Sura ya 99 kati ya 114 · Madaniya

Sura Az-Zalzala (Tetemeko)

سُورَةُ الزَّلۡزَلَةِ
Aya 8

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
إِذَا زُلْزِلَتِ ٱلْأَرْضُ زِلْزَالَهَا
Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! [1]
Maelezo ya chini[1] Ikitisika ardhi kwa mtikiso mkubwa, na ikasukika kwa ukomo wa kutisika na kusukika kunako mkinika na ikaweza kuchukua!
Kiungo 99:1
2
وَأَخْرَجَتِ ٱلْأَرْضُ أَثْقَالَهَا
Na itakapo toa ardhi mizigo yake! [2]
Maelezo ya chini[2] Na ardhi ikatoa yote yaliomo katika ndani ya tumbo lake, ikiwa khazina au maiti walio kwisha zikwa!
Kiungo 99:2
3
وَقَالَ ٱلْإِنسَـٰنُ مَا لَهَا
Na mtu akasema: Ina nini? [3]
Maelezo ya chini[3] Na binaadamu akasema kwa kushtuka na khofu: Ardhi hii ina nini hata inatikisika hivi, na inatoa vilivyomo tumboni mwake, ndio Saa imefika?
Kiungo 99:3
4
يَوْمَئِذٍۢ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا
Siku hiyo itahadithia khabari zake. [4]
Maelezo ya chini[4] Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua,
Kiungo 99:4
5
بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا
Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! [5]
Maelezo ya chini[5] Kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.
Kiungo 99:5
6
يَوْمَئِذٍۢ يَصْدُرُ ٱلنَّاسُ أَشْتَاتًۭا لِّيُرَوْا۟ أَعْمَـٰلَهُمْ
Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! [6]
Maelezo ya chini[6] Siku hiyo watu watatoka makaburini mbio, nao wamo katika mtafaruku, wapate kuziona hisabu zao na malipo yao aliyo waahidi Mwenyezi Mungu.
Kiungo 99:6
7
فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًۭا يَرَهُۥ
Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! [7]
Maelezo ya chini[7] Basi mwenye kufanya hata kitu chenye uzito wa punje ya mchanga cha kheri ataiona katika daftari lake, na atapata malipo yake.
Kiungo 99:7
8
وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍۢ شَرًّۭا يَرَهُۥ
Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! [8]
Maelezo ya chini[8] Na mwenye kufanya shari ya uzito wa chembe ya mchanga ataiona kadhaalika, na atapata malipo yake. Wala Mola wako Mlezi hatamdhulumu yeyote.
Kiungo 99:8

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure