Sura ya 106 kati ya 114 · Makkiya

Sura Quraysh (Makureshi)

سُورَةُ قُرَيۡشٍ
Aya 4

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
لِإِيلَـٰفِ قُرَيْشٍ
Kwa walivyo zoea Maqureshi, [1]
Maelezo ya chini[1] Hebu staajabuni kwa yanayo walazimu Makureshi! Kuwalazimu safari za musimu wa baridi kwenda Yaman,
Kiungo 106:1
2
إِۦلَـٰفِهِمْ رِحْلَةَ ٱلشِّتَآءِ وَٱلصَّيْفِ
Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto. [2]
Maelezo ya chini[2] Na safari za musimu wa joto kwenda Shamu, kufanya biashara na kutafuta riziki kwa utulivu na amani. (Hizo safari za biashara za Yaman ndizo zilizo waleta Waarabu Afrika Mashariki kwa maelfu ya miaka, na zikauleta Uislamu pande za Afrika kabla ya kuenea Arabuni. Kwani nchi za Afrika Mashariki zilikaliwa na Waarabu kwa maelfu ya miaka. Soma Periplus of the Erythrean Sea, na East Africa and Its Invaders ya Prof. Coupland, na vitabu vya Sir John Gray na Dr. L.W. Hollingsworth.)
Kiungo 106:2
3
فَلْيَعْبُدُوا۟ رَبَّ هَـٰذَا ٱلْبَيْتِ
Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii, [3]
Maelezo ya chini[3] Basi wamtakasie ibada Mola Mlezi wa Nyumba hii aliye wawezesha kuzifanya hizi safari mbili.
Kiungo 106:3
4
ٱلَّذِىٓ أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍۢ وَءَامَنَهُم مِّنْ خَوْفٍۭ
Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu. [4]
Maelezo ya chini[4] Ambaye anawalisha wasione njaa, na hali wao wamo katika bonde lisio na makulima, na akawalinda na khofu na watu wengine pembezoni mwao wananyakuliwa.
Kiungo 106:4

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure