Sura ya 111 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Masad (Kamba ya Mtende)

سُورَةُ المَسَدِ
Aya 5

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
تَبَّتْ يَدَآ أَبِى لَهَبٍۢ وَتَبَّ
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. [1]
Maelezo ya chini[1] Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.
Kiungo 111:1
2
مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ
Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. [2]
Maelezo ya chini[2] Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma.
Kiungo 111:2
3
سَيَصْلَىٰ نَارًۭا ذَاتَ لَهَبٍۢ
Atauingia Moto wenye mwako. [3]
Maelezo ya chini[3] Ataingia katika Moto unao waka, aungue.
Kiungo 111:3
4
وَٱمْرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلْحَطَبِ
Na mkewe, mchukuzi wa kuni, [4]
Maelezo ya chini[4] Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).
Kiungo 111:4
5
فِى جِيدِهَا حَبْلٌۭ مِّن مَّسَدٍۭ
Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. [5]
Maelezo ya chini[5] Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.
Kiungo 111:5

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure