Sura ya 51 kati ya 114 · Makkiya

Sura Adh-Dhariyat (Pepo Zinazopeperusha)

سُورَةُ الذَّارِيَاتِ
Aya 60

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلذَّٰرِيَـٰتِ ذَرْوًۭا
Naapa kwa pepo zinazo tawanya! [1]
Maelezo ya chini[1] Ninaapa kwa pepo zinazo timua mawingu, zikayasukuma kwa nguvu, huku zikibeba mizigo mizito ya maji, zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu, zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.
Kiungo 51:1
2
فَٱلْحَـٰمِلَـٰتِ وِقْرًۭا
Na zinazo beba mizigo! [2]
Maelezo ya chini[2] Huku zikibeba mizigo mizito ya maji.
Kiungo 51:2
3
فَٱلْجَـٰرِيَـٰتِ يُسْرًۭا
Na zinazo kwenda kwa wepesi. [3]
Maelezo ya chini[3] Zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
Kiungo 51:3
4
فَٱلْمُقَسِّمَـٰتِ أَمْرًا
Na zinazo gawanya kwa amri! [4]
Maelezo ya chini[4] Zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.
Kiungo 51:4
5
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌۭ
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli! [5]
Maelezo ya chini[5] Hakika hayo mnayo ahidiwa, nayo ya kufufuliwa na mengineyo, ni hakika ya kweli itakayo tokea.
Kiungo 51:5
6
وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٌۭ
Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea. [6]
Maelezo ya chini[6] Na kwamba kwa yakini malipo kwa vitendo vyenu yatakuwa tu hapana hivi wala hivi.
Kiungo 51:6
7
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْحُبُكِ
Naapa kwa mbingu zenye njia! [7]
Maelezo ya chini[7] Ninaapa kwa mbingu zenye njia zilizo wekwa baraabara.
Kiungo 51:7
8
إِنَّكُمْ لَفِى قَوْلٍۢ مُّخْتَلِفٍۢ
Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana. [8]
Maelezo ya chini[8] Kwamba nyinyi msemapo mnayo yasema ni maneno ya kugongana.
Kiungo 51:8
9
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ
Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. [9]
Maelezo ya chini[9] Huacha kuamini hiyo ahadi ya kweli na malipo yatakayo kuwa huyo anaye acha, kwa sababu amekhiari kufuata pumbao la nafsi yake kuliko akili yake.
Kiungo 51:9
10
قُتِلَ ٱلْخَرَّٰصُونَ
Wazushi wameangamizwa. [10]
Maelezo ya chini[10] Wameteketea waongo wanao sema katika khabari za Kiyama kuwa ni mambo ya dhana na kukisia tu, ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini.
Kiungo 51:10
11
ٱلَّذِينَ هُمْ فِى غَمْرَةٍۢ سَاهُونَ
Ambao wameghafilika katika ujinga. [11]
Maelezo ya chini[11] Ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini.
Kiungo 51:11
12
يَسْـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلدِّينِ
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? [12]
Maelezo ya chini[12] Wanauliza kwa kejeli, kwa kuwa wanaona hayawi hayo: Lini itakuwa hiyo siku ya malipo?
Kiungo 51:12
13
يَوْمَ هُمْ عَلَى ٱلنَّارِ يُفْتَنُونَ
Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. [13]
Maelezo ya chini[13] Siku watapo simamishwa Motoni wakichomwa!
Kiungo 51:13
14
ذُوقُوا۟ فِتْنَتَكُمْ هَـٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تَسْتَعْجِلُونَ
Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza. [14]
Maelezo ya chini[14] Wataambiwa: Onjeni adhabu yenu hii ambayo duniani mlikuwa mkiihimiza iwe.
Kiungo 51:14
15
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍۢ وَعُيُونٍ
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. [15]
Maelezo ya chini[15] Hakika walio mt'ii Mwenyezi Mungu na wakamkhofu watakuwa wananeemeka katika Mabustani na chemchem za Peponi ambazo haziwezi kusifika hakika yake.
Kiungo 51:15
16
ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ
Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. [16]
Maelezo ya chini[16] Wakipokea thawabu na takrima wanazo pewa na Mola wao Mlezi. Hakika hao kabla ya hapo walikuwa duniani ni wenye kufanya mambo mazuri kwa kutimiza waliyo takiwa wayafanye.
Kiungo 51:16
17
كَانُوا۟ قَلِيلًۭا مِّنَ ٱلَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ
Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. [17]
Maelezo ya chini[17] Walikuwa kulala kwao usiku ni kuchache, na wakikesha sana kwa ibada.
Kiungo 51:17
18
وَبِٱلْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. [18]
Maelezo ya chini[18] Na mwishoni mwa usiku walikuwa wakiomba maghfira.
Kiungo 51:18
19
وَفِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّۭ لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. [19]
Maelezo ya chini[19] Na katika mali yao wakiweka fungu maalumu lilio thibiti kwa ajili ya wenye haja, wanao omba na wanao jizuilia kuomba kwa kujiteta.
Kiungo 51:19
20
وَفِى ٱلْأَرْضِ ءَايَـٰتٌۭ لِّلْمُوقِنِينَ
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. [20]
Maelezo ya chini[20] Na katika ardhi zipo dalili nyingi zilizo wazi zinazo pelekea yakini, kwa mwenye kuitafuta njia.
Kiungo 51:20
21
وَفِىٓ أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? [21]
Maelezo ya chini[21] Na hali kadhaalika katika nafsi zenu zipo Ishara zilizo wazi. Je! Mmeghafilika nazo, hamzioni?
Kiungo 51:21
22
وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ
Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. [22]
Maelezo ya chini[22] Na katika mbingu ipo amri ya riziki zenu na kukadiriwa mnayo ahidiwa.
Kiungo 51:22
23
فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِنَّهُۥ لَحَقٌّۭ مِّثْلَ مَآ أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. [23]
Maelezo ya chini[23] Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi kwamba hakika yote hayo mnayo yakanya kuwa, yaani kufufuliwa, kulipwa, kuadhibiwa wanao kadhibisha, na kuwalipa thawabu wachamngu, yote hayo bila ya shaka ni ya kweli thaabiti kama hivyo kusema kwenu ambako hamna shaka nako kuwa mnasema.
Kiungo 51:23
24
هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَٰهِيمَ ٱلْمُكْرَمِينَ
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? [24]
Maelezo ya chini[24] Unakijua kisa cha Malaika, wageni wa hishima wa Ibrahim? Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Kiungo 51:24
25
إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَقَالُوا۟ سَلَـٰمًۭا ۖ قَالَ سَلَـٰمٌۭ قَوْمٌۭ مُّنكَرُونَ
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. [25]
Maelezo ya chini[25] Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Kiungo 51:25
26
فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجْلٍۢ سَمِينٍۢ
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. [26]
Maelezo ya chini[26] Akenda kwa mkewe naye ana khofu, akaja na ndama aliye nona.
Kiungo 51:26
27
فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? [27]
Maelezo ya chini[27] Akawakaribisha, nao hawakula. Akasema kwa kuto wajua hakika yao: Mbona hamli?
Kiungo 51:27
28
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةًۭ ۖ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَـٰمٍ عَلِيمٍۢ
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. [28]
Maelezo ya chini[28] Akahisi katika nafsi yake khofu kuwaogopa. Wakasema: Usiogope. Na wakampa bishara kuwa atapata mwana mwenye ilimu nzuri.
Kiungo 51:28
29
فَأَقْبَلَتِ ٱمْرَأَتُهُۥ فِى صَرَّةٍۢ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌۭ
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! [29]
Maelezo ya chini[29] Akatokea mkewe akipiga kelele alipo isikia ile bishara, akijipiga uso wake kwa mkono wake, kwa kuona muhali hayo na kustaajabu, na akasema: Mimi ni kizee, na tasa. Itakuwaje nizae?
Kiungo 51:29
30
قَالُوا۟ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْعَلِيمُ
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. [30]
Maelezo ya chini[30] Wakasema: Hivyo ndivyo alivyo kwisha hukumu Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima katika kila anayo hukumu, ni Mwenye ujuzi ambaye hapana linalo fichikana kwake lolote.
Kiungo 51:30
31
۞ قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا ٱلْمُرْسَلُونَ
AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa? [31]
Maelezo ya chini[31] Ibrahim akasema: Mna kazi gani tena baada ya khabari hii nzuri, enyi wajumbe?
Kiungo 51:31
32
قَالُوٓا۟ إِنَّآ أُرْسِلْنَآ إِلَىٰ قَوْمٍۢ مُّجْرِمِينَ
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu, [32]
Maelezo ya chini[32] Wakasema: Kwa hakika sisi tumetumwa kwa kaumu iliyo pita kiasi katika uasi,
Kiungo 51:32
33
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةًۭ مِّن طِينٍۢ
Tuwatupie mawe ya udongo, [33]
Maelezo ya chini[33] Tuwatupie mawe ya udongo, ambayo hapana anaye yajua yalivyo ila Mwenyezi Mungu.
Kiungo 51:33
34
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ
Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka. [34]
Maelezo ya chini[34] Mawe hayo ni makhsusi na maalumu kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka katika mambo machafu.
Kiungo 51:34
35
فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini. [35]
Maelezo ya chini[35] Basi tukahukumu tuwatoea kwenye mji huo walio amini.
Kiungo 51:35
36
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍۢ مِّنَ ٱلْمُسْلِمِينَ
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! [36]
Maelezo ya chini[36] Lakini hatukukuta ila nyumba moja tu ndiyo ya Waislamu.
Kiungo 51:36
37
وَتَرَكْنَا فِيهَآ ءَايَةًۭ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. [37]
Maelezo ya chini[37] Na katika mji huo tumeacha alama ya maangamizo ya watu wake, ili wapate kuzingatia wanayo ikhofu adhabu chungu.
Kiungo 51:37
38
وَفِى مُوسَىٰٓ إِذْ أَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَـٰنٍۢ مُّبِينٍۢ
Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi. [38]
Maelezo ya chini[38] Na katika kisa cha Musa yapo mawaidha. Tulipo mtuma kwa Firauni, na tukatilia nguvu kwa kumpa ushahidi ulio wazi.
Kiungo 51:38
39
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِۦ وَقَالَ سَـٰحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌۭ
Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! [39]
Maelezo ya chini[39] Firauni akapuuza kumuamini Musa kwa kutegemea ati nguvu zake. Akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
Kiungo 51:39
40
فَأَخَذْنَـٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذْنَـٰهُمْ فِى ٱلْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌۭ
Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. [40]
Maelezo ya chini[40] Tukamchukua yeye na hao anao jitapia kwao, tukawatumbukiza baharini, naye ni mwenye kuyatenda hayo ya ukafiri na inda anayo laumiwa kwayo.
Kiungo 51:40
41
وَفِى عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلْعَقِيمَ
Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi. [41]
Maelezo ya chini[41] Na katika kisa cha A'di yamo mawaidha pia. Tulipo wapelekea upepo usio kuwa na kheri yoyote.
Kiungo 51:41
42
مَا تَذَرُ مِن شَىْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَٱلرَّمِيمِ
Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka. [42]
Maelezo ya chini[42] Upepo huo haupiti kwa kitu chochote ila hukiacha kama fupa lilio nyambuka.
Kiungo 51:42
43
وَفِى ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا۟ حَتَّىٰ حِينٍۢ
Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. [43]
Maelezo ya chini[43] Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu.
Kiungo 51:43
44
فَعَتَوْا۟ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ
Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona. [44]
Maelezo ya chini[44] Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu. Wakajivuna na wakatakabari wasifuate amri ya Mola wao Mlezi. Basi radi ikawaangamiza nao wanaiona kwa macho yao inavyo tokea.
Kiungo 51:44
45
فَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ مِن قِيَامٍۢ وَمَا كَانُوا۟ مُنتَصِرِينَ
Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea. [45]
Maelezo ya chini[45] Basi hawakuweza kuinuka. Wala hawakuweza kujipigania kuijikinga na adhabu.
Kiungo 51:45
46
وَقَوْمَ نُوحٍۢ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًۭا فَـٰسِقِينَ
Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu. [46]
Maelezo ya chini[46] Na kaumu ya Nuhu tuliihiliki kabla ya hawa. Hakika hao walikuwa watu walio toka nje ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.
Kiungo 51:46
47
وَٱلسَّمَآءَ بَنَيْنَـٰهَا بِأَيْي۟دٍۢ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. [47]
Maelezo ya chini[47] Na mbingu tumeipanga kwa nguvu, na bila ya shaka Sisi ni waweza zaidi ya hayo.
Kiungo 51:47
48
وَٱلْأَرْضَ فَرَشْنَـٰهَا فَنِعْمَ ٱلْمَـٰهِدُونَ
Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! [48]
Maelezo ya chini[48] Na ardhi tumeikunjua, na Sisi ni wenye kuitengeneza vizuri kama kitanda. Aya hii tukufu inaashiria maana za kitaalamu nyingi; miongoni mwazo ni kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameumba ulimwengu huu mkunjufu kwa nguvu. Na Yeye ni Muweza kwa atakayo. Na maana ya mbingu katika Aya hii ni kila kilicho juu ya kitu na kikakifunika. Basi kila kilicho zunguka sayari na nyota na mkusanyiko wa jua katika sehemu hii inayo onekana ya ulimwengu kimetanda kupita inavyo kadirika na akili, wala haiwezi kupimika. Kwani masafa yao hukisiwa kwa mamilioni ya miaka ya mwangaza. Na mwaka mmoja wa mwangaza kwa ilivyo thibiti kwa ilimu za kisasa katika karne hii ya ishirini ni masafa yanayo kwenda mwangaza kwa mbio za kilomita 300,000 kwa nukta moja ya dakika. Na ibara ya Aya tukufu (Na hakika Sisi ndio twenye kuutanua) inaashiria hayo, yaani kutanda huko kwa ulimwengu kunako staajabisha tangu kuumbwa kwake. Kama vile vile kuwa kukunjuka huko kungali kunaendelea, na hayo sayansi ya sasa imethibitisha vile vile. Na imejuulikana kwa nadhariya ya kutanda ambayo katika mwanzo mwanzo wa karne hii imethibiti kuwa ni kweli kiilimu, na ufupi wake ni kuwa ulimwengu unaendelea kukua na kupanuka, na kila sayari za mbinguni zinajitenga wenyewe kwa wenyewe.
Kiungo 51:48
49
وَمِن كُلِّ شَىْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. [49]
Maelezo ya chini[49] Na kila kitu tumekiumba namna mbili, yaani kwa jozi, ili mpate kukumbuka muuamini uwezo wetu.
Kiungo 51:49
50
فَفِرُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ ۖ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌۭ مُّبِينٌۭ
Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. [50]
Maelezo ya chini[50] Basi fanyeni haraka kuendea kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.
Kiungo 51:50
51
وَلَا تَجْعَلُوا۟ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ ۖ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌۭ مُّبِينٌۭ
Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. [51]
Maelezo ya chini[51] Wala msimfanye mungu mwengine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nimekujieni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kukuonyeni kwa uwazi matokeo ya ushirikina.
Kiungo 51:51
52
كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا۟ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. [52]
Maelezo ya chini[52] Hivyo ndivyo ilivyo kuwa hali ya mataifa yote kwa Mitume wao. Hakuja Mtume kwa watu wa kabla ya kaumu yako ila walimwita: Mchawi au mwendawazimu.
Kiungo 51:52
53
أَتَوَاصَوْا۟ بِهِۦ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌۭ طَاغُونَ
Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi. [53]
Maelezo ya chini[53] Je! Mmeusiana, mmeambizana, nyinyi kwa nyinyi kusema hivyo ndio maana mnalirejea hilo kwa hilo? Bali hao ni watu walio pindukia mipaka, ndio wakawafikiana katika kuwashutumu Mitume!
Kiungo 51:53
54
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٍۢ
Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. [54]
Maelezo ya chini[54] Basi wapuuzilie mbali hawa wenye inda! Wewe hulaumiki usipo wajibu kitu.
Kiungo 51:54
55
وَذَكِّرْ فَإِنَّ ٱلذِّكْرَىٰ تَنفَعُ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. [55]
Maelezo ya chini[55] Wewe dumisha kukumbusha, kwani ukumbusho huwazidisha Waumini kufumbua macho na kuwa na nguvu za yakini.
Kiungo 51:55
56
وَمَا خَلَقْتُ ٱلْجِنَّ وَٱلْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. [56]
Maelezo ya chini[56] Wala sikuwaumba majini na watu kwa jambo la kuniletea Mimi manufaa, bali ili waniabudu, na kuniabudu Mimi ni manufaa kwao.
Kiungo 51:56
57
مَآ أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍۢ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ
Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. [57]
Maelezo ya chini[57] Sitaki kwao riziki, kwani Mimi si mhitaji kwa walimwengu wote; wala sitaki wanilishe, kwani Mimi ndiye ninaye lisha, wala silishwi.
Kiungo 51:57
58
إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلْقُوَّةِ ٱلْمَتِينُ
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. [58]
Maelezo ya chini[58] Hakika Mwenyezi Mungu peke yake, ndiye mdhamini wa kuwapa riziki waja wake, na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Aliye imara, hashindiki.
Kiungo 51:58
59
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ذَنُوبًۭا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَـٰبِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ
Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. [59]
Maelezo ya chini[59] Hakika hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na kukanusha wana fungu lao la adhabu mfano wa fungu la wenzao katika kaumu zilizo kwisha pita. Basi wasifanye haraka kuhimiza adhabu ishuke kabla ya wakati wake.
Kiungo 51:59
60
فَوَيْلٌۭ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن يَوْمِهِمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ
Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa. [60]
Maelezo ya chini[60] Basi maangamio yatawapata wenye kuikataa siku yao waliyo ahidiwa, kwa sababu ya shida na vitisho viliomo katika siku hiyo.
Kiungo 51:60

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure