Sura ya 103 kati ya 114 · Makkiya

Sura Al-Asr (Zama)

سُورَةُ العَصۡرِ
Aya 3

Tafsiri ya maana: Ali Mohsin Al-Barwani, QuranEnc.com, toleo 1.0.1. Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani. Qur'ani yenyewe ni maandishi ya Kiarabu.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1
وَٱلْعَصْرِ
Naapa kwa Zama! [1]
Maelezo ya chini[1] Naapa kwa Zama kwa sababu ya maajabu mengi na mazingatio yaliomo ndani yake.
Kiungo 103:1
2
إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ لَفِى خُسْرٍ
Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara, [2]
Maelezo ya chini[2] Hakika kila binaadamu bila ya shaka yumo katika namna fulani au fulani ya kukhasiri, kwa mujibu wa anavyo ghilibiwa na pumbao na matamanio.
Kiungo 103:2
3
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلْحَقِّ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلصَّبْرِ
Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri. [3]
Maelezo ya chini[3] Isipo kuwa wale walio muamini Mwenyezi Mungu na wakatenda mema, na wakadumu juu ya ut'iifu, na wakasemezana na kuusiana kwa kushikamana na Haki, kwa itikadi, na maneno, na vitendo. Na wakausiana wasubiri na wavumilie mashaka yanayo wapata wenye kushikamana na Dini. Basi hao ndio wenye kusalimika na hiyo khasara, wenye kufanikiwa duniani na Akhera.
Kiungo 103:3

Soma na usikilize kila siku kwenye programu ya Niyat, pamoja na nyakati za swala, kibla na mahali ulipofikia.

Pata Niyat bure