Sura ya 107 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Ma'un (Msaada Mdogo)

سُورَةُ المَاعُونِ
Aya 7

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo? [1]
Maelezo ya chini[1] Unamjua anaye kanusha malipo na hisabu ya Akhera?
Kiungo 107:1
2
فَذَٰلِكَ ٱلَّذِى يَدُعُّ ٱلْيَتِيمَ
Huyo ndiye anaye msukuma yatima, [2]
Maelezo ya chini[2] Ukitaka kumjua basi ni huyo ambaye anaye msukuma yatima kwa nguvu, na anamtumilia mabavu, na anamdhulumu,
Kiungo 107:2
3
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ
Wala hahimizi kumlisha masikini. [3]
Maelezo ya chini[3] Na wala hahimizi kulishwa masikini.
Kiungo 107:3
4
فَوَيْلٌۭ لِّلْمُصَلِّينَ
Basi, ole wao wanao swali, [4]
Maelezo ya chini[4] Maangamio yatawashukia wanao sali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.
Kiungo 107:4
5
ٱلَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ
Ambao wanapuuza Sala zao; [5]
Maelezo ya chini[5] Maangamio yatawashukia wanao swali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.
Kiungo 107:5
6
ٱلَّذِينَ هُمْ يُرَآءُونَ
Ambao wanajionyesha, [6]
Maelezo ya chini[6] Ambao huonyesha kwa watu vitendo vyao, ili wapate cheo katika nyoyo za hao watu, na wasifiwe.
Kiungo 107:6
7
وَيَمْنَعُونَ ٱلْمَاعُونَ
Nao huku wanazuia msaada. [7]
Maelezo ya chini[7] Na huku wanazuia hisani zao na msaada wao kwa watu
Kiungo 107:7

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure