? [38]
Maelezo ya chini
[38] Ya kwamba hapana mtu ataye mbebea dhambi mwenginewe?
Kiungo
53:38
39
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَـٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe? [39]
Maelezo ya chini
[39] Na kwamba mtu hapati ila malipo ya vitendo vyake mwenyewe.
Kiungo
53:39
40
وَأَنَّ سَعْيَهُۥ سَوْفَ يُرَىٰ
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? [40]
Maelezo ya chini
[40] Na kwamba vitendo vyake vitakuja tangazwa, na ataviona Siku ya Kiyama, iwe ni kumtukuza mtenda mema, na kumkebehi mtenda maovu.
Kiungo
53:40
41
ثُمَّ يُجْزَىٰهُ ٱلْجَزَآءَ ٱلْأَوْفَىٰ
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu. [41]
Maelezo ya chini
[41] Kisha kila mtu atalipwa malipo anayo stahiki.
Kiungo
53:41
42
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلْمُنتَهَىٰ
Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho. [42]
Maelezo ya chini
[42] Na kwamba kwa hakika ni kwa Mola wako Mlezi, wala si kwa mwenginewe, ndio miadi ya kurejea.
Kiungo
53:42
43
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio. [43]
Maelezo ya chini
[43] Na Yeye peke yake ni Mwenye uweza wa kuufanya uso uonyeshe furaha au maudhiko, na pia ni Mwenye kuziumba sababu za starehe na dhiki.
Kiungo
53:43
44
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا
Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha. [44]
Maelezo ya chini
[44] Na hakika ni Yeye, ndiye Mwenye kuondoa uhai, na kuuleta.
Kiungo
53:44
45
وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike [45]
Maelezo ya chini
[45] Na Yeye ndiye aliye umba vitu kwa jozi, yaani dume na jike, binaadamu na wanyama,
Kiungo
53:45
46
مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa. [46]
Maelezo ya chini
[46] Kutokana na manii yanayo miminwa. Makusudio ya Aya hii tukufu ni kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Yeye ameumba waume na wake katika wanaadamu na wanyama wote kutokana na tone ya manii ambayo humo humo mna ume na uke. Na juu ya udogo wake na udhaifu wake ndio chemchem ya uhai. Umuujiza wa Qur'ani unadhihirika katika Aya hii tukufu ukikumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa haujui mpaka hivi karibu kuwa katika maji ya mwanamume ndio zimo mbegu "sperms" na katika maji ya mwanamke mna vijiyai "ova", ndio vikikutana vijidudu vya manii ya mwanamume na vijiyai vya mwanamke vikawa kitu kimoja ndio hiyo huwa mimba. Ukweli huu ulitajwa na Qur'ani kabla ya kuvumbuliwa na ilimu za Sayansi.
Kiungo
53:46
47
وَأَنَّ عَلَيْهِ ٱلنَّشْأَةَ ٱلْأُخْرَىٰ
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine. [47]
Maelezo ya chini
[47] Na juu yake Yeye ndio kufufua baada ya kifo.
Kiungo
53:47
48
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ
Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha. [48]
Maelezo ya chini
[48] Na Yeye ndiye anaye toa kinacho tosheleza, na akaridhisha kwa kinacho kinaisha na cha kuweka akiba.
Kiungo
53:48
49
وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعْرَىٰ
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra. [49]
Maelezo ya chini
[49] Na hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa hii nyota kubwa inayo itwa Shii'ra (Sirius, Dog Star). Makusudio hapa ni Nyota hiyo inayo itwa Ash-shi'ra Alyamaaniya, au wanavyo ita Wazungu Sirius au Dog Star. Nyota hii inang'ara kwa nguvu zaidi kuliko nyota zote ziliomo katika kikundi cha nyota kinacho itwa Alkalbu l-akbar, kwa Kizungu Canis Major au Greater Dog. Nyota hiyo ndiyo inayo zagaa sana mbinguni, na huonekana kusini ya mstari wa kati wa mbinguni kiasi ya daraja 18. Na kwa jina hilo la Nyota ya Mbwa ikijuulikana hata miaka elfu tatu ilio pita. Katika mabaki ya michoro ya Mafirauni wa Misri imeashiriwa pia. Mwenyezi Mungu ameitaja khasa kwa kuwa Waarabu walikuwa wakiiabudu hapo kale, na pia Wamisri wa zamani, kwani kutokea kwake upande wa mashariki katikati ya mwezi wa Julai kabla ya kuchomoza jua kulikuwa kunawafikiana na wakati wa mafuriko ya Misri ya kati, yaani katika tukio muhimu kabisa katika ulimwengu huo wa kale. Na tukio hili huenda ndilo lilio fanya kuanzisha kuwekea kiwango urefu wa mwaka katika dunia nzima. Kwani kudhihiri Nyota ya Shiira kabla ya kuchomoza jua hakutokei ila mara moja tu katika mwaka. Basi huu ndio mwanzo wa mwaka mpya.
Kiungo
53:49
50
وَأَنَّهُۥٓ أَهْلَكَ عَادًا ٱلْأُولَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza, [50]
Maelezo ya chini
[50] Na Yeye ndiye aliye wateketeza kina A'di wa mwanzo, kaumu ya Nabii Hudi. Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.
Kiungo
53:50
51
وَثَمُودَا۟ فَمَآ أَبْقَىٰ
Na Thamudi hakuwabakisha, [51]
Maelezo ya chini
[51] Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.
Kiungo
53:51
52
وَقَوْمَ نُوحٍۢ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi; [52]
Maelezo ya chini
[52] Na aliwaangamiza kaumu ya Nuhu kabla ya kuwaangamiza A'di na Thamudi. Hakika hao walikuwa wamekithiri kudhulumu, na wamezidi kwa uasi kuliko A'di na Thamudi.
Kiungo
53:52
53
وَٱلْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ
Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua. [53]
Maelezo ya chini
[53] Na miji ya kaumu Lut'i iliyo pinduliwa juu chini, ni Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye ipindua.
Kiungo
53:53
54
فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ
Vikaifunika vilivyo funika. [54]
Maelezo ya chini
[54] Akaizunguka kwa kuiadhibu kama alivyo izunguka.
Kiungo
53:54
55
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka? [55]
Maelezo ya chini
[55] Basi katika neema za Mola wako Mlezi una shaka nayo ipi?
Kiungo
53:55
56
هَـٰذَا نَذِيرٌۭ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلْأُولَىٰٓ
Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani. [56]
Maelezo ya chini
[56] Hii Qur'ani ni onyo katika jinsi ya yale yale maonyo ya kale waliyo onywa kwayo watu walio tangulia.
Kiungo
53:56
57
أَزِفَتِ ٱلْـَٔازِفَةُ
Kiyama kimekaribia! [57]
Maelezo ya chini
[57] Kiyama kimekaribia;
Kiungo
53:57
58
لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ
Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu. [58]
Maelezo ya chini
[58] Na wala hapana wa kuujuulisha wakati kitapo tokea ila mwenyewe Mwenyezi Mungu.
Kiungo
53:58
59
أَفَمِنْ هَـٰذَا ٱلْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ
Je! Mnayastaajabia maneno haya? [59]
Maelezo ya chini
[59] Hivyo nyinyi mnapinga kila la kweli? Na mnaistaajabia kwa kuikaataa hii Qur'ani?
Kiungo
53:59
60
وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ
Na mnacheka, wala hamlii? [60]
Maelezo ya chini
[60] Na mnacheka kwa kejeli na maskhaara, wala hamlii kama wafanyavyo wenye yakini,
Kiungo
53:60
61
وَأَنتُمْ سَـٰمِدُونَ
Nanyi mmeghafilika? [61]
Maelezo ya chini
[61] Nanyi mmo katika pumbao na kutakabari?
Kiungo
53:61
62
فَٱسْجُدُوا۟ لِلَّهِ وَٱعْبُدُوا۟ ۩
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu. [62]
Maelezo ya chini
[62] Basi msujudieni Mwenyezi Mungu aliye iteremsha Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu wote, na muabuduni Yeye tu peke yake Mwenye kutukuka kwa utukufu wake.
Kiungo
53:62