Sura ya 93 kati ya 114 · Makkiya

Sura Ad-Duha (Asubuhi)

سُورَةُ الضُّحَىٰ
Aya 11

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلضُّحَىٰ
Naapa kwa mchana! [1]
Maelezo ya chini[1] Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati wa uchangamfu na kazi!
Kiungo 93:1
2
وَٱلَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ
Na kwa usiku unapo tanda! [2]
Maelezo ya chini[2] Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake!
Kiungo 93:2
3
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. [3]
Maelezo ya chini[3] Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia.
Kiungo 93:3
4
وَلَلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌۭ لَّكَ مِنَ ٱلْأُولَىٰ
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. [4]
Maelezo ya chini[4] Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko mwanzo wake.
Kiungo 93:4
5
وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰٓ
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. [5]
Maelezo ya chini[5] Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa kheri za duniani na Akhera hata utaridhia.
Kiungo 93:5
6
أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًۭا فَـَٔاوَىٰ
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? [6]
Maelezo ya chini[6] Kwani hakukukuta wewe yatima unahitaji wa kukutunza naye akakupa makaazi ya kukuhifadhi kwa mwenye kukuangalia vyema kwa mambo yako?
Kiungo 93:6
7
وَوَجَدَكَ ضَآلًّۭا فَهَدَىٰ
Na akakukuta umepotea akakuongoa? [7]
Maelezo ya chini[7] Na akakuona umebabaika hukukinaika na itikadi zilizo kuzunguka, naye akakuongoa kwenye Njia ya Haki?
Kiungo 93:7
8
وَوَجَدَكَ عَآئِلًۭا فَأَغْنَىٰ
Akakukuta mhitaji akakutosheleza? [8]
Maelezo ya chini[8] Akakukuta fakiri wa mali naye akakutajirisha kwa kukupa riziki?
Kiungo 93:8
9
فَأَمَّا ٱلْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ
Basi yatima usimwonee! [9]
Maelezo ya chini[9] Ikiwa hii ndiyo hali yetu nawe, basi yatima usimdhili,
Kiungo 93:9
10
وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنْهَرْ
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! [10]
Maelezo ya chini[10] Na mwenye kuomba au kuuliza usimjibu kwa ukavu,
Kiungo 93:10
11
وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. [11]
Maelezo ya chini[11] Na ama neema za Mola wako Mlezi zitangaze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndio kudhihirisha neema.
Kiungo 93:11

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure