Sura ya 114 kati ya 114 · Makkiya

Sura An-Nas (Wanadamu)

سُورَةُ النَّاسِ
Aya 6

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ
Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, [1]
Maelezo ya chini[1] Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha mambo yao.
Kiungo 114:1
2
مَلِكِ ٱلنَّاسِ
Mfalme wa wanaadamu, [2]
Maelezo ya chini[2] Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote wafalme wao na maraia.
Kiungo 114:2
3
إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ
Mungu wa wanaadamu, [3]
Maelezo ya chini[3] Mungu wa wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa ukamilifu atakavyo.
Kiungo 114:3
4
مِن شَرِّ ٱلْوَسْوَاسِ ٱلْخَنَّاسِ
Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, [4]
Maelezo ya chini[4] Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma ukiomba msaada kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake.
Kiungo 114:4
5
ٱلَّذِى يُوَسْوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ
Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, [5]
Maelezo ya chini[5] Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.
Kiungo 114:5
6
مِنَ ٱلْجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ
Kutokana na majini na wanaadamu. [6]
Maelezo ya chini[6] Kutokana na majini na wanaadamu.
Kiungo 114:6

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure