Sura ya 97 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Qadr (Cheo Kitukufu)

سُورَةُ القَدۡرِ
Aya 5

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
إِنَّآ أَنزَلْنَـٰهُ فِى لَيْلَةِ ٱلْقَدْرِ
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. [1]
Maelezo ya chini[1] Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika usiku wa Cheo na Utukufu.
Kiungo 97:1
2
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا لَيْلَةُ ٱلْقَدْرِ
Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? [2]
Maelezo ya chini[2] Na kitu gani kitakufunza ni nini usiku huo wa Cheo na Utukufu?
Kiungo 97:2
3
لَيْلَةُ ٱلْقَدْرِ خَيْرٌۭ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍۢ
Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. [3]
Maelezo ya chini[3] Usiku wa Qadr na Sharaf, Cheo na Utukufu, ni bora kuliko miezi elfu, kwa kuwa umekhusika kwa kuteremka ndani yake Qur'ani tukufu.
Kiungo 97:3
4
تَنَزَّلُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍۢ
Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. [4]
Maelezo ya chini[4] Huteremka Malaika na Jibrili katika usiku huo mpaka kwenye ardhi kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa sababu ya kila jambo.
Kiungo 97:4
5
سَلَـٰمٌ هِىَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ ٱلْفَجْرِ
Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. [5]
Maelezo ya chini[5] Na wameaminika na maudhi na uovu. Hali inabaki hivyo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
Kiungo 97:5

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure